Tafuta

Mongolia:Mkurugenzi ya Nyumba ya Huruma amshukuru Papa

Bruda Andrew Tran aliwasilisha mpango wa upendo katikati ya mji mkuu wa Mongolia ambao Papa Francisko aliutembelea na kuubariki.Ni Jengo la ghorofa tatu tayari kuwakaribisha wahamiaji,wasio na makazi,walemavu,waathirika wa unyanyasaji wa nyumbani.Kuna pia kliniki ya matibabu ndani.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Kila kitu kimekuwa tayari kwa Juma moja kama vile  jikoni, vyumba vya kulala, kuta za rangi ya bluu na katika mchoro wa sura ya njiwa nyeupe, hata kliniki ya ndani. Bamba la dhahabu pekee lililopewa jina la Papa Francisko ndilo lililokosekana. Baba Mtakatifu Francisko mwenyewe alizindua Jengo hilo tarehe 4 Septemba 2023, hivyo hiyo Nyumba ya Huruma katikati ya mji mkuu Ulaanbaatar, katika wilaya ya Bayangol, ambayo ilikuwa ni kitendo cha mwisho cha ziara yake ya kitume Nchini Mongolia. Ni Jengo  lililotengenezwa lenye ghorofa tatu ambazo Papa Francisko mara baada ya kukutana na mashirika ya upendo wa Mongolia, alitaka kutembelea kabla ya kurudi Roma ambapo aliona vyumba mbalimbali na kuwasalimu mmoja baada ya mwingine vijana wagonjwa walioimba pamoja na wimbo uliotungwa wakati wa ziara hiyo. “Nyumba ya Huruma” itatoa makazi, hata ya muda kwa maskini, wagonjwa, wasio na makazi, wahamiaji, au waathirika wa wa unyanyasaji wa nyumbani.

Papa wakati wa kukutana na wahudumu wa upendo
Papa wakati wa kukutana na wahudumu wa upendo

Hii ni kwa sababu wale wanaume na wanawake wote ambao wamepata taabu na kuteseka papo hapo katika familia pia wanabisha kwenye mlango wa Nyumba ya Huruma. Alieleza Bruda  Andrew, Mkurugeniz wa Kituo hicho na kwamba “Watu wengi, wanaondoka kwa sababu ya makosa ya familia zao au kwa sababu wamepoteza familia. Wengine wengi wana familia, lakini wametengana kutokana na matatizo mbalimbali. Shughuli yao wanajaribu kuwaunganisha tena, ili kuwarudisha katika jamii, hasa wazee, watoto na wanawake waathiriwa wa unyanyasaji wa nyumbani, na kwa njia hiyo hiyo wanajaribu kuwasaidia watu ambao ni walevi kuwapa nguvu na kuwasaidia kupona kutoka kwa utumwa huo” Andrew Tran Le Phuong,  mkurugenzi  wa kituo hicho aliwaambia waandishi wa habari wa Vatican kuhusiana na jengo hilo ambalo wamshirikisnao katika maandalizi ya ziara ya Papa nchini Mongolia. Kikweli makao hayo sio kimbilo laki itakuwa nyumba ya kweli ya watu kwa sababu wakati wa baridi nyumba yenyewe ni baridi sana”. Kwa hiyo Papa Fransisko alitembelea  ghorofa ya kwanza ya jengo hilo, pia akimweleza Papa mwanzo wa mpango huu uliozaliwa kwa msukumo wa Kanisa la mahali hapo na Kardinali Giorgio Marengo, Balozi wa Vatican , na iliyoko katika shule ya zamani ambayo hapo awali ilikuwa nyumba ya  Masista wa Hospitali ya Mtakatifu Paulo wa Chartres.

