Papa,Tamasha la VIII la Wahamiaji na wakimbizi:tuepuke mantiki za dunia,kujipendelea
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko ametuma ujumbe wake kwa washiriki wa Tamasha la VIII la Wahamiaji huko Modena na miji mingine ya Italia kuanzia tarehe 25 hadi 28 Oktoba 2023. Katika ujumbe huo anawasalimia wote katika Tamasha lenye kuongozwa na mada: “Uhuru wa kuhama, uhuru wa kubaki.”Amewapongeza kwa uhai wote waandaaji wa tukio hilo muhimu kati ya Mfuko wa Migrantes (Wahamiaji wa Baraza la Maaskofu Italia (CEI). Baba Mtakatifu aidha amekazia kusema kuwa katika Mada ya Tamasha hilo linachukua Ujumbe ule wa Siku ya Wahamiaji na Wakimbizi duniani kwa mwaka 2023, ambao ulijikita kuhusu uhuru wa kuchagua kuhama au kubaki. Katika hilo Papa anabainisha kuwa ni wazi zaidi kuhusiana na kuanzishwa michato ya mshikamano iliyohamasishwa mwaka mmoja uliopita na Baraza la Maaskofu Italia, ambayo analitaja hasa katika Ujumbe wake kama jibu la dhati katika changamoto za wahamiaji mamboleo.
Uhamiaji mamboleo
Katika kazi yao wanatafakari kuingia kwa uhamiaji mbamboleo kwa njia ya kufikiria kuwa inakwenda zaidi ya dharura, na utambuzi kwamba tunajikuta mbele ya matukio ambayo yanatazama dunia na suluhisho za muda mrefu. Hivyo majibu ya changamoto za uhamiaji leo hi hayawezi kutotazamiwa na mipango ya muda mrefu duniani. Katika hilo, wao wanapendekeza kuweka kiini cha mtu katika ishara ya kisiasa na mipango ya uhamiaji kuwa na umakini kwa namna ya pekee katika watu walio katika mazingira magumu kama vile wanawake na watoto wadogo. Kiukweli Papa anaongeza: “msingi wa mtu binadamu, na kutokiukwa hadhi yake, unatulazimisha kutafuta usalama daima wa kibinadamu na ule wa kitaifa.” (Ujumbe wa Siku ya wahamiaji na wakimbizi 2018). Na bado “ Yesu anatuomba tusiangukia katika mantiki za ulimwengu huu ambayo inahalalisha kuwaonea wengine kwa manufaa yangu binafsi au ya kundi langu: mimi kwanza na kisha wengine! Badala yake kauli mbiu ya Wakristo wa kweli ni kuanza na wa 'mwisho!”(Ujumbe wa Suku ya wahamiaji na wakimbizi 2019).
Kuendekeza juhudi za kukarimu na haki
Baba Mtakatifu Francisko amewatia moyo washiriki wote hawa waendeleze kwa dhati mipango hiyo ya kusaidia wahamiaji wa kuingia kihalali na kwa usalama. Katika hlo “ni lazima kuongeza zaidi nguvu za kupambana na mitandao ya kihalifu, ambayo inatumia kuharibu ndoto za wahamiaji. Lakini pamoja na hayo ni muhimu kuonesha njia salama. Kwa sababu hiyo, lazima tujitolee kupanua njia za kawaida za uhamiaji” (Ujumbe wa siku ya wahamiaji dunaini 19 Novemba 2023). Lakini wakati huo huo tunapaswa kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha kila mtu haki ya kutolazimika kuhama.
Watu wanahama kutokana na sababu
Papa Francisko amekazia kusema tena kuwa “Wahamiaji wanakimbia kutokana na umaskini, hofu na kukata tamaa. Ili kuondoa sababu hizo na hivyo kukomesha uhamiaji wa kulazimishwa, dhamira ya pamoja ya kila mtu ni muhimu, kila mmoja kulingana na majukumu yake. Ahadi ambayo huanza kwa kujiuliza tunaweza kufanya nini, lakini pia ni nini tunapaswa kuacha kufanya. Ni lazima tufanye kila tuwezalo kukomesha mbio za silaha, ukoloni wa kiuchumi, uporaji wa rasilimali za watu wengine, uharibifu wa makazi yetu ya pamoja. Papa anahitimisha ujumbe wake akiomba Bwana awabariki kazi yao na kwa maombezi ya Bikira Maria Mtakatifu awasaidia daima katika jitihada zao za kukarimu, kulinda, kuhamasisha na kufungamanisha wahamiaji na wakimbizi wote ambao wanabisha hivi milangoni kwetu.