2023.10.20 Kitabu cha mapadre Wadominikani Timothy Radcliffe na Łukasz Popko chenye kichwa:'Maswali ya Mungu,Maswali kwa Mungu' (LEV). 2023.10.20 Kitabu cha mapadre Wadominikani Timothy Radcliffe na Łukasz Popko chenye kichwa:'Maswali ya Mungu,Maswali kwa Mungu' (LEV). 

Papa Francisko:Neno la Mungu linazungumza tena na kuuliza maswali!

Oktoba 31,kitabu chenye dibaji ya Papa:"Maswali ya Munungu,maswali kwa Mungu.Mazungumzo na Biblia”,kilichoandikwa na Mapadre wa Kidominikani Timothy Radcliffe na Łukasz Popko kitatolewa na Nyumba ya vitabu,Vatican(LEV).Ni kitabu kinachotathimini maswali ambayo Mungu anauliza nwanaume na mwanamke.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Tarehe 31 Oktoba 2023 Kitabu cha mapadre Wadominikani Timothy Radcliffe na Łukasz Popko chenye kichwa: Maswali ya Mungu, Maswali kwa Mungu katika mazungumzo ba Biblia kitachapishwa na nyumba ya vitabu ya Vatican (LEV). Tarehe 29 Oktoba zilitolewa ndondoo mbili za mwanzo kutoka katika Gazeti la ‘Avvenire’ kuhusu utangulizi na kati Gagazeti la ‘La Lettura’(mahojiano na waandishi wa kitabu hicho pamoja na lengo la kitabu hicho.) Utangulizi huo ni kutoka kwa Papa Francisko,ambapo tunachapisha utangulizi huo jinsi ulimvyo:

Papa Francisko

Yesu alikuwa anauliza. Moja ya sentesi zake kwa mujibu wa Injili ya Yohane ilikuwa ni swali la “Mnatafuta nini!”, akiwageukia wanafunzi wa Yohane Mbatizaji ambao walikuwa wanafuata. Kwa misngi wa Mwinjili Luka neno la kwanza la Yesu lilikuwa hasa swali la wazazi wake, Yosef una Maria: “Kwa nini mlikuwa mnamnitafuta?” Na juu ya Msalaba baada ya kuhitimisha maisha yake hapa duniani akitumika kutangaza huruma ya Mungu, alimgeukia Baba yake kwa swali hili:“Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?” Na siyo  hiyo tu wakati wa kufufuka katika wafu, alijiwakilisha kwa Maria Magdalena kwa maswali mawili aliyomwelekeza: “Mwanamke, kwa nini unalia? Unamtafuta nani? Yesu alikuwa anapenda kuuliza maswali. Kwa sababu alikuwa anapenda kuzungumza na wanaume na wanawake wa wakati wake ambao walikuwa wanakusanyika wengi wakimzunguka kwa Mwalimu huyo wa kiyahudi wa ajabu ambaye alikua anazungumza ya Mungu na semina za Ufalme wa Mungu na hazina za shamba, ya mfalme anayekwenda vitani na ya karamu za vinywaji za kitajiri. Kwa wale waliokuwa wakisililiza Yesu walikuwa wanaelewa kuwa mazungumzo yake hayakuwa jukwaa la kejeli, lakini watu hasa kutoka moyoni, kwa namna ya kuombea kwa kina kila mmoja. Namna ya kujaribu kutoboa ganda la nafsi ili kuruhusu kuchuja manukato ya upendo.