Shukrani kwa msaada wa kurugenzi ya kitaifa ya Mashirika ya Kimisionari ya Kipapa ya Australia, Utume wa Kikatoliki na usaidizi wa polisi wa eneo hilo na wafanyakazi wa kijamii wa wilaya hiyo, ghorofa tatu za nyumba hiyo zitakaribisha ubinadamu wote waliojeruhiwa ambao wanaishi katika mji mkuu wa Mongolia. Bruda Andre aidha alisema msaada unaofanywa na watawa, mapadre na watu wa kujitolea pia hutolewa kwa wale ambao, kwa mfano, wamepoteza kitambulisho chao na hivyo hawawezi kufikia mfumo wa afya au serikali. Wanawasaidia kujiandikisha upya ili waweze kupata bima ya afya katika mfumo wa umma, ili kuwasaidia kurejea katika hali ya kawaida”, alifafanua Padre Andrew na kusisitiza kuwa, kwa sasa hakuna utabiri wa idadi ya watu watakaopatikana aliwahi. Kwa ujumla katika hotuba yake Bruda Andre  alisema kwamba:“Asante kwa kuwa hapa leo na karibu katika Nyumba ya Huruma. Uwepo wako unaonesha msaada wako kwa kazi hii ya kutoa uhai. Nyumba ya Huruma imejitolea kuwafikia wale ambao kwa namna fulani wanahisi kuwa pembezoni mwa jamii. Tumeunda nyumba ambayo watu wote wanakaribishwa. Matarajio yetu ni kujenga makazi ya watu wanaoishi katika mazingira magumu, hasa wanawake na watoto, ili wakusanyike katika mazingira ya upendo na kujisikia kuthaminiwa, salama na amani. Nyumba pia inafanya kazi kama kituo cha huduma ya kwanza kwa wasio na makazi.

Salamu kwa Papa na uwakilishi wa shughuli za upendo
Salamu kwa Papa na uwakilishi wa shughuli za upendo

Tunajaribu tuwezavyo kusaidia watu kupata ufikiaji wa kile wanachohitaji, iwe ni kurejesha kile wanachostahili au kuunganishwa tena na familia zao wakati wa shida. Tunawapa wale wanaohitaji vifaa vya kufulia na kuoga bila malipo, chakula cha kimsingi na nguo ikihitajika. Zaidi ya yote, tunahakikisha kwamba daima kuna mtu wa kuzungumza nao, mtu ambaye ameketi tu na kusikiliza kwa neema yeyote anayekuja na kubisha mlango. Maono ya awali ya Mwadhama Kardinali Giorgio Marengo yalikuwa ni kuunda kituo ambapo taasisi zote za Kanisa zinazohudumu katika maeneo ya haki ya kijamii na huduma kwa waliojeruhiwa zingeweza kuja pamoja na kuwa ukweli. Kwa njia hii, ingekuwa mchango wa kawaida na wa kweli wa Kanisa fulani huko Mongolia. Sisi, katika Nyumba ya Huruma, tunatafuta kuunganishwa na wale wote wanaoshiriki maadili ya huruma ya upendo na uwajibikaji wa kijamii wa pamoja, katika roho ya sinodi. Tukirejea yale ambayo Baba Mtakatifu  umesema mara kadhaa, tungependa kuwa upande wa wale “wasio na haki ya kusema au kutosikilizwa”. Nyumba ya Huruma ni mahali pa kutia moyo. Kwa pamoja tunatumai kujenga ulimwengu tofauti katika roho ya umoja na huruma. Tunaondoa vizuizi kupitia kazi ya kujitolea ya kidini, inayolenga jamii. Katika roho hii, tunavuka "mipaka ya tofauti", kufikia wale ambao mara nyingi hupuuzwa. Baba Mtakatifu, wakati wako pamoja nasi nchini Mongolia unapokaribia mwisho, tunapenda kukushukuru. Pia tunatazamia kuendelea na safari hii ya kutumaini pamoja" kwa mustakabali wenye umoja na angavu kwa watu wa Mongolia.

 

04 September 2023, 09:05