Papa ametoa mwito wa kuombea Ukraine inayoteseka na vita!
Na Angella Rwezaula, -Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko Jumatano tarehe 27 Septemba 2023 amerudia kutoa ombi lake kwa wakati wa kumaliza katekesi na akiwa katika kutoa salamu kwa waamini na mahujaji waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro kuwakumbuka kaka na dada zetu wa Ukraine ambao wamelazimika kuondoka katika nchi yao iliyokumbwa na vita, na wanaotafuta msaada, kimbilio na nia njema.
Na wakati huo huo Papa Francisko aliwatia moyo waamini wanaozungumza lugha ya Kipoland ili waendelee kuwakaribisha majirani zao wa Ukraine waliolazimika kukimbia kutokana na vita. Papa amesema kwa wapoland hao: “Wanapotafuta msaada, wakimbizi, wapate ukarimukatika nchi yenu.”
Ikumbukwe tangu kuanza kwa vita nchini Ukraine, wakati Urussi ilipovamia mwezi Februari 2022, Baba Mtakatifu ametoa miito mingi kwa ajili ya kuwasaidia watu wa Ukraine wanaoteseka, kukomesha vita na kwa jitihada zote za kurejesha amani. Poland imekuwa mstari wa mbele katika mataifa yanayowakaribisha na kuwasaidia wakimbizi wa Ukraine tangu mwanzo wa vita.
Akiwageukia wanahija kwa lugha ya kiitaliano amewasalimia wote na zaidi ametoa wazo kwa vijana, wagonjwa, wazee na wanandoa wapya. Amekumbusha siku ya Kumbukizi katika kiliturujia Mtakatifu Vincenti wa Pauli ambaye amesema “anatukumbusha kiini cha upendo wa ndugu. Papa amewashauri kila mmoja kukuza mtindo wa umakini kwa wengine na kwa ufunguzi wa wale ambao wanahitaji msaada kutoka kwetu.” Hatimaye amewabariki wote.