Ukaribu na upendo kutoka kwa Papa kwa Tamasha la Mediterranea
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Katika ujumbe ambao Baba Mtakatifu Francisko aliutuma kwa Padre Mattia Ferrari, anayejihusiana na masuala ya ukoaji wa kibinadamu katika bahari ya Mediterranea kwa ajili ya Tamasha la Shirika hilo lisilo la Kiserikali i (NGO,) lililoanzishwa na Luca Casarini, ambalo lililofunguliwa mnamo tarehe 7 Septemba 2023 mjini Roma, Papa ameandika kwamba: “Ninawatumia nyote salamu za dhati nikiwahakikishia ukaribu wangu na mapenzi. Ninawaombea, na tafadhali mniombee hivyo.”
Maneno ya Baba Mtakatifu ni namna ya kuwatia moyo wale wanaosafiri baharini kila siku na meli ya ‘Mare Jonio’ kusaidia wahamiaji wanaojaribu kufika Ulaya kutoka Afrika. Ni makumi ya wafanyakazi wa kujitolea wa Mediterranea ambao wamewasili kutoka Italia yote katika Jiji la Uchumi Mwingine Roma ili kujadili hali halisi ya wahamiaji.
Na pia aliyezungumza nao ni Kadinali Matteo Zuppi, rais wa Baraza la Maaskofu wa Italia, (CEI) na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Bologna Italia ambaye pia ali piga picha na wahudumu wa kujitolea wa Shirika lisilo la Kiselikali (NGO.) Kwa mujibu wake Kadinali Zuppi alisema: “Huwezi kufa kwa matumaini" na kusisitiza jinsi ambavyo mwanabinadamu lazima asitambulishwa kwa wema wa kufanya na kuhojwa. Kardinali alionesha kuwa katika ubinadamu kuna dharua ambayo si chochcote zaidi ya kujihusisha kwa sababu kuna kutojali ambao sio ushirikiano. Kwa hiyo “hakuna ushirikiano na hakuna kufanya mambo kwa sababu ni rahisi," alisema Rais wa CEI na kutoa onyo kuwa hakuna haja ya kuhoji kanuni ya kuokoa maisha bali kujitoma kujitolea zadi na hivyo baadaye alishukuru sana shirika hilo la kimediterranea kwa kujitolea kuongeza ufahamu wa hali nyingi kuhusiana na wahamiaji.