Tafuta

2023.09.22 Papa Francisko huko Marsiglia - Wakati wa sala kwenye kumbusho la mabaharia na wahamiaji waliopote majini. 2023.09.22 Papa Francisko huko Marsiglia - Wakati wa sala kwenye kumbusho la mabaharia na wahamiaji waliopote majini.  (Vatican Media)

Papa Francisko:Mediteranea ni njia za udugu au za sintofahamu

Papa katika siku yake ya kwanza Marsiglia,alitoa heshima kwa waliopotea katika Mediterania.Hawa ni mabaharia na wahamiaji waliopotea baharini. Ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa:vifo baharini sio takwimu ni majina na ukoo,ni sura na historia,ni maisha yaliyovunjika na ndoto zilizovunjika kuziokoa ni jukumu la ubinadamu na ustaarabu.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko akiwa katika ziara yake ya 44 ya kitume kusini mwa Ufaransa, tarehe 22 -23 Septemba 2023 ili kufunga tukio la Mikutano ya Mediteranea, kwa kuongozwa na mada ya "muundo mziri wa matumaini", ameingilia kati kutoa muda wa kukumbuka mabaharia na wahamiaji waliopotea baharini katika mnara wa kumbu kumbu huko Marsiglia. Akianza hotuba yake ameshukuru uwepo wao hapo. “Mbele yetu ni bahari, chanzo cha uhai, lakini mahali hapa panaibua maafa ya ajali ya meli, ambayo husababisha vifo. Tumekusanywa kwa kumbukumbu ya wale ambao hawakufanikiwa, ambao hawakuokolewa. Tusizoee kuchukulia ajali za meli kama historia za habari na vifo vya baharini kama namba: hapana, ni majina na ukoo, ni sura na historia, ni maisha yaliyovunjika na ndoto zilizovunjika. Ninawafikiria kaka na dada wengi waliozama kwa woga, pamoja na matumaini waliyokuwa nayo mioyoni mwao. Kukabiliana na janga kama hilo, tunahitaji vitendo, sio maneno. Kabla ya hapo, hata hivyo, tunahitaji kuonesha ubinadamu fulani: ukimya, kilio, huruma na sala. Kwa sasa ninawaalika kutumia muda wa kimya kuwakumbuka hawa ndugu zetu: tuguswe na misiba yao.(Kumekuwa na ukimya...).

Kumbu kumbu kwa mabaharia na wahamiaji waliomezwa maji ya mediteranea
Kumbu kumbu kwa mabaharia na wahamiaji waliomezwa maji ya mediteranea

Baba Mtakatifu aliendelea kusema kuwa watu wengi sana, wanaokimbia migogoro, umaskini na majanga ya mazingira katika kutafuta kwao maisha bora ya baadaye, wanaona katika mawimbi ya Bahari ya Mediterania kukataliwa kabisa. Na hivyo bahari hii nzuri imekuwa makaburi makubwa, ambapo kaka na dada wengi wananyimwa hata haki ya kaburi. Kuzikwa baharini ndio heshima pekee waliyopewa. Katika ushuhuda wa kitabu “Ndugu Mdogo,” mhusika mkuu, mwishoni mwa safari yenye matatizo iliyomleta kutoka Jamhuri ya Guinea hadi Ulaya, alisema, “Unapoketi juu ya bahari uko kwenye njia panda. Upande mmoja ni uhai, na upande mwingine ni kifo. Hakuna chaguzi nyingine.” Kwa njia hiyo Papa amesema sisi pia tuko njia panda: kwa upande mmoja, kuna udugu, unaoifanya jumuiya ya wanadamu kustawi kwa wema; kwa upande mwingine, kutojali, kwa damu ya Mediterranea. Tunajikuta kwenye njia panda ya ustaarabu.

Papa alikuwa katika mnara wa kumbu kumbu la mabaharia na wahamiaji walipoteza maisha yao baharini
Papa alikuwa katika mnara wa kumbu kumbu la mabaharia na wahamiaji walipoteza maisha yao baharini

 

Hatuwezi kukata tamaa ya kuona wanadamu wakitendewa biashara, kufungwa na kuteswa kwa njia mbaya; hatuwezi tena kutazama tamthilia ya ajali ya meli, inayosababishwa na biashara ya kikatili na ushabiki wa kutojali. Watu ambao wako katika hatari ya kuzama wakati wa kutelekezwa kwenye mawimbi lazima waokolewe. Ni wajibu wa ubinadamu; ni wajibu wa ustaarabu! Baba Mtakatifu Francisko kwa uchungu amesema kwamba Mungu atatubariki, ikiwa juu ya nchi kavu na baharini tunajua jinsi ya kuwatunza walio dhaifu zaidi, ikiwa tunaweza kushinda kupooza kwa hofu na kutojali ambako, kwa ujuu juu huwahukumu wengine kifo. Katika hili, sisi wawakilishi wa dini mbalimbali tunaitwa kuwa mfano. Hakika Mungu alimbariki baba Ibrahimu. Aliitwa aondoke katika nchi yake: “bila kujua aendako” (Ebr 11:8). Baba Mtakatifu akisisitiza Zaidi kuhusu Ibrahimi amesema: “Akiwa mgeni na msafiri katika nchi ya ugenini, aliwakaribisha wasafiri waliopita karibu na hema lake (rej. Mwa. 18): “aliyehamishwa kutoka katika nchi yake na asiye na makao mwenyewe, alikuwa makao na nchi ya watu wote.  

