Papa Francisko anaonya dhidi ya itikadi katika Kanisa na ulimwengu

Katika mazungumzo yake na waandishi wa habari waliokuwa kwenye ndege ya kurudi kutoka Mongolia,Papa Francisko alizungumzia mada mbalimbali,ikiwa ni pamoja na Mkutano Mkuu ujao wa Sinodi.Amefafanua juu ya matamshi yake ya hivi karibuni na vijana katoliki wa Urussi kuwa alitoa mwaliko kwao kutosahau urithi wao wa kiutamaduni.

Vatican News.

Jumatatu tarehe 4 Septemba 2023, Baba Mtakatifu Francisko alifanya mkutano wake na waandishi wa habari kama utamaduni wa kila anapokuwa anakwenda au kurudi katika kila ziara yake na hivyo  katika muktadha huu kwa  waliokuwa wakisafiri naye kwa ndege wakati wa kurejea Roma kutoka nchini Mongolia katika ziara yake ya 43 ya kitume iliyoanza tangu tarehe 31 Agosti 2023. Maswali yaliyoulizwa yalikuwa na mada kadhaa, kuanzia na swali kutoka kwa mwandishi wa habari wa taifa lililokuwa mwenyeji wa ziara yake ya kitume huko  Mongolia. Kwa hiyo yafuatayo ni maswali na majibu kwa lugha ya kiswahili kuhusu mkutano huo na Waandishi wa habari:

Jargalsaikhan Dambadarjaa (Gazeti la Defacto): Asante sana, Baba Mtakatifu, kwa kutembelea Mongolia. Swali langu ni nini lengo lako kuu na ziara hii na umeridhika na matokeo yaliyopatikana?

Papa Francisko: Wazo la kutembelea Mongolia lilinijia nikifikiria kuhusu jumuiya ndogo ya Wakatoliki. Ninafanya safari hizi kutembelea jumuiya za Kikatoliki na pia kuingia katika mazungumzo na historia na utamaduni wa watu, na mafumbo ya watu. Ni muhimu kwamba uinjilishaji usichukuliwe kama ugeuzaji imani. Uongofu siku zote huzuia. Papa Benedikto alisema kwamba imani haikui kwa kugeuza watu imani, bali kwa kuvutiwa. Utangazaji wa Injili unaingia katika mazungumzo na utamaduni. Kuna uinjilishaji wa utamaduni na pia utamadunisho wa Injili, kwa sababu Wakristo pia huonesha maadili yao ya Kikristo na utamaduni wa watu wao wenyewe. Hii ni kinyume cha ukoloni wa kidini. Kwangu mimi, safari ilikuwa ni kufahamiana na watu wa Mongolia, kuingia katika mazungumzo nao, kupokea utamaduni wao, na kulisindikiza Kanisa katika safari yake kwa heshima kubwa kwao na kwa utamaduni wao. Nimeridhika na matokeo.

Ulambadrakh Markhaakhuu (ULS Suld Tv): Leo, mzozo kati ya ustaarabu unaweza tu kutatuliwa kwa mazungumzo, kama wewe, Baba Mtakatifu ulisema. Je, Ulaanbaatar inaweza kujitoa kama jukwaa la mazungumzo ya kimataifa kati ya Ulaya na Asia?

Papa Francisko: Ninafikiri hivyo. Kuna kitu cha kufurahisha sana, ambacho pia kinapendelea mazungumzo haya, ninajiruhusu kuyaita 'mystique ya tatu ya jirani'. Unafikiri kwamba Ulaanbaatar ni mji mkuu wa nchi iliyo mbali zaidi na bahari, na tunaweza kusema kwamba ardhi yao iko kati ya madola makubwa mawili, Urussi na China. Ndio maana fumbo lao ni kujaribu kufanya mazungumzo hata na 'majirani zao wa tatu': sio kwa dharau katika wawili hawa, kwa sababu wana uhusiano mzuri na wote wawili, lakini kwa shauku ya ulimwengu wote, ili kuonesha maadili yao kwa watu wote, dunia nzima, na pia kupokea kutoka kwa wengine maadili yao ili kuingia katika mazungumzo. Inashangaza kwamba, katika historia, katika kwenda kutafuta ardhi nyingine mara nyingi kulichanganyikiwa na ukoloni, au na wazo la kuingia kutawala…daima. Badala yake, wewe, kwa fumbo hilo la jirani wa tatu, una falsafa ya kwenda kutafuta, lakini ili kufanya mazungumzo. Nilipenda sana usemi huu wa jirani wa tatu. Ni utajiri wako.

