Tafuta

2023.10.10 Rais Mtaafu László Sólyom, wa Hungeria ameaga dunia 2023.10.10 Rais Mtaafu László Sólyom, wa Hungeria ameaga dunia 

Papa atuma salamu za rambirambi kwa kifo cha rais wa zamani wa Hungaria

Rais Mstaafu wa Hungaria aliyekuwa madarakani kuanzia 2005 hadi 2010,alifariki tarehe 8 Oktoba 2023 akiwa na umri wa miaka 81 baada ya kuugua kwa muda mrefu.Katika telegram kwa rais wa sasa wa Hungaria Bi Novak,Papa Francisko anatoa rambirambi zake na kumwomba Mungu ili "amkaribishe marehemu kwa amani yake."

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko Jumanne tarehe 10 Oktoba 2023 ametuma salamu za rambirambi kuafuatia na kifo cha László Sólyom, aliyekuwa rais Mstaafu wa Jamhuri ya Hungaria kuanzia mwaka 2005 hadi 2010. Marehemu Sólyom aliaga dunia Dominika tarehe 8 Oktoba  2023 akiwa na umri wa miaka 81, kufuatia kuugua kwa muda mrefu. Katika telegramu kwa Rais wa Hungaria Bi Katalin Novák, Baba Mtakatifu Francisko anatuma salamu za rambirambi kwa serikali na watu wa nchi ya Hungari ambayo alitembelea kuanzia tarehe 28 hadi 30 Aprili 2023.

Baba Mtakatifu katika telegramuhiyo anaandika kuwa, "Ninaomba kwa moyo wangu wote kwa Mungu ampokee  marehemu katika amani yake na awape wote faraja ya matumaini walioguswa na kifo chake, hasa familia yake. Mungu ibariki Hungaria na watu wake wote." Unahitimishwa  hivyo ujumbe huo wa Papa.

 

10 October 2023, 15:11