AFGHANISTAN-LIFESTYLE

Papa Francisko:Mitindo ya uchumi inayojumuisha walio hatarini zaidi iendelezwe

Papa alituma ujumbe katika hafla ya mkutano wa”hakuna aliyetengw;Kukua pamoja katika nchi iliyo sawa zaidi uliohamaishwa na Bank ya Intesa:"fedha ni sanaa ambayo msingi wake ni uaminifu katika mahusiano na ambayo inaweza kujengwa tu kupitia maendeleo ya utamaduni wa kukutana,anasema Papa.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Fedha ni sanaa ambayo msingi wake ni uaminifu katika mahusiano ambayo inaweza kujengwa tu kupitia maendeleo ya utamaduni wa kukutana. Ni maneno kutoka  Ujumbe wa Papa. Ujumbe huo umekuwa kama mwendelezo wa mada pendwa na mafundisho ya Mapapa katika zama za utandawazi wa masoko, uchumi na fedha unaoelekezwa kwa ajili ya manufaa ya wote na kuheshimu utu na hadhi ya binadamu. Kwa hiyo  imekuwa hivyo kila mara kwa Baba Mtakatifu Francisko ambaye amerudia tena katika ujumbe uliotumwa kwa Carlo Messina, Mkurugenzi Mtendaji wa Bank ya  Intesa , Italia, katika fursa ya tukio la Mkutano ulioongozwa na kauli mbiu: "Hakuna aliyetengwa. Kukua pamoja katika nchi iliyo sawa zaidi" uliofanyika tarehe 26 Oktoba 2023 na wakati huo huo Sr. Alessandra Smerilli, Katibu Mkuu wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Kuhamasisha Maendeleo Fungamani ya Binadamu alikuwa kati ya washiriki  na ambaye alisoma ujumbe wa Papa.

Kuimarisha mchakato wa Ujumuishaji wa kiuchumi

Ushauri wa  Papa Francisko kama tunavyosoma  katika ujumbe huo, ni kuimarisha mchakato wa ujumuishaji wa kiuchumi na kijamii unaolenga umakini maalum kwa wahamiaji dhaifu na,  wa kwanza kabisa, na kwa utekelezaji wa kushuka kwa idadi ya watu katika uendelevu wa mipango ambayo lazima wapate wahusika wakuu kama vijana na wazee,na wafanye kama dawa ya kuzuia utamaduni wa kutupa.”

Sababu za sanaa ya mikopo na fedha ni kutokana na imani na matumizi yake

Papa Francisko aidha katika ujumbe huo  anakumbuka kwamba sababu za awali na motisha za sanaa ya mikopo na fedha zinatokana na imani na matumizi ya fedha kama maisha ya mfumo wa kiuchumi, ni kwa sababu  kila mtu apate uwezekano wa kufanikiwa. Sanaa ambayo, inahitaji imani, mahusiano na ambayo Papa Francisko anatumaini  kuwa itajengwa tu kupitia maendeleo ya utamaduni wa kukutana ambapo kila sauti inaweza kusikika na kila mtu anaweza kufanikiwa, kutafuta sehemu za pamoja za kuwasiliana, kujenga madaraja na kufikiria mipango  shirikishi ya muda mrefu.”

26 October 2023, 16:58