Cristina Cabrejas (EFE): Jana, ulituma ujumbe kwa watu wa China, ukiwaomba Wakatoliki kuwa raia wema baada ya mamlaka ya nchi kutoruhusu maaskofu kwenda Mongolia. Uhusiano na China ukoje kwa sasa? Je, kuna habari zozote kuhusu safari ya Kadinali Zuppi kwenda Beijing na utume wa kwenda Ukraine?

Papa Francisko: Utume wa Kardinali Zuppi ni utume wa amani ambao nilimkabidhi. Na alifanya mpango wa kutembelea Moscow, Kyiv, Marekani, na pia Beijing. Kardinali Zuppi ni mtu wa mazungumzo makubwa na maono ya ulimwengu wote. Historia yake ni pamoja na uzoefu wake wa kufanya kazi Msumbiji katika kutafuta amani, na ndiyo maana nilimtuma. Uhusiano na China ni wa heshima sana, wa heshima sana. Binafsi ninawapenda sana Wachina. Njia ziko wazi sana, kwa uteuzi wa maaskofu kuna tume ambayo imekuwa ikifanya kazi na serikali ya China na Vatican kwa muda mrefu. Kisha kuna wengi, au tuseme kuna baadhi, mapadre wa Kikatoliki au wasomi wa Kikatoliki ambao mara nyingi hualikwa kwenye vyuo vikuu vya Chima kutoa kozi. Nadhani tunapaswa kusonga mbele katika nyanja ya kidini ili kuelewana zaidi na ili raia wa China wasifikirie kuwa Kanisa halikubali utamaduni na maadili yao na kwamba Kanisa linategemea nguvu nyingine, ya kigeni. Njia hii ya kirafiki inafuatwa vyema na Tume inayoongozwa na Kardinali Parolin: wanafanya kazi nzuri, hata kwa upande wa China, mahusiano yanasonga mbele. Ninawaheshimu sana Wachina.

Gerard O'Connell (Jarida la Amerika): Baba Mtakatifu, mahusiano kati ya Vietnam na Vaticanhivi sasa  ni mazuri sana, yamepiga hatua ya ajabu hivi karibuni. Wakatoliki wengi wa Vietnam wanakuomba uwatembelee, kama ulivyofanya Mongolia. Je, kuna uwezekano sasa wa kutembelea Vietnam? Je, kuna mwaliko kutoka kwa serikali? Na ni safari gani zingine unapanga?

Papa Francisko: Vietnam ni mojawapo ya uzoefu mzuri sana wa mazungumzo ambayo Kanisa limekuwa nayo katika siku za hivi karibuni. Ningesema ni kama kuhurumiana katika mazungumzo. Pande zote mbili zimekuwa na nia njema ya kuelewana na kutafuta njia za kusonga mbele; kumekuwa na matatizo, lakini katika Vietnam naona kwamba mapema au baadaye matatizo ni kushindwa. Muda kidogo uliopita, na Rais wa Vietnam, tulizungumza kwa uhuru. Nina maoni chanya sana kuhusu uhusiano na Vietnam; kazi nzuri imekuwa ikiendelea kwa miaka. Ninakumbuka miaka minne iliyopita, kundi la wabunge wa Vietnam walikuja kutembelea: kulikuwa na mazungumzo mazuri nao, yenye heshima sana. Wakati utamaduni unakuwa wazi, kuna uwezekano wa mazungumzo; ikiwa kuna kufungwa au tuhuma, mazungumzo ni magumu sana. Pamoja na Vietnam, mazungumzo ni wazi, pamoja na zaidi na kidogo  lakini ni wazi na kusonga mbele polepole. Kumekuwa na matatizo fulani, lakini yametatuliwa. Katika safari ya Vietnam, ikiwa sitakwenda, Yohane wa XXIV hakika atafanya. Hakika kutakuwa na safari kwa sababu ni nchi ambayo inastahili maendeleo na ambayo yana huruma yangu. Mbali na safari nyingine, kuna Marseille; na kisha kuna moja kwa nchi ndogo katika Ulaya, na tunaona kama tunaweza kuifanya. Lakini kusema ukweli, kwangu kwenda safari sasa sio rahisi kama ilivyokuwa mwanzo. Kuna mapungufu katika kutembea na hiyo inaniwekea vizingiti. Lakini tutaona.

