Papa huko Mongolia,ishara ya ujumuishaji na kupinga mantiki ya vita
Vatican News.
Ulimwengu wa haki zaidi na wa kidugu tofauti na mantiki ya vita, ambayo huweka masilahi ya wahusika mbele ya haki na ulinzi wa hadhi ya mwanadamu ndiyo maneno aliyomwelekea Papa Francisko kutoka kwa Rais Sergio Mattarella wa Jamhuri ya Italia kuhusiana na ziara yake ya kitume Mongolia, ambaye alitua katika mji mkuu Ulaanbaatar wakati Italia ilikuwa ni usiku wa manane tarehe 1 Septemba 2023. Katika ujumbe wa kiutamaduni akijibu telegramu iliyotumwa na Papa Francisko wakati wa ziara yake, Rais wa Jamhuri ya Italia anathibitisha kwamba hija, iliyoongozwa na kauli mbiu rasmi na nguvu ya matumaini, inatoa ushuhuda wa kujitolea bila kuchoka kwa kupendelea mazungumzo, ujumuishi na kuishi pamoja kwa ajili ya amani kati ya watu ya Papa wa kwanza kusafiri kwenda nchi ya Asia.
Ujasiri kwa ulimwengu wa kidugu zaidi
Akirejea hasa katika mkutano wa kiekumeni na wa kidini atakaofanya Baba Mtakatifu Dominika tarehe 3 Septemba 2023, Rais Mattarella amebainishaa kwamba “uwepo wa Papa utawatia moyo wale wote, waamini na wasioamini, ambao wanataka kufanya kazi kwa ajili ya ulimwengu wa haki na wa kidugu zaidi kupinga mantiki ya vita, ambayo inatanguliza maslahi ya kivyama mbele ya haki na ulinzi wa hadhi ya binadamu.”
Salamu za Papa kwa Italia
Tukumbuke kuwa katika telegramu kwa mkuu wa taifa wa Italia, Baba Mtakatifu Francisko alikuwa amesema kwamba aliandamana na salamu na matashi mema kwa taifa kwa matumaini kwamba manufaa wote yawe kipaumbele na kwa maombi kwa Mungu kusaidia wale wanaofanya kazi na mipango ya mshikamano.”