Wakati muhimu wa kuomba kuwakumbuka kaka na dada zetu wahamiaji
Wakati muhimu wa kuomba kuwakumbuka kaka na dada zetu wahamiaji

Na “kama thawabu kwa ukarimu wake, alipokea karama ya uzao”. Hivyo, katika mizizi ya dini tatu za Mediterania zinazoamini Mungu mmoja ni ukarimu, upendo kwa mgeni katika jina la Mungu. Na hili ni muhimu ikiwa, kama baba yetu Ibrahimu, tunaota ndoto za wakati ujao wenye mafanikio. Sisi waamini, basi, lazima tuwe mfano wa kuigwa katika kukaribiana na kidugu. Uhusiano kati ya vikundi vya kidini mara nyingi si rahisi, pamoja na mdudu wa itikadi kali na tauni ya kiitikadi ya msingi ambayo huharibu maisha halisi ya jamii. Kuhusiana na hilo, Baba Mtakatifu amependa kurudia maneno ambayo mtu wa Mungu aliyeishi karibu na hapo aliandika kuwa: “Mtu yeyote asiendelee kumchukia jirani yake moyoni mwake, bali apende, kwa maana mtu akimchukia mtu mmoja, hawezi kuwa na amani pamoja na Mungu. Ombi la mtu halisikiki kwa Mungu maadamu hasira huihifadhi nafsini mwake.” 

Kufanya kumbu kumbu na kuwaombea waliopoteza maisha baharini
Kufanya kumbu kumbu na kuwaombea waliopoteza maisha baharini

Kwa maana hiyo Baba Mtakatifu amesema kuwa Marseille (Marsiglia) pia, yenye sifa nyingi za wingi wa kidini, inasimama kwenye njia panda: kukutana au kugombana. Amewashukuru wote, wanaochagua njia ya kukutana; ametoa asante kwa mshikamano wo na kujitolea madhubuti katika kukuza maendeleo na utangamano wa binadamu. Ni vyema kuwa hapo, pamoja na vikundi mbalimbali vinavyofanya kazi na wahamiaji, Marseille-Espérance, shirika la majadiliano ya kidini linalokuza udugu na kuishi pamoja kwa amani. Papa amesema kuwa na matarajio kwa waanzilishi na mashahidi wa mazungumzo, kama vile Jules Isaac, ambaye aliishi karibu na ambaye kumbukumbu ya miaka sitini ya kifo iliadhimishwa hivi karibuni. Kwa hiyo nayo ni Marsiglia  ya siku zijazo. Isonge  mbele bila kukata tamaa, ili mji huu uwe kwa Ufaransa, Ulaya na ulimwengu kama muundo mzuri wa matumaini.

Matukio ya siku ya Papa huko Marsiglia 22 Septemba

Vivile vile katika hotuba ya Baba Mtakatifu kabla ya kuhitimisha amependa , kunukuu baadhi ya maneno ya David Sassoli aliyoyasema huko Bari, wakati wa mkutano uliopita wa  Bahari ya Mediterania: “Huko Baghdad, katika Nyumba ya Hekima ya Khalifa Al-Ma'mun, Wayahudi, Wakristo na Waislamu walikuwa wakikutana kusoma vitabu vitakatifu na wanafalsafa wa Kigiriki. Leo hii sisi sote tunahisi, waamini na wasioamini, hitaji la kuijenga upya nyumba hiyo ili kuendelea pamoja kupambana na sanamu, kubomoa kuta, kujenga madaraja, na kuupatia umuhimu ubinadamu mpya.” Kwa  kutazama undani wakati wetu na kuupenda hata zaidi wakati ni ngumu kupenda, Papa Francisko anaamini, kuwa  hii ni mbegu iliyopandwa katika siku hizi wakati tunazingatia sana hatima yetu. Amewamba wasiogope matatizo ambayo Mediterranean inaleta. [...]. Kwa Umoja wa Ulaya na kwetu sote, tuishi kwetu kunategemea hili. Tukabiliane na matatizo haya pamoja; tusilete tumaini la kuvunjika kwa meli; tufanye pamoja picha ya amani! Amehitimisha.

Kumbu kumbu kwa mabaharia na wakimbizi

 

22 September 2023, 19:29