Kitabu hiki ambacho ninashukuru watunzi wake, kinachunguza maswali kumi na nane kati ya maswali mbalimbali ambayo Mungu anauliza wanaume na wanawake katika Biblia, na kwamba wahusika mbalimbali wanauliza Mungu na Yesu. Swali ni ishara ya kibinadamu, ubindamu kabisa ambao unafanya kuonekana wazi shauku ya kujua, ya kufahamu, asili ya kila mmoja wetu kutoridhika na kile kilichopo, lakini kwenda zaidi, kufikia kitu, kwenda kwa kina juu ya mada. Wanaouliza maswali hawaridhiki. Wale wanaouliza maswali huhuishwa na hali ya kutotulia ambayo huakisi  kama dalili ya uhai. Mioyo iliyotosheka haiulizi maswali. Mwenye jibu juu ya yote hajiuliza maswali kuhusu lolote. Anafikiri  kuwa na ukweli mfukoni kama unavyotunza karamu mfukoni, tayari kuitumia. Mwenyeheri Pierre Claverie, Askofu wa Algeria, mdominikani kama walivyo waandishi wa kitabu hiki, shuhuda wa urafiki na mazungumzo na ndugu zetu waislamu alikuwa anapenda kurudia: Mimi ni mwamini, ninaamini kuwa Mungu yupo. Lakini sidai kummiliki, wala kupitia Yesu, ambaye hunifunulia, wala kupitia mafundisho ya imani yangu. Mungu hamilikiwi. Ukweli huwezi kuumiliki”.

Hapa, utafiti huu, hamu hii, shauku hii hutokea katika kuuliza maswali, kwa kuwa na maswali, katika kusikiliza maswali ya wengine. Tunajua vizuri: falsafa ilizaliwa kutokana na maswali makubwa ya kuwepo: “Mimi ni nani?”, “Kwa nini kuna kitu na sio chochote?”, “Ninatoka wapi?”, “Maisha yangu yanakwenda wapi?.” Ni kwa sababu hii kwamba Ukristo daima umejiweka karibu na wale wanaojiuliza, kwa sababu - nina hakika - Mungu anapenda maswali, anayapenda kweli. Nadhani anapenda maswali kuliko majibu. Kwa sababu majibu yamefungwa, maswali yanabaki wazi. Kama vile alivyoandika mshairi kuwa Mungu ni mkato,  si kuacha kamili: mkato unarejea kitu zaidi, husogeza mazungumzo mbele, huacha wazi uwezekano wa mawasiliano. Hoja inafunga mjadala, inamaliza mjadala, inasimamisha mazungumzo. Ndiyo, Mungu ni mkato. Na anapenda maswali. Kitabu hiki kinatuelimisha juu ya umuhimu wa kuchunguza maswali yetu. Yale yaliyo katika Biblia ni mazuri, yanachokoza na yanatusumbua. Mungu anamuuliza Adamu: “Uko wapi? ”Aliye Juu zaidi anamuuliza Kaini: “Yuko wapi ndugu yako?" Maria anauliza Malaika: “Itatokeaje?”Yesu anawauliza wafuasi wake: “Ninyi mwasema mimi ni nani?” Na hatimaye anamkasirisha Petro: “Je, unanipenda mimi zaidi ya hawa?” Hapa, kuuliza maswali kunamaanisha kubaki wazi kwa kukaribisha kitu ambacho kinaweza kutuvuka. Kutoa majibu pekee kunamaanisha kubaki kwenye maono yako ya mambo.

Maswali ambayo waandishi huchunguza kati ya kurasa za Maandiko pia hupitisha fundisho lingine kwetu: ubora na uaminifu wa kuuliza kwetu. Kuna wale ambao huuliza maswali ili kumweka mpatanishi katika shida na wale ambao, kama mtoto akizungumza na wazazi wake, humsikiliza kwa dhati mpatanishi, wakijua kuwa hajui. Wakati mwingine tunawauliza watu kwa kashfa, tukijaribu kumweka yule anayeingilia kati hatarini,  ikiwa anajibu kwa njia moja, sifa yake iko hatarini, akijibu nyingine anajisaliti mwenyewe. Ndiyo maana waandishi pia huchunguza baadhi ya maswali ya Biblia ambayo si ya dhati kama swali lolote linapaswa kuwa. Neno la Mungu ni mwalimu mkuu katika hili, kwa sababu, kama Mtakatifu Paulo anavyosema  kuwa ni upanga wenye ncha mbili kali hufunua ukweli wa moyo. Na ingawa unafunua utu wetu wa ndani kwetu, Neno linathibitisha kuwa linaweza kuwa la sasa, na siku zote: Mungu, katika Biblia, hasemi na kuwasiliana sio tu na wanaume na wanawake wa wakati ambao iliandikwa, lakini huzungumza na kila mtu, hata kwetu. Anaongea na mioyo yetu isiyotulia, ikiwa tunajua jinsi ya kumsikiliza.