Fausto Gasparroni (ANSA): Baba Mtakatifu, matamshi yako ya hivi majuzi kwa Wakatoliki vijana s wa Urusi kuhusu “Mama mkuu wa Urussi.” Picha ya mrithi wa watu kama vile Petro Mkuu na Catherine II yamechochea mjadala fulani. Maoni haya yameudhi sana, kwa mfano, Waukraine, pia yamekuwa na matokeo ya kidiplomasia, na yameonekana kwa kiasi fulani kama karibu kuinua ubeberu wa Urussi na aina ya kuidhinisha hata sera za Putin. Nilitaka kukuuliza: kwa nini ulihisi hitaji la kufanya matamshi haya, ikiwa umetafakari juu ya fursa ya kuyatoa, ikiwa ungeyarudia? Na pia, ili tu kuweka mambo wazi, unaweza kutuambia nini unafikiria juu ya ubeberu na kwa namna ya pekee juu ya ubeberu wa Urussi?

Papa Francisko: Hebu tuzungumze juu ya muktadha: ilikuwa mazungumzo na vijana wa Urussi. Na mwisho wa mazungumzo, niliwapatia ujumbe, ujumbe ambao ninarudia kila mara: kuwajibika kwa ajili ya urithi wao. Jambo la kwanza: kuchukua urithi wao. Ninasema kitu kimoja kila mahali. Na kwa kuzingatia hili, ninajaribu kuunda mazungumzo kati ya babu na wajukuu: kwamba wajukuu wachukue urithi wao. Ninasema hivyo kila mahali, na huo ndio ulikuwa ujumbe. Jambo la pili, kufafanua ninachomaanisha na urithi: Nilitaja wazo la Urussi kubwa, kwa sababu urithi wa Urussi ni mzuri sana; mzuri sana. Fikiria juu ya uwanja wa fasihi, muziki, ukirudi kwa Dostoevsky, ambaye leo hii anazungumza nasi juu ya ubinadamu uliokomaa. (Urussi) ilichukua jukumu hili la ubinadamu, ambalo lilikua katika sanaa na fasihi. Hiki kingekuwa kipengele cha pili nilipozungumza kuhusu urithi, sivyo? Jambo la tatu, labda, halikuwa sahihi, lakini kwa kuzungumzia juu ya Urussi kubwa sio sana kwa maana ya kijiografia, lakini kwa maana ya kiutamaduni, nilikumbuka kile tulichofundishwa shuleni: Petro I, Catherine II. Na hii ya tatu ilikuja baadaye, ambayo labda haikuwa sawa kabisa. Sijui. Hebu wanahistoria watuambie. Lakini ilikuwa ni maelezo ya ziada ambayo yalikuja akilini mwangu kwa sababu nilisoma shuleni. Nilichowaambia Warussi vijana ni kuchukua jukumu la urithi wao, kuchukua urithi wao, ambao inamaanisha kutoweza kuununua mahali pengine. Kuchukua urithi wao. Na Urussi kuu iliacha urithi gani? Utamaduni wa Kirussi ni wa uzuri mkubwa, na kina, na haupaswi kufutwa kwa masuala ya kisiasa.

Kumekuwa na miaka ya giza nchini Urussi, lakini urithi wake umebaki sawa. Kisha ulizungumza juu ya ubeberu, na sikuwa nikifikiria ubeberu niliposema hivyo. Nilizungumza juu ya tamaduni, na usambazaji wa tamaduni sio wa kifalme, kamwe. Daima ni mazungumzo, na nilikuwa nikizungumza juu ya hilo. Ni kweli kwamba kuna ubeberu ambao unataka kulazimisha itikadi zao. Nitaishia hapa: wakati utamaduni unatolewa na kugeuzwa kuwa itikadi, ni sumu. Utamaduni unatumika, lakini unaingizwa kwenye itikadi. Ni lazima tutofautishe utamaduni wa watu na itikadi zinazojitokeza kutoka kwa mwanafalsafa fulani, mwanasiasa fulani wa watu hao. Na ninasema hivi kwa kila mtu, pia kwa ajili ya Kanisa. Ndani ya Kanisa mara nyingi kuna itikadi zinazotenganisha Kanisa na maisha yanayotoka kwenye mzizi na kwenda juu. Zinatenganisha Kanisa kutoka katika ushawishi wa Roho Mtakatifu. Itikadi haina uwezo wa kupata mwili; ni wazo tu. Lakini itikadi inapokusanya nguvu na kuwa siasa, kwa kawaida inakuwa udikteta, sivyo? Inakuwa kutokuwa na uwezo wa mazungumzo, kusonga mbele na tamaduni. Na ubeberu hufanya hivyo. Ubeberu siku zote hujiimarisha kuanzia itikadi. Katika Kanisa pia tunapaswa kutofautisha fundisho na itikadi yaani mafundisho ya kweli na kamwe yasiyo ya kiitikadi. Yanatokana na watu watakatifu waamini wa Mungu. Badala yake, itikadi inajitenga na ukweli, imejitenga na watu ... sijui kama nilijibu swali lako.

