Kimbunga kikali na mvua kilipitia nchini Brazil na kusababisha vifo vingi. Papa amewakumbuka kwa sala zake. Kimbunga kikali na mvua kilipitia nchini Brazil na kusababisha vifo vingi. Papa amewakumbuka kwa sala zake. 

Papa atuma Salamu za rambi rambi nchini Brazil

Papa ametuma salamu za rambi rambi kufuatia na waathirika wa mafuriko na kimbunga kikali katika Serikali ya Rio Grande nchini Brazil.Katika salamu hizo zilizotiwa sahini na Kardinali Pietro Parolin,Katibu wa Vatican,Papa anaonesha ukaribu wake kwa waliokumbwa na mkasa huo.Zaidi ya watu 40 wamekufa na wengine zaidi ya 50 kupotea.

Vatican News

Mshikamano na sala zilioneshwa na  Baba Mtakatifu Francisko katika telegramu iliyotiwa saini na Kardinali, Pietro Parolin, Katibu wa Vatican  iliyotumwa kwa Askofu Mkuu  Leomar Brustolin, wa Jimbo Kuu Katoliki la Mtakatifu  Maria na rais wa Kanda ya Kusini ya 3 ya Baraza la Maaskofu wa Brazil kutokana na mvua kubwa iliyonyesha katika jimbo la Rio Grande katika siku za hivi karibuni na kuacha nyuma yake uharibifu na vifo. Kwa hiyo, Baba Mtakatifu kwa kujali kwake  amewabariki watu wote walioathiriwa na mafuriko makubwa, na anawahakikishia  sala na  maombi ya haki kwa pumziko la milele kwa wale wote waliopoteza maisha yao na vile vile majeruhi waliopoteza nyumba, huku akitumaini kwamba ujenzi upya wa maeneo hayo utafanyika haraka na kwa ufanisi.”

Idadi ya waathrika inaongezeka

Wakati huo huo, idadi ya vifo kutokana na kimbunga kilichopiga kusini mwa Brazil Jumatatu  tarehe 4 Septemba 2023  bado kinaendelea kuongezeka. Mamlaka za nchi hiyo zinazungumza kuhusu watu 41 waliofariki, 46 hawajulikani walipo na 223 kujeruhiwa. Misako inaendelea  na zaidi kuona juu ya  usalama wa raia wa Jimbo la Rio Grande do Sul  ambapo  jumla ya watu elfu 11 wamelazimika kuacha makazi yao. Majengo mengi yaliharibiwa na miji ikafurika, huku manispaa 87 zikiathirika kwa jumla.

09 September 2023, 15:22