Papa akutana na wakuu wa Vyuo Vikuu vya Amerika Kusini na Carribean
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Siku ya Alhamisi, tarehe 21 Septemba, Baba Mtakatifu Francisko alikutana katika ukumbi wa Clementina, mjini Vatican, takriban na washiriki 200 katika mkutano wa wakuu wa Vyuo Vikuu vya umma na binafsi vya Amerika ya Kusini na Karibiani, uliohamaishwa na Chuo Kikuu cha Red cha Ulinzi wa Kazi ya Uumbaji (RUC) na Tume ya Kipapa ya Amerika ya Kusini (Pcal) tarehe 20 na 21 Septemba katika Chuo Kikuu cha Baba wa Kanisa cha Agostino yenye mada “Kuandaa Tumaini” kwa kushirikisha baadhi ya wakuu na makatibu wa Mabaraza ya Kipapa.
Akitafakari masuala mbalimbali yanayotolewa na waelimishaji yakiwemo mabadiliko ya tabia nchi, uhamiaji, utamaduni wa upotevu, Baba Mtakatifu amewataka kuwa wabunifu katika kuwafunza vijana kuanzia hali halisi na changamoto za sasa. Rectors waliuliza Papa maswali juu ya masuala ya mazingira na hali ya hewa ambayo yeye alijibu kwa kusisitiza kusikitisha "utamaduni wa kutupa au utamaduni wa kutelekezwa". Alieleza kuwa ni "utamaduni wa matumizi yasiyofaa ya maliasili, ambayo haiambatani na asili kwa maendeleo kamili na hairuhusu kuishi. Utamaduni huu wa kuachwa - alisema - unatudhuru sisi sote". Papa alitoa hata jina la Waraka Mpya wa kitume kuwa ni “Laudate Deum.