Robert Messner (DPA):  Habari za asubuhi. Swali kuhusu sasisho lako la Laudato si': je, linaweza kueleweka kama onesho la huruma na wanaharakati wa mazingira kama vile ‘Kizazi cha Mwisho,’ ambacho huandaa maandamano yenye maandamano makubwa? Labda pia kuna ujumbe katika sasisho hili kwa wanaharakati vijana wanaoingia mitaani?

Papa Francisko: Kwa ujumla, siwagusi hawa wenye msimamo mkali. Lakini vijana wana wasiwasi. Mwanasayansi mzuri wa Kiitaliano  wakati tulikuwa na mkutano katika Chuo (cha Sayansi), alitoa hotuba nzuri na kuhitimisha kwa kusema: “Nisingependa mjukuu wangu, aliyezaliwa jana, aishi katika hali mbaya kama hiyo. duniani katika muda wa miaka thelathini.” Vijana wanafikiri juu ya wakati ujao. Na kwa maana hiyo, ninapenda kwamba wapambane  vizuri. Lakini itikadi inapohusika, au shinikizo la kisiasa linapohusika au linatumiwa kwa hilo, inashindwa. Waraka Wangu wa Kitume utatolewa katika siku kuu ya Mtakatifu Francisko, tarehe 4 Oktoba, na ni mapitio ya kile kilichotokea tangu COP huko Paris, ambayo labda imekuwa yenye matunda zaidi hadi leo. Kuna habari kuhusu baadhi ya COP nyingine na kuhusu baadhi ya mambo ambayo bado hayajatatuliwa, na kuna uharaka wa kuyatatua. Si kubwa kama Laudato si’, lakini ni mwendelezo wa Laudato si' kuhusu mambo mapya, na pia ni uchanganuzi wa hali hiyo.

Etienne Loraillère (KTO TV): Ungependa Kanisa la Sinodi nchini Mongolia na duniani kote. Kusanyiko la Oktoba tayari ni matunda ya kazi ya watu wa Mungu. Wabatizwa kutoka ulimwenguni kote wanawezaje kuhusika katika awamu hii? Mgawanyiko wa kiitikadi unawezaje kuepukwa?Je,washiriki wataweza kuzungumza na kushiriki hadharani yale wanayopitia ili kuruhusu kutembea pamoja nao? Au mchakato mzima utakuwa wa faragha?

Papa Francisko: Ulizungumza juu ya jinsi ya kuzuia shinikizo la kiitikadi. Hakuna nafasi ya itikadi katika Sinodi, kwani ni nguvu tofauti. Sinodi inahusu mazungumzo: kati ya wabatizwa, kati ya washiriki wa Kanisa, juu ya maisha ya Kanisa, mazungumzo na ulimwengu, juu ya matatizo ambayo yanawahusu binadamu leo hii. Lakini mtu anapofikiria kuteneneza njia ya kiitikadi, Sinodi inaisha! Hakuna nafasi ya itikadi katika Sinodi, kuna nafasi ya mazungumzo. Kuzungumza na kila mmoja, kama kaka na dada, na kujadili mafundisho ya Kanisa. Kusonga mbele. Kisha ninataka kusisitiza kwamba sinodi sio uvumbuzi wangu: ilikuwa ni Mtakatifu Paulo VI. Katika Mtaguso wa Pili wa Vatican ulipomalizika, alitambua kwamba huko Magharibi Kanisa lilikuwa limepoteza mwelekeo wa kisinodi; Kanisa la Mashariki bado lilikuwa nayo. Kwa sababu hiyo, aliunda Sekretarieti ya Sinodi ya Maaskofu, ambayo katika miaka hii sitini imefanya tafakari ya mbele kwa njia ya sinodi kama maendeleo endelevu, na kusonga mbele. Ilipofika miaka hamsini ya uamuzi huu wa Mtakatifu Paulo VI, nilitia saini na kuchapisha waraka kuhusu nini maana ya Sinodi na jinsi  gani ilivyosonga mbele. Na sasa imekwenda mbele; imekomaa zaidi na kwa sababu hiyo nilifikiri itakuwa vizuri sana kuwa na Sinodi ya Kisinodi, ambayo si mwelekeo; ni ukweli wa kale; Kanisa la Mashariki limekuwa nalo daima.

