Papa anamkumbuka kwa hisia ya upendo kwa Rais Mstaafu wa Italia Bwana Napoletano aliyeaga dunia Septemba 20. Papa anamkumbuka kwa hisia ya upendo kwa Rais Mstaafu wa Italia Bwana Napoletano aliyeaga dunia Septemba 20.  (AFP or licensors)

Papa atuma salamu za rambi kufuatia na kifo cha Rais Mstaafu wa Italia

Katika telegramu kwa mkewe Rais Mtaafu Napoletano,Papa anakumbuka mtazamo wake katika kufanya chaguzi muhimu kwa ajili ya maisha ya nchi.Papa Francisko katika katekesi yaJumatano 20 Septemba iliyopita aliwaalika waamini kutoa wazo na sala kwa rais mstaafu wa Jamhuri ya Italia, akimfafanua kama "mtumishi wa nchi."

Na Angella Rwezaula, - Vatican

Papa Francisko ametuma Telegramu kifuatia na Kifo cha Rais Mstaafu Giorgio Napoletano wa  Jamhuri ya Italia akimwelekea mama mjane kilichotokea tarehe 22 Septemba 2023. Giorgio Napolitano, rais wa zamani wa Jamhuri ya Italia. Alikuwa na umri wa miaka 98 na alilazwa katika zahanati ya ‘Salvator Mundi’ jijini Roma. Hali yake ya kiafya ilizidi kuwa mbaya katika siku za hivi karibuni, kiasi kwamba Papa Francisko katika katekesi yake Jumatano 20 Septemba iliyopita aliwaalika waamini kutoa wazo na sala kwa rais mstaafu wa Jamhuri ya Italia, akimfafanua kama "mtumishi wa nchi. "

Baba Mtakatifu kwa hiyo katika telegramu hiyo anabainisha kwamba kuondoka kwa mme wake, rais Mstaafu, kumeibua ndani mwake hisia za uchungu na wakati huo huo za shukrani kwa mwanaume huyo wa Serikali ambaye katika kujikita kwenye majukumu ya ngazi za juu za kitaasisi, alionesha sifa kubwa za akili na shauku ya dhati katika maisha ya kisiasa ya Italia pamoja na kuweka maslahi ya hatima ya mataifa. Aidha Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe huo anabainisha jinsi alivyo na kumbu kumbu za shukrani kwa mikutano binafsi aliyopata kukutana naye, wakati ambapo aliweza kumpongeza kwa ubinadamu  na mtazamo wa mbele katika kufanya chaguzi muhimu kwa haki, hasa katika wakati muhimu wa maisha ya nchi, kwa nia daima ya kuendeleza umoja na makubalino, katika roho ya mshikamano, inayohuishwa na kutenda mema ya kawaida. Baada ya kutaja sifa hizo, Baba Mtakatifu Francisko katika telegramu hiyo anageukia familia ya marehemu kuwa: “Ninapenda kutoa ukaribu wangu kwako, watoto na familia yako, nikiwahakikisha kuwakumbuka katika maombi. Kwa kuwapatia rambi rambi zangu, ninaomba juu yetu wapendwa faraja katika moyo.

Kwa upande wake, Rais wa sasa wa Jamhuri ya Italia Bwana Sergio Mattarella mara baada ya kupata habari hizo, alitoa taarifa ambayo alielezea masikitiko yake makubwa na hisia za Jamhuri ya shukrani kwa kumbukumbu ya Napoletano na Taifa la rambirambi kwa familia yake. Sehemu kubwa ya historia ya nusu yjanga  zake, utata wake, malengo yake, matumaini yake anaandika  Mattarella akikumbusha  kwamba tangu ujana wake kwa kufahamiana na mazingira ya kiutamaduni ya Neapolitana alishikamana na sababu ya kupinga ufashisti na harakati za kikomunisti, huku akijitolea kwa maendeleo ya Kusini mwa Italia na  tabaka la kijamii za  chini, hadi kazi iliyoaminika ya uimarishaji wa maadili.

Papa na rambi rambi kwa kifo cha Rais Mstaafu wa Italia
23 September 2023, 16:56