Papa akutana na Pato:Nilisali sana kwa ajili ya mke wako na binti yako

Alasiri 17 Novemba katika Nyumba ya Mtakatifu Marta Mjini Vatican,Papa alikutana na Mbengue Nyimbilo Crepin,anayejulikana kwa wote Pato miaka 30,mhamiaji wa Cameroon,ambaye mwishoni mwa Julai alipoteza mke wake Matyla na binti Marie wa wa miaka 6,ambaye alifariki kwa njaa,joto na kiu katika jangwa kati ya Tunisia na Libia.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, alasiri tarehe 17 Novemba 2023 akiwa katika nyumba ya Mtakatifu Marta mjini Vatican alikutana na Mbengue Nyimbilo Crepin, anayejulikana kwa wote kama Pato, mwenye umri wa miaka 30, mhamiaji wa Cameroon, ambaye mwishoni mwezi Julai  2023 alipoteza mke wake Matyla na binti yake mdogo Marie, mwenye umri wa miaka 6, aliyefariki kwa njaa, joto na kiu katika jangwa kati ya Tunisia na Libya. Kijana huyo aliyelia mara baada ya kusikia maneno ya Papa, alisindikizwa na Padre Mattia Ferrari, anayetoa huduma katika Harakati ya Mediterranea Saving Humans,  yaani ya kuhudumia wakimbizi na Kardinali Michael Czerny, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu.

Kundi zima la wahamiaji walioktana na Papa
Kundi zima la wahamiaji walioktana na Papa

Baba Mtakatifu akitoa maeno yake bila kuandika alisema vijana hawa ni wazuri. Huyu ndiye Kristo, anayeteseka, alirudia- Kristo anayeteseka, Kristo wa sasa. Kristo wetu yuko karibu nasi, hatutakiwi kwenda kumtafuta kwa mbali, yuko katika kila mtu anayeteseka na dhuluma hii na anayekufa: wengi wanakufa ... Inaruhusiwa kumtazama mtu katika wakati mmoja tu kutoka juu hadi chini ambao ni  wakati unapopiga magoti ili kumsaidia kuinuka. Njia nyingine za kumtazama mtu kuanzia juu hadi chini sio za mwanadamu.

Kijana Pato
Kijana Pato

Mara baada ya kuwasalimia na kuwasikiliza maneno yao Papa Francisko aliwashukuru waliokuwapo kwa jitihada zao na kwamba Ni vizuri zaidi kukaa nyumbani, usifanye chochote, kuishi kwa kujifurahisha, kuishi kwa masilahi ya kibinafsi. Lakini anayetoka kuhudumia anahisi wengi hawamfuati, kiukweli anahisi haeleweki, haelewi. Msiogope: Endeleeni mbele. Aliwaambia,  hayo akiwakumbusha juu ya upendeleo wa kuzaliwa mahali ambapo unaweza kusoma na kufanya kazi: "Upendeleo ni deni", alisema, "mnachofanya sio nyongeza, ni jukumu". Hatimaye, kabla ya kuondoka, Baba Mtakatifu aliwaombea wale waliokuwapo, akimwomba Bwana awaangalie wale “wanaofanya kazi kwa ajili ya wengine,” juu ya watu ambao hawakuweza kufika, juu ya wale walio katika kambi za kizuizini na “juu ya wengi, wengi ambao kuteseka."

Baraka kwa za Papa
Baraka kwa za Papa

Kwa  hiyo Pato alipoteza mke wake na binti  yake mwenye umri wa miaka 6 mwezi Julai 2023, baada ya kuzuiwa na kurejeshwa kwenye jangwa kati ya Libya na Tunisia na mamlaka ya Tunisia. Katika hali ya hisia kwa historia yake, Papa alisikiliza maneno ya shukrani kwa mkutano huo na historia chungu za maelfu ya watu wanaoteseka wakijaribu kufika Ulaya. David, kutoka Sudan Kusini, akifanya kazi pamoja na wafungwa katika kambi za kizuizini huko Afrika Kaskazini, alimshukuru Papa Francisko  kwa kutia moyo na kuingilia kati kwa ajili ya wahamiaji: "Hutupatii ndoto tu, unatukaribisha".

18 November 2023, 14:06