Lakini je, tunaishije sinodi hizi, ni kuziishi kama Wakristo, kama nilivyosema hapo awali, bila kukubali itikadi. Katika mchakato wa kusanyika: kuna jambo moja ambalo ni lazima tulinde, hali ya kisinodi. Hiki sio kipindi cha runinga ambacho unazungumza juu ya kila kitu. Hapana. Kuna wakati wa kidini; kuna wakati wa kubadilishana mawazo ya kidini. Katika utangulizi wa sinodi, watazungumza kwa dakika tatu hadi nne kila mmoja na kisha kutakuwa na dakika tatu hadi nne za ukimya kwa maombi. Bila roho hii ya maombi hakuna sinodi; inakuwa siasa na ubunge. Sinodi sio bunge. Kuhusu faragha ya majadiliano: kuna idara inayoongozwa na Dk. Ruffini, ambaye yuko hapa, na ambaye atatoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu maendeleo ya Sinodi. Katika Sinodi, ni muhimu kulinda dini na kulinda uhuru wa wale wanaozungumza. Kwa hilo kutakuwa na tume, itakayoongozwa na Dk. Ruffini, ambayo itatoa taarifa kuhusu maendeleo ya Sinodi.

Antonio PELAYO (Vida Nueva): Baba Mtakatifu, umezungumza hivi punde kuhusu Sinodi na sote tunakubaliana nawe kwamba Sinodi hii imezua udadisi na shauku nyingi. Kwa bahati mbaya, pia imeleta ukosoaji mwingi kutoka na  ukweli wa Kikatoliki. Ninarejea kitabu chenye utangulizi wa Kardinali Burke anayesema kwamba Sinodi ni sanduku la pandora ambapo majanga yote kwa Kanisa yatatoka. Una maoni gani kuhusu nafasi hii? Je, unafikiri itashindwa na ukweli au inaweza kuwa kuathiri Sinodi?

Papa Francisko: Sijui kama nimeshasema haya hapo awali. Miezi michache iliyopita, niliita Mkarmeli. “Watawa wanaendeleaje, Mama Mkuu?” Alikuwa Mkarmeli asiye Mwitaliano. Na yule aliyetangulia akanijibu. Na mwishowe akaniambia: Baba ‘Mtakatifu  tunaogopa na Sinodi hii.’ “Ni nini kinaendelea sasa?” Nilisema kwa mzaha. “Unataka kumtuma Sisita kwenye Sinodi?” ‘Hapana, tunaogopa utabadilisha mafundisho.’ Na hivi ndivyo alivyokuwa akisema, alikuwa na wazo hili… Lakini ukienda kwenye mzizi wa mawazo haya, utakuta itikadi. Siku zote, mtu anapotaka kujitenga na njia ya ushirika katika Kanisa, ni nini hutenganisha kila mara ni itikadi. Na wanalishutumu Kanisa kwa hili au lile, lakini wao kamwe hawashitaki kwa yaliyo kweli:kanisa linaundwa na wakosefu. Hawazungumzi kamwe juu ya dhambi... Wanatetea ‘fundisho’, fundisho kama maji yaliyeyushwa ambayo hayana ladha na si mafundisho ya kweli ya Kikatoliki, yaani, katika Imani. Na kwamba mara nyingi sana kashfa. Wazo la kwamba Mungu alifanyika mwili ni la kashfa kiasi gani, kwamba Mungu alifanyika Mwanadamu, kwamba Mama Yetu aliutunza ubikira wake? Hii inatia kashfa.

