Papa amepokea salio la familia ya Ulma na turubai la wahamiaji kutoka Cutro
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Safu ya familia ya Ulma iliyotangazwa kuwa mwenyeheri huko Poland, turubai iliyoundwa na wafungwa wa Crotone katika kukumbuka ajali ya meli ya wahamiaji huko Cutro na jiwe la msingi la seminari mpya huko Ukraine zilikuwa ni alama tatu za historia tofauti ambazo zilikabidhiwa mikononi mwa Papa Francisko, Jumatano tarehe 13 Septemba 2023, mara baada ya katekesi. Kwa hiyo wakati wa salamu na picha za makundi tofauti Papa aliweza kuona na kukabidhiwa mambo hayo. Na hivyo ushuhuda wa wanandoa wa Ulma na watoto wao saba ulirudiwa kuonekana katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican. Hii ni Familia nzima iliyouawa kwa kuchukiwa imani yao wakati wanatoa ushuhuda wa ukarimu kwa Wayahudi, enzi za Kinazi, mnamo tarehe 24 Machi 1944 huko Markowa, na kutangazwa Wenyeheri na Kardinali Marcello Semeraro Mwenyekiti wa Baraz ala Kipapa la Kuwatangaza Wenyeheri na Watakatifu, Dominika tarehe 10 Septemba 2023.
Papa alipewa masalia ya wenyeheri hao ambapo aliibusu kwa upole na picha inayoonesha familia hiyo. Waliokabidhi zawadi hizo muhimu ulikuwa ni ujumbe wa Poland, ukiongozwa na Askofu Mkuu wa Przemyśl wa Kilatini, Adam Szal, ambaye alimwomba Baba Mtakatifu kubariki mchoro wa Moyo Mtakatifu wa Yesu ambao utapelekwa katika parokia zote za Jimbo kuu.
“Tulikuja hasa kumshukuru Papa kwa uamuzi wake wa kuwatangaza Józef na Wiktoria Ulma tukitumaini kwamba tukio hili la ajabu litazaa matunda ya kudumu na mengi katika maisha ya Kanisa. Tunaamini kwamba kwa ajili hiyo hija ya mchoro wa Moyo Mtakatifu wa Yesu ambayo inaanza tarehe 18 Septemba 2023 na pia kutembelea Ufaransa itakuwa ya msaada mkubwa. Kwa dhamana maalum kwa Mtakatifu Maria Margaret Alacoque," alielezea Padre Witold Burda.
Kumbukumbu ya wahamiaji waliokufa huko Cutro
Mnamo Februari 26 iliyopita, huko Steccato ya Cutro, Meli ya “Summer love", iliyojaa wahamiaji, ilizama mita chache kutoka ufukweni na vifo 94 vilivyothibitishwa, ambapo 35 walikuwa watoto. Ili kukumbuka moja ya janga kubwa la uhamiaji, wafungwa wa gereza la Crotone walitaka kukutoa zawadi kwa Papa Francisko la turubai, iliyokuwa kwenye sanduku la kioo, ambapo tukio hilo kubwa limeibuliwa tena la kuwakumbuka wafa maji katika harakati za kuvuka Bahari ya Mediterranea.
Kwa hiyo "Kuundwa kwa kazi hiyo pia ni njia ya kutoa sauti kwa wafungwa, alisema Padre msmamizi wa kiroho katika gereza la Crotone, Padre Oreste Mangiacapra ambapo yeye ni nyeti kwa masula kama haya, akionesha kuwa wanataka kubadilika na kujiandaa, mara moja katika hukumu ili kuwa na muunganisho wa kweli wa kijamii, wa kibinadamu na wa kazi kama Papa Francisko ambavyo amezoea kusema na kutarajia. Kazi hiyo, aliongeza Federico Ferraro, mdhamini wa manispaa ya haki za wafungwa, kuwa “inawakilisha hisia zote za kushiriki wafungwa. Kwa wathirika na ukaribu na waathirika na familia. Hii inamulika jinsi gani katika vituo vya magereza kuna watu ambao huhifadhi hisia za ushiriki wa kijamii."
Jiwe la msingi la Redemptoris Mater ya Uzhgorod
Ishara ya amani na onesho la hamu ya kujenga upya ndiyo maneno yaliyooneshwa na Padre Francesco Andolfatto, Mkuu wa Seminari ya Redemptoris Mater ya Uzhgorod, akielezea jiwe la msingi ambalo watajenga katika jiji la Kiukraine mpaka na Slovakia na Hungaria ambalo limebarikiwa na Papa Ftancisko, Jumatano 13 Septemba 2023 mara baada ya katekesi, katika Uwanja wa Mtakatifu Petro. Kwa mujibu wa Padre huyo amesema “Wakati tunapopata ugumu sana huko Ukraine tuko hapa kutokana na kibali maalum cha kuwachukua wanaseminari na wafundaji wote nje ya nchi, ambayo, kwa sababu ya kuandikishwa, haiwezekani kwa watu wa Ukraine wenye umri wa miaka 18 na zaidi ya miaka 60 kutoka nje. Kwa hivyo, pia tulifanya hija kusherehekea miaka kumi ya kuundw akwa mfuko wa seminari."
Makundi yalikuwa mengi ambayo yamemfuahia Baba Mtakatifu hata akwa ua kati ya waamini kutoka bara la Asia.
Vile hata makundi mengine ya mahujaji kutoka bara la Afrika.