2023.09.23 Papa ameaga watu wa Marsiglia katika ziara yake ya kitume ya siku mbili 22-23 Septemba 2023. 2023.09.23 Papa ameaga watu wa Marsiglia katika ziara yake ya kitume ya siku mbili 22-23 Septemba 2023.  (Vatican Media)

Papa Francisko atoa shukrani kwa Marsiglia na kumbukizi ya wahanga wa Nice

Mwishoni mwa Ibada ya Misa Takatifu katika Uwanja wa Velodrome,kwa waamini wa Ufaransa Papa aliwasalimia viongozi na raia wa Ufaransa kwa namna ya pekee hata kuwakumbuka wahanga wa shambulio la kigaidi la 2016 na kuomba kuwa:“tusichoke kuombea amani katika kanda zilizoharibiwa na vita.

Baba Mtakatifu Francisko Jumamosi tarehe 23 Septemba 2023 mara baada Ibada ya Misa Takatifu katika uwanja wa Velodrome huko Marsiglia, amependa kutoa shukrani zake. Akianza amesema “Ninakushukuru, mwadhama, kwa maneno yake amewashukuru wote kaka na dada , kwa uwepo wao na kwa maombi yao. Papa amebainisha alivyofikia mwisho wa ziara yake ambapo ametaka kutoka shukrani zake kwa mapokezi mazuri aliyopokea, pamoja na kazi na maandalizi yote ambayo yamefanyika. Amemshukuru Rais wa Jamhuri na kupitia kwake, ametoa salamu za matashi mema kwa wanaume na wanawake wote wa Ufaransa. Amemsalimia Waziri Mkuu aliyekuja kumkaribisha katika uwanja wa ndege na pia aliwasalimia viongozi waliokuwapo, hasa Meya wa Marsiglia.

Kanisa la Marsiglia wamekuwa na furaha ya mchungaji wa Kanisa
Kanisa la Marsiglia wamekuwa na furaha ya mchungaji wa Kanisa

Papa Francisko ameonesha kukumbatia Kanisa zima la Marsiglia, pamoja na parokia zake na jumuiya za kitawa, taasisi zake nyingi za elimu na mashirika yake ya upendo. Jimbo kuu hilo lilikuwa la kwanza ulimwenguni kuwekwa wakfu kwa Moyo Mtakatifu wa Yesu, wakati wa mlipuko wa tauni mnamo mwaka 1720. Kwa hiyo Papa ameongeza kusema “mioyoni mwenu muwe ishara za upendo mwororo wa Mungu, pia katikati ya janga la leo  hii la kutojali”. Asante kwa huduma yao ya  upole na ya kujitolea, ambayo inashuhudia ukaribu na huruma ya Bwana! Baadhi yao walifika  hapo kutoka sehemu mbalimbali za Ufaransa: waliwashukuru kwa kifarasa merci à vous!

Papa akisalimia viongozi wa kidini mara baada ya misa
Papa akisalimia viongozi wa kidini mara baada ya misa

Pia Baba Mtakatifu  alipenda kuwasalimu kaka na dada kutoka Nice, wakisindikizwa na Askofu na Meya wao. Amekumbuka shambulio baya la tarehe 14 Julai 2016, ambalo  walikuwa ni manusura.  Kwa hiyo ameomba “Wakumbukwe katika sala wale wote waliopoteza maisha katika mkasa huo, pamoja na vitendo vyote vya kigaidi ambavyo vimekuwa vikifanyika nchini Ufaransa na kila sehemu ya dunia. Ugaidi ni woga. Tusichoke kuombea amani katika maeneo yenye vita, na hasa kwa watu waliokumbwa na vita wa Ukraine.”

Papa ametoa shukrani
Papa ametoa shukrani

Ni matumanini ya Papa kuwa salamu zake za dhati zitafika kwa wagonjwa, kwa watoto na wazee, ambao ni kumbukumbu ya ustaarabu. Amewafikiria hasa wale walio katika matatizo na wafanyakazi wote katika jiji hilo: Jacques Loew, Padre wa kwanza mfanyakazi wa Ufaransa, aliyefanya kazi kwenye bandari ya Marsirglia alisema kuwa “Heshima ya wafanyakazi iheshimiwe, ikuzwe na kulindwa! Papa kwa kuhitimisha amewahakikishia kubeba moyoni mwake matukio ya siku hizi Na kwamba Mama Yeru wa Ulinzi alitazame jiji hilo, ambalo ni jiwe la matumaini, juu ya familia zao  zote, na juu ya kila mmoja wao amembariki  huku akimbwa wamuombee. Sio kazi rahisi na ameshukuru.

Msalaba wa wokovu
Msalaba wa wokovu
Hitimisho la siku mbili za ziara ya Papa 22-23 Septemba 2023
23 September 2023, 19:13