Ziara ya Kitume Mongolia:Papa akutana na viongozi wa kidini
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Tofauti kati ya kila mmoja na kuungana pamoja katika makao ya geri kubwa ambayo ni Uwanja wa Tamasha la michezo(Hun Theatre) huko Ulaanbaatar, dini kuu za ulimwengu zilizopo nchini Mongolia zimemkaribisha Baba Mtakatifu Dominika tarehe 3 Septemba 2023 kabla ya hotuba yake wakati wa mkutano wa kiekumeni na kidini, katika ziara ya 43 ya kitume. Kwa njia hiyo kinachounganisha madhehebu yote, kwa mujibu wa maelezo katika salamu za awali kutoka kwa kiongozi wa Wabudha wa Kimongolia Gabju Choijamts Demberel, alisema ni sala na shughuli kwa madhumuni ya pamoja, yale ya ustawi wa ubinadamu.
Katika ulimwengu ambapo ubinadamu umefikia kiwango cha kipekee cha maendeleo katika habari na teknolojia, alisisitiza pia Khamba Nomun Khan na abate wa monasteri ya Gandan Tegchenling, kuwa kuna uwezekano wa hatari ya kupoteza maadili muhimu ya ndani kama vile fadhili, huruma, maadili, uvumilivu, msamaha na karma. Kwa hiyo, malengo na shughuli za dini zote za jadi lazima zijaze akili na maadili ya ndani yaliyotajwa, ili kuchangia kuundwa kwa jamii yenye hadhi na huruma. Ubuddha uliopitishwa nchini Mongolia kati ya karne ya pili na ya kwanza KK na kufutwa na asilimia 53% ya wakazi wa Mongolia, ulizaliwa upya, pamoja na madhehebu mengine, na kurejeshwa kwa uhuru wa kidini baada ya mwisho wa ukomunisti mnamo 1992. Historia ya mateso na kufungwa pia ilisimuliwa na paroko wa Kanisa pekee la Kiorthodox la Urussi huko Mongolia, lililowekwa wakfu kwa Utatu Mtakatifu wa Upatriaki wa Moscow na kuhudhuriwa na waamini wapatao mia mbili. Padre aliyekuwepo kwenye mkutano huo ni mmoja wa viongozi kumi na mmoja wa kidini waliompatia salamu Papa Francisko katika tukio hilo.
Danbajav Choijilav, abate mkuu wa nyumba ya watawa ya Zuun Khuree Dashicholing pia alizungumza kwa niaba ya Wabudha wa Mongoli, huku akisisitiza jinsi amani na maelewano ilivyo kanuni mbili zinazodumisha maisha ya mwanadamu, kama vile nguzo mbili zinazounga mkono geri ya Kimongolia. Kiukweli, geri yaani Nyumba ya kijadi kwa maneno ya D. Jargalsaikhan, rais wa Muungano wa Shamans wa Mongolia ni sehemu ndogo ya ulimwengu mkubwa, lakini ina michakato yote ya maisha ya mwanadamu, uhuru, na kuishi kwa mwanadamu na asili, kielelezo cha amani na hata sanamu zao, alisisitiza. Pamoja na ukaribu wa 3% ya waamini kati ya idadi ya watu, ibada ya jadi ya shaman ya ‘Mbingu ya Milele’, ambayo kiongozi wake amefafanuakuwa “ ni kama sehemu ya uhusiano wa kitovu kati ya asili ya dunia na ulimwengu, iliyokuzwa na kupitishwa tangu uumbaji wa mwanadamu”, ni dini ya tatu inayofuatiliwa zaidi nchini Mongolia, ikiwa na wafuasi elfu chache kuliko Uislamu.
Kufanana kati ya maelewano yanayohitajika ili kuishi katika nyumba ya jadi ya Wamongolia na yale ambayo ubinadamu unahitaji kuishi pamoja bila mzozo kwa hiyo pia ulikumbukwa na kiongozi wa Waislamu wa Kimongolia. Kwa mujibu wake alisema “Ulimwengu ni janga,na ili kuweka ulimwengu kuwa utaratibu na amani katika nyumba hii lazima tuishi pamoja kama ndugu.”Alisisitiza. Aidha “Geri ya Kimongolia ni mahali pazuri pa ushirika pia ilisisitizwa na Adiyakhuu Oktyabri, wa Kanisa la Waadventisti Wasabato, kwamba siku zote wako wazi kwa kila mtu na mahali pazuri pa kuishi ili kuunda mbingu ndogo duniani.” Wakati huo Geri inawakilisha kimbilio na umoja kama alivyosema, kiongozi wa Kanisa la Mormoni na ambaye aliwaalika watu kujikabidhi kwa Yesu kama wahamiaji wa nyika miongoni mwao.
Siku chache kabla ya Mwaka Mpya wa Kiyahudi, Yair Jacob Porat alitoa wito wa uwajibikaji wa pamoja wa kuifanya dunia kuwa mahali pazuri zaidi, akiwahimiza watu binafsi kushiriki, bila kujali itikadi zao za kidini, katika vitendo vya "adhili, upendo na haki ya kijamii. Kiongozi huyo wa Kihindu kwa upande wake alimshukuru Papa kwa kuwa mwanga wa matumaini na baraka zake ambazo zimebadilisha maisha ya watu wengi. Ujumbe na salamu pia ulitoka kwa Umoja wa Shirikisho la Kiinjili wa Kimongolia, kutoka katika jumuiya ya Shinto na kutoka katika jumuiya ya Bahà'ì. Naye Dambajav Choijiljav, abate mkuu wa Monasteri ya Zuun Khuree Dashichoiling, mojawapo ya mahekalu makubwa zaidi ya Kibudha huko Ulaanbaatar, alikuwa kwenye mkutano huo wa kiekumeni na wa kidini na Baba Mtakatifu Francisko. Kwa upande wake alisema anapatana na Papa katika kutafuta mema ya wote kwa hiyo “ Lazima tushirikiane katika hili. Kisha alizindua kwa upya wito wa Papa juu ya ya kazi ya pamoja ya kidini dhidi ya ufisadi.
Kwa mujibu wake alisema “Papa amekuja kati yetu na kwa hivyo jambo la kwanza ni kuweza kukutana naye. Alikuja kuzungumza juu ya amani na kipengele cha kidini na maisha ya mwanadamu. Jana alitoa tamko dhidi ya ufisadi ambalo tunaungana nalo kwa sababu Ubudha daima umekuwa dhidi ya ufisadi. Ni uovu unaopaswa kudhibitiwa na kisha kukomeshwa kwa sababu una athari mbaya kwa jamii nzima.” Kwa upande wa Khamba Lama, Dambajav Choijiljav, ambaye ni abate mkuu wa Monasteri ya Zuun Khuree Dashichoiling, mojawapo ya mahekalu makubwa ya Kibudha huko Ulaanbaatar yenye zaidi ya watawa 150, Monasteri ya Pili baada ya Monasteri ya Gandan Tegchenling yenye (watawa 400). Lakini hata hivyo Dambajav Choijiljav ndiyo kongwe zaidi, thamani ya Ubuddha, na kwa hivyo ni sehemu ya marejelo ya jumuiya ya Wabuddha wa Tantric wa Tibet, dini iliyo na watu wengi nchini Mongolia.