Cindy Wooden (CNS): Habari za asubuhi Baba Mtakatifu, ningependa kufuatilia swali la Mfaransa mwenzangu kuhusu Sinodi na habari. Waamini walei wengi sana wametoa muda mwingi, maombi, kushiriki katika kuzungumza,  na kusikiliza. Wanataka kujua kinachoendelea wakati wa Sinodi. Na ulizungumza kuhusu uzoefu wako wa Sinodi ya kidini, ambapo baadhi ya watu walikuwa wamesema, “usiweke hili…”, “Huwezi kusema hivi...” Sisi waandishi wa habari hatuna hata fursa ya kuingia kwenye mkutano na vikao vya jumla. Je, tunawezaje kuwa na uhakika kwamba kile tunachopewa kama  ‘utando’ ni kweli? Je, hakuna uwezekano wa kuwa wazi zaidi na waandishi wa habari?

Papa Francisko: Lakini ni wazi sana, mpendwa; iko wazi sana! Kuna tume inayoongozwa na Paolo Ruffini Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Vatican, ambaye atatoa habari kila siku, lakini wazi zaidi, sijui, wazi zaidi, sijui. Ni vyema kwamba tume hii itaheshimu sana hotuba za kila mtu na itajaribu kutopiga soga bali kusema mambo kwa usahihi kuhusu maendeleo ya sinodi, ambayo ni ya kujenga kwa Kanisa. Ikiwa unataka, ikiwa mtu anataka habari iwe, “Mtu huyu ameitoa kwa mtu huyo kwa sababu hii au ile,” hiyo ni porojo za kisiasa. Kamati haina kazi rahisi, kwa kusema: “Leo tafakari ilikwenda hivi, ilikwenda hivi,” na kuwasilisha roho ya kikanisa, si ya kisiasa. Bunge ni tofauti na sinodi. Usisahau kwamba mhusika mkuu wa Sinodi ni Roho Mtakatifu. Na hii inawezaje kupitishwa? Hii ndiyo sababu maendeleo ya kikanisa lazima yasambazwe.

Vincenzo Romeo (RAI TG 2):  Habari za asubuhi, Baba Mtakatifu. Wewe ni Papa wa pembezoni, na pembezoni, hasa katika Italia, wanateseka sana. Tumekuwa na matukio yanayotia wasiwasi ya vurugu, uharibifu... Kwa mfano, karibu na Napoli, Padre wa parokia, Padre Maurizio Patriciello Paroko  wa parokia ya Caivano,  hata kukualika kwenda huko, kisha huko Palermo, Sicilia. Je, nini kifanyike? Ulitembelea ‘villas miserias’ huko Buenos Aires, kwa hivyo una uzoefu na hilo. Waziri Mkuu wetu pia alitembelea moja ya pembezoni hizi. Kuna mjadala mwingi. Nini kifanyike, Kanisa na taasisi za Serikali zinaweza kufanya nini ili kuondokana na uharibifu huu na kufanya pembezoni kuwa sehemu ya nchi kweli?

Papa Francisko: Unazungumza kuhusu maeneo ya pembezoni, kama vile vitongoji duni: lazima uende mbele, lazima uende huko na kufanya kazi huko, kama ilivyofanywa huko Buenos Aires na makasisi waliofanya kazi huko na  timu ya mapadre ikiwa na Askofu Msaidizi mstari wa mbele na unafanya kazi hapo. Lazima tuwe wazi kwa hili, serikali lazima ziwe wazi, serikali zote za ulimwengu, lakini kuna pembezoni ambazo ni za kusikitisha. Ninarudi kwenye kando ya kashfa ambayo watu wanajaribu kuficha: ile ya Rohingya. Warohingya wanateseka. Wao si Wakristo; ni Waislamu, lakini wanateseka kwa sababu wamegeuzwa kuwa pembezoni; wamefukuzwa. Inabidi tuone aina tofauti za pembezoni na pia kujifunza kwamba pembezoni ndipo uhalisia wa binadamu unapodhihirika zaidi na usio wa kisasa zaidi – ambapo kwa nyakati mbaya, sitaki kuainisha, lakini inatambulika vyema zaidi. Mwanafalsafa mmoja aliwahi kusema jambo ambalo lilinishangaza sana: “Ukweli unaeleweka vyema zaidi kutoka katika mambo ya pembezoni.” Lazima tuzungumze na pembezoni, na serikali lazima zifanye haki halisi ya kijamii, haki halisi ya kijamii, na nyanja tofauti za kijamii na pia na pembezoni za kiitikadi, ili kuwafanya wazungumze, kwa sababu mara nyingi  pembezoni  ni nzuri za kiitikadi ambazo huchochea jamii. Ni pembezoni, Ulimwengu wa pembezoni sio rahisi. Asante.

05 September 2023, 09:46