Mtumishi wa Mungu Maria wa Yesu wa Ágreda, alizaliwa huko Agreda, katika Jimbo la “Soria, huko Old Castile” kwenye mpaka na Aragon, tarehe 2 Aprili 1602. Mtumishi wa Mungu Maria wa Yesu wa Ágreda, alizaliwa huko Agreda, katika Jimbo la “Soria, huko Old Castile” kwenye mpaka na Aragon, tarehe 2 Aprili 1602.   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Mtumishi wa Mungu Maria wa Yesu wa Agreda: Neno, Mahusiano, Utume na Umisionari

Baba Mtakatifu Francisko katika hotuba yake kwa washiriki wa Kongamano hili kuhusu Mtumishi wa Mungu Maria wa Yesu wa Ágreda, amekazia mambo yafuatayo: Mwanampekee wa pekee aliyependa Maandiko Matakatifu, akajikita katika ukimya, moyo wa kusikiliza Neno la Mungu; Pili alijenga na kukuza uhusiano na mafungamano na Mwenyezi Mungu kutokana na Maandiko Matakatifu na Tatu ni Utume, ari na moyo wa kimisionari, toba na wongofu wa walimwengu.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Mtumishi wa Mungu Maria wa Yesu wa Ágreda, alizaliwa huko Agreda, katika Jimbo la “Soria, huko Old Castile” kwenye mpaka na Aragon, tarehe 2 Aprili 1602. Katika familia yake, wote walijiweka wakfu kwa Mungu katika Mashirika mbalimbali ya kitawa.  Mtumishi wa Mungu Maria wa Yesu wa Ágreda, aliweka nadhiri zake kunako mwaka 1620 na aliishimaisha yake yote katika Monasteri ya Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili na alishikilia nafasi kama Mama mkuu wa Shirika kwa muda wa miaka thelathini na mitano. Ni mtawa aliyebahatika kupata maono mbalimbali kati ya Mwaka 1620 hadi mwaka 1631. Taasisi ya Kipapa ya Bikira Maria Kimataifa kuanzia tarehe 16 hadi tarehe 18 Novemba 2023 imeandaa Kongamano la Kimataifa linalonogeshwa na kauli mbiu “Mtawa aliyependa Maandiko Matakatifu, Msomi wa Bikira Maria na Mwinjilishaji wa Amerika: “Mwanamke aliyeandika Historia.” Wajumbe wa Kongamano hili, Alhamisi tarehe 16 Novemba 2023 wamekutana na kuzungumza na Baba Mtakatifu Francisko mjini Vatican. Baba Mtakatifu katika hotuba yake kwa washiriki wa Kongamano hili kuhusu Mtumishi wa Mungu Maria wa Yesu wa Ágreda, amekazia mambo yafuatayo: Mwanampekee wa pekee aliyependa Maandiko Matakatifu, akajikita katika ukimya, moyo wa kusikiliza Neno la Mungu; Pili alijenga na kukuza uhusiano na mafungamano na Mwenyezi Mungu kutokana na Maandiko Matakatifu na Tatu ni Utume, ari na moyo wa kimisionari.

Mtumishi wa Mungu Maria wa Yesu wa Agreda: Neno, Mahusiano na Utume
Mtumishi wa Mungu Maria wa Yesu wa Agreda: Neno, Mahusiano na Utume

Baba Mtakatifu Francisko ameipongeza Taasisi ya Kipapa ya Bikira Maria Kimataifa kwa sera na mikakati yake inayojikita katika tafiti makini juu ya Bikira Maria na tafakari zake. Mtumishi wa Mungu Maria wa Yesu wa Ágreda, alikuwa ni Mwanamke wa shoka aliyependa sana kusoma Maandiko Matakatifu, akajenga na kukuza ukimya na tabia ya kusikiliza kwa makini, kama wito maalum wa wanawake. Ni mwanamke aliyepata mang’amuzi ya Maandiko Matakatifu na katika sala, wakanywa na kushibishwa kutoka katika chemchemi iliyo hai na hivyo kujizamisha katika upendo kwa Maandiko Matakatifu. Wakabahatika kumwona Kristo Yesu anayezungumza nao kupitia Neno la Mungu, mwaliko kwa kufuata na kujifunza kutoka kwa Bikira Maria: “Aliyaweka hayo yote moyoni mwake.” Lk 2:51.

Washiriki wa Kongamano la Mtumishi wa Mungu Maria wa Yesu Agreda
Washiriki wa Kongamano la Mtumishi wa Mungu Maria wa Yesu Agreda

Jambo la pili ni kwamba, alijenga na kukuza uhusiano na mafungamano na Mwenyezi Mungu kutokana na Maandiko Matakatifu kiasi cha kumkirimia furaha iliyokita mizizi kutoka katika sakafu ya maisha yake na hivyo kushinda kishawishi cha ubinafsi na uchoyo unaotaka kutawala furaha hii. Huu ni mwaliko wa kujenga utamaduni wa kujinyenyekeza mbele ya Mungu kwa kumpokea na kumkaribisha Mungu Mwenyezi ili afanye makazi katika maisha ya waja wake. Hivi ndivyo Bikira Maria alivyomkaribisha Mtoto Yesu, tumboni mwake na hivyo kuwa ni Tabernakulo ya kwanza ya Neno la Mungu. Hapa waamini wajifunze kwa kupitia njia ya kujinyima, uaminifu na furaha ya kweli ili kuishi kadiri ya mpango wa Mwenyezi Mungu. Waamini wajifunze utamaduni wa kukaa kimya katika ulimwengu huu ambao umesheheni migogoro mingi, ni mwaliko wa kujenga ukimya wa ndani ili kudumisha mawasiliano na Mwenyezi Mungu.

Neno la Mungu, Mafungamano na Utume ni muhimu sana
Neno la Mungu, Mafungamano na Utume ni muhimu sana

Tatu ni utume, ari na moyo wa kimisionari, ushuhuda unaotolewa na Mtumishi wa Mungu Maria wa Yesu wa Ágreda. Hapa Mama Kanisa anamkumbuka kwa heshima kuu Mtakatifu Theresa wa Mtoto Yesu. Itakumbukwa kwamba Mtakatifu Rosa wa Lima ndiye mwamini wa kwanza kutangazwa na Mama Kanisa kuwa ni Mtakatifu. Mtumishi wa Mungu Maria wa Yesu wa Ágreda alijikita katika maisha ya sala kwa ajili ya kuombea wokovu kwa walimwengu. Bikira Maria katika Arusi ya Kana ya Galilaya aliingilia kati kuokoa jahazi la wanandoa lililokuwa likienda mrama kwa kutindikiwa divai, lakini Bikira Matia akaingilia kati na kuokoa jahazi. Waamini wanaweza kutambua mahali inapotoka divai mpya kwa sababu kuna watu wanawategemeza kwa njia ya sala. Huu ni mwaliko wa kutenda kadiri ya mapenzi ya Mungu.

Kongamano
16 November 2023, 15:12