Tafuta

Papa:Umoja,utamadunisho na uhuru ni njia za kuinjilisha na imani lazima itamadunishwe

Umoja,utamadunisho na huru ni mambo matatu msingi yaliyojitokeza katika Katesi ya Baba Mtakatifu Jumatano Oktoba 25,kwa waamini na mahujaji waliofika katika uwanja wa Mtakatifu Petro katika mwendelezo wa shauku ya Uinjilishaji.Sura ya Watakatifu Cyril na Mehodius mitume wa Waslavi imesikika kwa uhai.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko katika Mzunguko wa Katekesi kuhusu shauku ya Uinjilishaji: ari ya kitume ya mwamini, Jumatato tarehe 25 Oktoba 2023 amejikita na sura nyingine ya Wakatifu Cyril na Methodius, mitume wa Ulaya Mashariki (Waslavi). Ameanza tafakari hiyo mara baada ya kusomwa somo la Matendo ya Mitume (Mdo 11,2-4.15.17). Baba Mtakatifu Francisko akizungumzia ndugu hao  wawili maarufu katika Mashariki, amesema walifikia  hadi kuitwa: “Mitume wa Waslavi”: Mtakatifu Cyrily na Methodius. Walizaliwa huko Ugiriki katika Karne ya IX na familia inayojiweza (aristocratica) kwa kuacha kazi za kisiasa ili kujikita katika maisha ya kimonasteri. Lakini ndoto yao ya kuishi wamejitenga ilidumu kidogo. Wao walikuja kutumwa kama wamisionari katuka nchi ya Monravia Kubwa ambayo nyakati zile ilikuwa inajumuisha watu wa aina mbali mbali, ambapo tayari kwa sehemu kubwa  ilikuwa imekwisha injilishwa, lakini ikiwa bado wanaishi tamaduni na mila za kipagani. Mfalme wao alikuwa anaomba mwalimu ambaye angeelezea imani ya kikristo katika lugha yao.

Katekesi 25 Oktoba 2023
Katekesi 25 Oktoba 2023

Shughuli ya kwanza ya Cyril na Methodius ilikuwa ni kujifunza kwa kina utamaduni wa watu wale. Ni kiitikio daima kile kwamba imani lazima itamadunishwe na utamaduni wa kuinjilishwa. Utamadunisho wa imani,uinjilishaji wa tamadini daima”. Cyril aliomba ikiwa walikuwa na alfabeti; na walijibu kwamba hapana. Na yeye alijibu: “Ni nani anaweza kuandika hotuba juu ya maji.” Papa amesema “kwa hakika, ili kuweza kutangaza Injili na ili kusali ilikuwa inahitaji chombo hasa kinachofaa, na maalum. Kwa hiyo alivumbua namna hiyo alfabeti. Alitafsiri Biblia na maandiko ya kiliturujia. Watu walihisi kuwa imani ile ya kikristo haikuwa tena ya “kigeni”, bali  ikageuka kuwa imani yao na kuzungumza kwa lugha yao mama. Papa Francisko ameongeza kusema: “fikirieni: mamonaki wawili wa kigiriki walitoa alfabeti ya kislavi. Ndiyo ufunguzi huu ambao ulikita mzizi wa Injili kati yao. Hawakuwa na woga, watu hawa wawili kwani walikuwa wajasiri. Lakini mapema ilianza mivutano kutoka kwa baadhi. Ni Walatini ambao waliona ukiritimba wao wa kuhubiri miongoni mwa Waslavi ukiondolewa.

Hawakosekani wana ndoa wapya kati ya mahujaji
Hawakosekani wana ndoa wapya kati ya mahujaji

Mapambano  ndani ya Kanisa daima huwa hivyo. Upinzani wao ulikuwa wa kidini lakini ambao ulikuwa tu wa wazi, kwani  wao walisema kwamba: Mungu anaweza kusifiwa tu katika lugha tatu zilizoandikwa juu ya Msalaba: Kiyahudi, Kigiriki na Kilatino.” Hawa walikuwa na akili iliyofungwa ya kulinda kujitosheleza kwao”. Lakini Cyril alijibu kwa nguvu kuwa “Mungu anataka kila mtu asifu katika lugha yake. Pamoja na kaka yake Methodius, walimkimbilia Papa na hivyo  waliridhiwa maandishi yao ya kiliturujia katika lugha ya kislavi na kuiweka juu ya Altare ya Kanisa la Mtakatifu Maria Mkuu na kuimba nao Sifa za Bwana kwa mujibu wa vitabu vile. Baba Mtakatifu amesema kwamba Cyrily alifarika baada ya miezi michache na masalia yake bado yanaheshimiwa katika Basilika la Mtakatifu Clementi, jijini Roma. Methodius kinyume alipewa wakfu wa kiaskofu na kutumwa tena katika eneo la Waslavi. Hapo  aliteseka sana na  hata atafungwa, lakini  sisi sote tunatambua kuwa Neno la Mungu halikufungwa minyororo na lilienea kati ya watu wale.

Papa akisalimia mahujaji na waamini
Papa akisalimia mahujaji na waamini

Baba Mtakatifu Francisko amebainisha kuwa kwa kutazama ushuhuda wa wainjilishaji wawili hao  ambao Mtakatifu Yohane Paulo II alipendelea wawe Wasimamizi wenza wa Bara la Ulaya na ambapo juu yao aliandika: “Waraka wa Slavorum Apostoli, yaani Mitumwa Waslavi tuone  mantiki tatu muhimu. Awali ya yote amesema umoja: Wagiriki, Papa na Waslavi. Katika wakati ule barani Ulaya kulikuwa na Ukristo ambao haukugawanyika, ambao ulikuwa unashirikishana kuinjilisha.

Makund mbali mbali na nguo za kiutamaduni katika katekesi ya Papa
Makund mbali mbali na nguo za kiutamaduni katika katekesi ya Papa

Kipengele cha pili muhimu ni utamadunisho ambao alisema kitu kabla kwamba  utamaduni wa kuinjilisha na utamadunisho unaonesha kwamba uinjilishaji na utamaduni una uhusiano wa karibu. Huwezi kuhubiri Injili ya kidhahania, iliyosafishwa, hapana: Injili lazima izidishwe na pia iwe kielelezo cha utamaduni.

Kipengele cha mwisho, ni uhuru. Baba Mtakatifu amesema katika kuhubiri tunahitaji uhuru lakini siku zote uhuru unahitaji ujasiri, kadiri mtu anavyokuwa huru ndivyo anavyokuwa jasiri na hajiruhusu kufungwa na mambo mengi yanayomwondolea uhuru. Kwa kuhitimisha Papa amesema tuwaombe Watakatifu Cyril na Methodius, mitume wa Waslavi, kuwa vyombo vya "uhuru katika upendo" kwa wengine. Kuwa wabunifu, kuwa thabiti na kuwa wanyenyekevu, kwa maombi na kwa hudumia.

Katekesi ya Papa 25 Oktoba
25 October 2023, 13:09