Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Kardinali Telesphore Placidus Toppo, Askofu mkuu Mstaafu wa Jimbo kuu la Ranchi, nchini India. Baba Mtakatifu Francisko amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Kardinali Telesphore Placidus Toppo, Askofu mkuu Mstaafu wa Jimbo kuu la Ranchi, nchini India. 

Tanzia: Kardinali Telesphore Placidus Toppo, 84 Amefariki Dunia

Baba Mtakatifu Francisko amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Kardinali Telesphore Placidus Toppo, Askofu mkuu Mstaafu wa Jimbo kuu la Ranchi, lililoko nchini India, kilichotokea tarehe 4 Oktoba 2023 akiwa na umri wa miaka 84. Alizaliwa mwaka 1939, akapewa Daraja Takatifu ya Upadre tarehe 3 Mei 1969, Akawekwa wakfu kuwa Askofu, tarehe 7 Oktoba 1978. Mwaka 1985 akateuliwa kuwa Askofu mkuu na mwaka 2003 akateuliwa kuwa ni Kardinali.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Kardinali Telesphore Placidus Toppo, Askofu mkuu Mstaafu wa Jimbo kuu la Ranchi, lililoko nchini India, kilichotokea tarehe 4 Oktoba 2023 akiwa na umri wa miaka 84. Baba Mtakatifu katika salam zake za rambirambi alizomwandikia Askofu mkuu Felix Toppo wa Jimbo kuu la Ranchi, India anamwomba, awafikishie salam zake za rambirambi watu wote wa Mungu Jimbo kuu la Ranchi. Anaungana nao ili kuiombea roho ya Marehemu Kardinali Telesphore Placidus Toppo, ionje na kupata huruma ya Mungu. Baba Mtakatifu anamkumbuka Marehemu Kardinali Telesphore Placidus Toppo, kwa sadaka na majitoleo yake kama Padre na katika Daraja takatifu ya Uaskofu, katika kuongoza, kufundisha na kuwatakatifuza watu wa Mungu Jimbo kuu la Ranchi, India.

Hayati Kardinali Telesphore Placidus Toppo amefariki dunia 4 Oktoba 2023
Hayati Kardinali Telesphore Placidus Toppo amefariki dunia 4 Oktoba 2023

Marehemu Kardinali Telesphore Placidus Toppo alichangia sana katika ustawi, maendeleo na mafao ya Kanisa la India na Kanisa la Kiulimwengu. Ni kiongozi aliyejitanabaisha kwa kupenda kutangaza na kushuhudia Habari Njema ya Wokovu, kukuza na kueneza Ibada ya Kuabudu Ekaristi Takatifu pamoja na huduma makini kwa maskini na wale wote waliokuwa wanasukumizwa pembezoni mwa jamii. Baba Mtakatifu anapenda kutoa faraja na baraka zake za kitume kwa wale wote wanaoomboleza na walioguswa na msiba huu mzito, huku wakiwa na matumaini ya ufufuko na uzima wa milele. Kutokana na kifo cha Kardinali Telesphore Placidus Toppo, Baraza la Makardinali sasa linaundwa na Makardinali 241, kati yao kuna Makardinali 136 wenye haki ya kupiga na kupigiwa kura kuwa ni Makhalifa wa Mtakatifu Petro na hao wengine 105 hawana tena sifa ya kupiga au kupigiwa kura wakati wa uchaguzi wa Khalifa Mtakatifu Petro.

Watawa wakimwombelezea Kardinali Toppo
Watawa wakimwombelezea Kardinali Toppo

Marehemu Kardinali Telesphore Placidus Toppo alizaliwa tarehe 15 Oktoba 1939 huko Chainpur, Jimbo Katoliki la Gumla, India. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 3 Mei 1969 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tarehe 8 Juni 1978 akateuliwa kuwa Askofu na kuwekwa wakfu tarehe 7 Oktoba 1978. Tarehe 8 Novemba 1985, Mtakatifu Yohane Paulo II akamteuwa kuwa ni Askofu mkuu mwandamizi mwenye haki ya kurithi Jimbo kuu la Ranchi, India. Akasimikwa rasmi kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Ranchi tarehe 25 Agosti 1985 na kuliongoza Jimbo kuu la Ranchi hadi tarehe 24 Juni 2018 alipong’atuka kutoka madarakani. Akiwa madarakani aliweza kuhudhuria na kushiriki katika maadhimisho mbalimbali ya Sinodi za Maaskofu. Mtakatifu Yohane Paulo II akamteuwa kuwa Kardinali mwaka 2003. Na ilipogota tarehe 4 Oktoba 2023, Kardinali Telesphore Placidus Toppo akaitupa mkono dunia! RIP.

Kardinali Toppo
06 October 2023, 15:24