Mapambano bado yanaendelea kati ya Israeli na Gaza. Mapambano bado yanaendelea kati ya Israeli na Gaza.  (ANSA)

Papa:mateka waachiliwe na misaada ipate kungia huko Gaza!

Papa Francisko katika salamu mbali mbali kwa mahujaji na wamini waliofika katika katekesi yake,amerudia kuzungumzia hali ya vita Nchi za Mashariki ya kati, Ukraine na kanda zote zilizojeruhiwa na vita ulimwenguni.Amekumbusha tukio la sala na kufunga na toba siku ya Ijumaa Oktoba 27 ili kuomba amani Ulimwenguni.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Majanga ya hali halisi katika Nchi za Mashariki ya kati zinaendelea kuwa wazo kuu  na maneno ya Baba Mtakatifu Francisko, mara baada ya tafakari ya Katekesi, na salamu zake Jumatano tarehe 25 Oktoba 2023 kwa mahujaji na waamini waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican. Kwa njia hiyo katika salamu zake akizungumza namahujaji wa Italia aliwageukia kwa mara nyingine wito wa amni, nchini Israel na Palestina, katika Ukraine na  Ulimwengu mzima.

Papa afikiria watu waliotekwa nyara

Maneno ya Baba Mtakatifu alisema: “Siku zote ninafikiria hali mbaya ya Palestina na Israel: Ninahimiza kuachiliwa kwa mateka na kuingia kwa misaada ya kibinadamu huko Gaza. Ninaendelea kusali kwa ajili ya wale wanaoteseka na kutumaini njia za amani, katika Mashariki ya Kati, katika Ukraine inayoteswa na katika maeneo mengine yaliyojeruhiwa na vita.

Waamini wamealikwa kuungana na Papa kusali 27 Oktoba

Hata hivyo kutokana na muktadha huo, Baba Mtakatifu Francisko tena amewakumbusha siku ya kusali na kwa hiyo amesema:  Ninawakumbusha wote kwamba kesho kutwa, Ijumaa, tarehe 27 Oktoba, tutapata siku ya kufunga, kuomba na kutubu; saa kumi na mbili jioni, Katika Kanisa la Mtakatifu Petro  tutakusanyika kusali ili kusihi amani duniani.”

Tusiruhusu mawingu ya mgogoro

Na kwa upande wa salamu kwa mahujaji wa kireno, Papa Francisko pia alikuwa amekabidhi kwa Mama Maria dharura ya amani: “Tusiruhusu mawingu ya migogoro yasifiche jua la matumaini. Hakika, tunamkabidhi Mama Yetu uharaka wa amani ili tamaduni zote zifungue msukumo wa maelewano ya Roho Mtakatifu.”

Wito wa Papa kwa misaada ipatikane Gaza
25 October 2023, 13:13