Vyombo vya habari Ufaransa vya tazama ziara ya Papa Marsiglia
Na Padre Paul Samasumo – Marseille
Baada ya kuwasili Marsiglia siku ya Ijumaa, Septemba 22,Papa Francisko alitua katika ardhi, mara moja akizindua shughuli zilizopangwa katika ziara hii ya mwisho wa Juma katika mji wa kusini mwa Ufaransa. Hata hivyo matokeo ya ziara ya Papa Francisko yalionekana wazi kama vile katika vyombo vya habari vya Ufaransa, ambavyo kwa kawaida vilinyamaza kuripoti juu ya mambo ya kidini, ambayo hata hivyo yalionekana kuvutia kila kitu ili kufunika ziara ya Papa Francisko, hasa mara tu baada ya kuwasili kwake. Kwa muda, hata hivyo michezo ya Raga ya Dunia kwa mwaka 2023 ndiyo ilionekana kuchukua nafasi ya pili.
Kwa njia hiyo tangu kuwasili kwake, vituo kadhaa vya televisheni vimebeba matangazo ya ukuta na mabango yanayoonesha ziara ya Papa Francisko huko Marsiglia. Kituo cha televisheni kinachomilikiwa na serikali cha ‘France 24’, ambacho ni chaneli ya habari na masuala ya mbashara chenye mawasiliano ya kimataifa, kimulika habari zake Jumamosi asubuhi 23 Septemba kwenye ukumbusho wa Papa Francisko kwa serikali za Ulaya kwamba “wana jukumu la kuwaokoa wahamiaji katika hali hatari baharini.”
Papa Francisko alipowasilia alitoa hotba zake ambapo alisisitiza kwamba kuwaokoa wahamiaji ni wajibu wa ubinadamu. ‘Le Figaro’, mojawapo ya magazeti ya zamani zaidi ya Ufaransa, ilifuatilia njia sawa ya uhariri, ikirudia juu ya ujumbe wa Papa Francisko dhidi ya kulazimishwa kurudi kwa wakimbizi, wahamiaji au wanaotafuta hifadhi. ‘La Provence’, nalo ni moja ya majarida maarufu yaliyochapishwa huko Marsiglia, limezungumza juu ya Papa katika kukabiliana na ajali ya meli ya kutojali kuhusu kifo cha wahamiaji baharini.
Kwa upande mwingine, gazeti la Ufaransa linalosambazia watu wengi, ‘Le Monde’, lilichukua mtazamo wa kutatanisha zaidi, likisema kwamba ziara ya Papa huko Marsiglia ni kumulika uhusiano mgumu wa Papa Francisko na watu wa Ufaransa. Gazeti hilo pia lililalamikia ulinzi na usalama uliozidi kiasi uliowekwa kwa ajili ya ziara ya Papa Francisko na Rais Emmanuel Macron katika mji wa bandari. Kwa ujumla, mtazamo wa vyombo vya habari katika Siku ya kwanza ya ziara ya siku mbili ya Papa Francisko ulikuwa mzuri na wa heshima.