Tafuta

Papa,Sala ya kuombea amani:Geuza macho yako ya huruma kwa familia ya kibinadamu

Wewe, Malkia wa Amani,unateseka pamoja nasi na kwa ajili yetu,ukiona watoto wako wengi sana wakijaribiwa na migogoro,wakihuzunishwa na vita vinavyosambaratisha ulimwengu.Katika saa hii ya giza tunajizamisha katika macho yako angavu na kutegemea moyo wako,nyeti kwa shida zetu:Ni sala Ya Papa Francisko kwa ajili ya Amani Oktoba 27 katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko Ijumaa jioni tarehe 27 Oktoba 2023 ameongoza sala ya Rozari, ambayo ilifuatiwa na kuabudu mara baada ya sala kwa Bikira Maria katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, kwa kuudhuriwa na Mababa na Mama, Walei waamini wa Sinodi, na waamini kutoka  Jimbo la Roma na mahujaji kutoka pande za dunia. Ilikuwa ni wakati mzuri wa sala ya kina na matumaini kwa Mama Maria na Bwana wetu Yesu Kristo katika Umbo la Ekaristi wakati wa Kuambudu. Katika sala aliyomwelekeza Mama Maria, Baba Mtakatifu mara baada ya Rozari takatifu amesali hivi: Maria, tuangalie! Tuko hapa mbele yako. Wewe ni Mama, unajua shida zetu na majeraha yetu.Wewe, Malkia wa Amani, unateseka pamoja nasi na kwa ajili yetu, ukiona watoto wako wengi sana wakijaribiwa na migogoro, wakihuzunishwa na vita vinavyosambaratisha ulimwengu. Ni saa ya giza. Mama ni wakati wa giza, tunajizamisha katika macho yako angavu na kutegemea moyo wako, nyeti kwa shida zetu. Hakuwa huru kutokana na mahangaiko na woga: ni wasiwasi kiasi gani wakati hapakuwa na nafasi ya Yesu katika nyumba hiyo, ni hofu kiasi gani ulipokimbilia Misri kwa haraka kwa sababu Herode alitaka kumuua, ni uchungu kiasi gani ulipompoteza katika hekalu! Lakini katika majaribu mlikuwa shupavu na jasiri: mlimwamini Mungu na kuitikia wasiwasi kwa uangalifu, kwa hofu kwa upendo, kwa uchungu na sadaka.

SALA KWA AJILI YA AMANO
SALA KWA AJILI YA AMANO

Hukusitasita, lakini katika nyakati za kuamua ulichukua hatua: ulikwenda haraka kwa Elizabeti, kwenye harusi ya Kana ulipata muujiza wa kwanza kutoka kwa Yesu, katika Karamu Kuu uliwaweka wanafunzi  kubaki na umoja. Na pale Kalvari upanga ulipoichoma roho yako, wewe, mwanamke mnyenyekevu na hodari, uliufuma usiku wa maumivu kwa tumaini la Pasaka. Sasa, Mama, ongoza kwa mara nyingine tena kwa ajili yetu, katika nyakati hizi zilizoharibiwa na migogoro na kuharibiwa na silaha. Geuza macho yako ya huruma kwa familia ya kibinadamu, ambayo imepoteza njia ya amani, ambayo imependelea Kaini kuliko Abeli ​​na, ikipoteza hisia ya udugu, haiwezi kupata hali ya nyumbani tena. Uombee ulimwengu wetu katika hatari na machafuko. Tufundishe kukaribisha na kutunza maisha - kila maisha ya mwanadamu! - na kukataa wazimu wa vita, ambayo hupanda kifo na kufuta siku zijazo.

SALA YA ROZARI KWA AJILI YA AMANI
SALA YA ROZARI KWA AJILI YA AMANI

Maria, umekuja kukutana nasi mara nyingi, ukiomba maombi na toba. Sisi, hata hivyo, tukichukuliwa na mahitaji yetu na kukengeushwa na mambo mengi ya kidunia, tumekuwa viziwi kwa mialiko yako. Lakini wewe unayetupenda usituchoke. Utushike mkono, utuongoze kwenye uongofu, tumtangulize Mungu. Utusaidie kulinda umoja katika Kanisa na kuwa mafundi wa ushirika ulimwenguni. Utukumbushe umuhimu wa jukumu letu, utufanye tujisikie kuwajibika kwa amani, wito wa kuomba na kuabudu, kuombea na kufanya marekebisho kwa ajili ya jamii nzima ya binadamu.

Hatuwezi kufanya hivyo peke yetu, bila Mwanao hatuwezi kufanya lolote. Lakini unaturudisha kwa Yesu ambaye ndiye amani yetu. Kwa hivyo, Mama wa Mungu na wetu, tunakuja kwako, tunatafuta kimbilio katika Moyo wako safi. Tunaomba hruma, Mama wa rhuruma; amani, Malkia wa amani! Tikisa roho za walionaswa na chuki, waongoze wale wanaochochea na kuzua migogoro. Kausha machozi ya watoto, wasaidie walio peke yao na wazee, wasaidie waliojeruhiwa na wagonjwa, linda wale ambao wamelazimika kuondoka katika nchi yao na wapendwa wao wapendwa, fariji waliovunjika moyo, uwaamshe tena tumaini. Tunakukabidhi na kuyaweka wakfu maisha yetu, kila nyuzi ya utu wetu, kile tulicho nacho na tulicho, milele. Tunaliweka wakfu Kanisa kwako ili kwamba, kwa kuushuhudia ulimwengu kuhusu upendo wa Yesu, liwe ishara ya maelewano na chombo cha amani. Tunaweka ulimwengu wetu wakfu kwako, hasa nchi na maeneo yaliyo kwenye vita.

ROZARI KWA AJILI YA AMANO
ROZARI KWA AJILI YA AMANO

Wewe, alfajiri ya wokovu, fungua mihali ya mwanga  katika usiku wa migogoro. Wewe, makao ya Roho Mtakatifu, vuvia njia za amani kwa viongozi wa mataifa. Wewe, Mama wa mataifa yote, patanisha watoto wako, walioshawishiwa na uovu, wamepofushwa na nguvu na chuki. Wewe, ambaye ni karibu na kila mmoja, fupisha umbali wetu. Wewe, ambaye una huruma kwa kila mtu, utufundishe kutunza wengine. Wewe unayedhihirisha huruma ya Bwana, tufanye kuwa  mashahidi wa faraja yake. Wewe, Malkia wa Amani, mimina maelewano ya Mungu ndani ya mioyo yetu.Amina.

Sala kwa ajili ya amani
Sala kwa ajili ya amani

Baada ya sala hiyo ilifuatia Ibada ya kuabudu Ekaristi Takatifu.

sala ya Papa kwa ajili ya amani
27 October 2023, 19:30