Maswali ambayo waandishi huchambua na kujadili bado ni muhimu leo hii, yanatutikisa hadi msingi hata katika jamii yetu ya kidijitali, kwa sababu ni maneno ambayo kila moyo usio na ganzi unaweza kushika kama uamuzi kwa maisha yao wenyewe: niko wapi katika maisha yangu? Nimefanya nini na kaka na dada zangu katika ubinadamu? Je, inawezaje kutokea kwamba Mungu aje katika maisha yangu? Kwangu mimi Yesu ni nani? Ninajali nini kuhusu mtu huyo aliyejiita Mungu na ambaye alitoa maisha yake kwa ajili yangu? Neno la Mungu bado linazungumza nasi pamoja na maswali yake. Lakini si yeye pekee. Kama vile kitabu hiki kinavyoonesha vizuri, kila neno la mwanadamu, la kibinadamu, limejaa neno la kimungu. Karl Rahner aliandika kwamba “mwandishi kama huyo yuko chini ya ushawishi wa mwito wa neema ya Kristo na kwa hiyo lazima awe Mkristo; Kuwa mwandishi kwa ajili ya mwanaume ni ukweli muhimu wa Kikristo.”

Kurasa za kitabu hiki zinathibitisha hili: Utajiri wake wa marejeo ya kifasihi, ya kishairi na ya sinema yanarejea wingi wa kueleza unaoboresha mtazamo wetu juu ya imani. Vinatufanya tuelewe vizuri zaidi kauli ya Mtaalimungu wa Kijerumani: wakati ni mwanadamu kweli, wakati ni kielelezo cha hali halisi ya ndani ya mwanadamu, usemi wa kisanii huwa wa theophanic (onesho), kwa sababu anajua jinsi ya kufahamu muhimu, anajua jinsi ya kutoa sauti kwa neema, ina uwezo wa kuwasilisha fumbo. Kama vile mbele ya usiku wenye nyota au machweo ya jua, mioyo yetu haiwezi kusaidia lakini kumsifu Mungu, kwa hivyo mbele ya muziki wa  Bach au ukurasa wa Dostoevsky tunakuwa na hakika kwamba ulimwengu ni mzuri na kwamba maisha yetu yana maana. Huu ndio uwezo wa mawazo ya mwanadamu: kutuweka katika mawasiliano na Mungu.

Hatimaye, jambo la kuzingatia. Kitabu hiki kimejaa ucheshi. Ninadhani ni kipengele muhimu na cha kushukuru maradufu kwa waandishi. Kwanza kabisa kwa sababu ucheshi ni usemi wa kibinadamu unaokaribia sana neema. Ucheshi ni mwepesi, ni mtamu, unachangamsha nafsi na hutupatia matumaini. Wale ambao wana ucheshi mara chache kutowapenda wengine, wana uwezekano wa kuwa wakarimu, na wana uwezo wa kujilinganisha  mtu fulani aliandika hivi: “Heri wale wanaojua jinsi ya kucheka wenyewe, kwa sababu hawataacha kujifurahisha.” Na wakati huo huo, ucheshi, unapopatikana na mwamini, unaonesha jinsi imani ya Kikristo sio kitu cha kusikitisha au cha kunyoosha, sio kujitazama, wala kudhalilisha. Imani inazifanya nyuso za wale wanaoshikamana nayo kung'aa. Injili inatoa furaha, furaha ya kweli, si ile ya mwisho bila shaka, lakini furaha ya kweli: wale wanaoamini wana furaha, hawana uso kama wa  maombolezo. Mtu mwenye furaha, unaweza kuuona kwenye uso wake! Kwa hivyo, kutoka katika kitabu hiki, nasikia  miito mitatu ikiunga mkono: kwamba sisi waumini tunabaki bila utulivu, kila wakati tunaweza kujiuliza maswali na pia kuwa mtaalam mdogo wa ucheshi.

Dibaji ya Papa katika kitabu:Maswali ya Mungu,maswali kwa Mungu

 

30 October 2023, 09:12