Tafuta

Papa alikutana na Maaskofu wa Kigiriki-Katoliki wa nchi za Ulaya  ambao wanafanya Sinodi hadi 13 Septemba 2023 mjini Roma. Papa alikutana na Maaskofu wa Kigiriki-Katoliki wa nchi za Ulaya ambao wanafanya Sinodi hadi 13 Septemba 2023 mjini Roma.  (ANSA)

Papa Francisko:Ukraine inakabiliwa na kifo cha kishahidi ambacho

Papa Jumamtano 6 Septemba 2023 alikutana na Maaskofu wa Kigiriki-Katoliki wa nchi za Ulaya waliokusanyika katika siku hizi kwa Sinodi yao:vita ni vya kishetani vinaondoa tabasamu za watoto,alisema.Rozari kwa mwezi wa Oktoba ni maalum kwa ajili ya amani na mwisho wa mzozo.

Na Alessandro De Carolis - Vatican

Janga la kikatili na la jinai pamoja, ambalo lenyewe lina mwelekeo wa mauaji ambayo hakuna mazungumzo ya kutosha. Ndiyo umakini wa Papa na aliyeguswa moyo ambaye kwa karibu saa mbili, kabla ya kuteremka kwenye Uwanja wa Mtakatifu Petro kwa ajili ya Katekesi yake alisikiliza, kutoka kwenye vinywa vya maaskofu wa Sinodi ya Kanisa Katoliki la Kigiriki-Kiukreni kwa maelezo ya maumivu ya kutisha ya vita na ya idadi yake ya watu waliokufa, waliojeruhiwa, walioteswa ambayo anafafanua kuwa kitu cha shetani, ambacho anataka kuharibu.

Vita huondoa tabasamu kutoka kwa watoto

Kwa mujibu wa taarifa ndefu kutoka Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican, Papa Francisko alishiriki katika janga ambalo ushuhuda kutoka sehemu mbalimbali nchini Ukraine zimeletwa mbele yake na “kwa hatua chache za uingiliaji kati”  na hivyo ameelezea hisia zake za ukaribu na wakati huo huo “hisia ya ukosefu wa nguvu unaopatikana mbele ya vita”, hasa historia inapogusa watoto wadogo. Papa alifikiria nyuma ya watoto wa Kiukraine aliokutana nao “ambao alisema  wanapokutazama wamesahau tabasamu lao. Hii ni moja ya matunda ya vita ya kuondoa tabasamu kutoka kwa watoto”, Papa alisisitiza.

Kuweka wakfu rozari ya Oktoba kwa ajili ya amani nchini Ukraine

Mtu ambaye ameteseka kwa  ukatili wa vita na haja ya maombi zaidi, kwa ajili ya uongofu na mwisho wa mgogoro ambapo Papa anawasindikiza na shauku ya  kutimiza ombi alilopokea wakati wa mkutano, au tuseme kwamba katika mwezi wa Oktoba, hasa katika mahali patakatifu, sala ya rozari na iwe kwe wakfu kwa ajili ya amani na amani katika Ukraine. Mazungumzo hayo pia yaligusa baadhi ya kutoelewana kwa upande wa Ukraine kutokana na kauli fulani za Papa, kama zile zilizotolewa wakati wa mazungumzo kwa njia ya video na Warussi vijana  mnamo tarehe 25 Agosti iliyopita. Papa Francisko alirudia kusema kwa Maaskofu kile alichokuwa amewaambia waandishi wa habari wakati wa kurudi kutoka Mongolia kuhusu maneno yake juu ya mada ya Urussi Kubwa, dhana ambayo alielewa katika muktadha huo kwa maana ya kiutamaduni.

Watu wanataka tuwe wajasiri kama Yesu katika Mateso

Kile ambacho  Ukraine inapaswa kukiangalia katika awamu hii ya kutisha ya historia yake  kwa mujibu wa Papa ni  “mfano wa Yesu wakati wa Mateso, ambaye hakubaki kuwa mwathirika wa matusi, mateso na Kusulubiwa, bali alishuhudia ujasiri wa kusema ukweli; kuwa karibu na watu, ili wasivunjike moyo. Si rahisi , Papa Francisko anakubali kuwa  huu ni utakatifu, lakini watu wanataka tuwe watakatifu na walimu wa njia hii ambayo Yesu alitufundisha. Akimwomba Mama Yetu Maria mwishoni mwa mkutano huo, Papa, alihitimisha taarifa hiyo, akiwaambia maaskofu jinsi ambavyo kila siku anakumbuka Waukraine katika sala yake mbele ya picha ya Bikira aliyopewa na Askofu Mkuu Sviatoslav Shevchuk, kabla hajaondoka huko Buenos Aires nchini Argentina.

Papa na maaskofu wa Ukraine wa ibada ya kigiriki katoliki
06 September 2023, 18:19