Papa Francisko katika Sala ya Malaika wa Bwana Papa Francisko katika Sala ya Malaika wa Bwana  (ANSA)

Papa atoa wito kwa ajili ya Myanmar,Palestina,Israel na Ukraine

Baba Mtakatifu mara baada ya tafakari na sala ya Malaika wa Bwana ametoa Wito kwa ajili ya Mashariki ya Kati,Ukraine na Myanmar.Amekumbusha Siku ya VII ya Maskini Duniani inayoadhimishwa Novemba 19 na Siku ya Wavuvi Duniani itakayofanyika tarehe 21 Novemba.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Baba Mtakatififu Francisko mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana Dominika tarehe 19 Novemba 2023  akiwageukia Waamini na mahujaji waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, amewafahamisha juu ya Jumamosi tarehe 18 Novemba 2023  huko Seville, Manuel Gonzales-Serna, Padre wa jimbo na Mapadre kumi na tisa wenzake na walei, waliouawa mwaka wa 1936 katika mazingira ya mateso ya kidini ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Hispania, walitangazwa kuwa wenyeheri. Wafia imani hawa walimshuhudia Kristo hadi mwisho. Mfano wao na uwafariji Wakristo wengi ambao katika nyakati zetu wanabaguliwa kwa ajili ya imani yao.  Kwa njia hiyo ameomba kuwapongezwa hao wenyeheri wapya…..

Siku ya Maskini duniani 19 Novemba
Siku ya Maskini duniani 19 Novemba

Baba Mtakatifu amendelea kusema kuwa anawaweka kwa upya ukaribu wangu kwa watu wapendwa wa Myanmar, ambao kwa bahati mbaya wanaendelea kuteseka kutokana na vurugu na unyanyasaji. Ninaomba kwamba wasivunjike moyo na kutumaini msaada wa Bwana kila wakati. Papa pia amewageukia kaka dada wote waliokusanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro kwamba  tuendelee kuiombea Ukraine inayoteswa - aliona bendera hapo -  na kwa watu wa Palestina na Israel. Amani inawezekana. Inachukua mapenzi mema. Amani inawezekana. Tusijitoe kwenye vita! Na tusisahau kwamba vita daima, daima, daima ni kushindwa. Watengenezaji wa silaha pekee ndiyo wanaofaidika.

Siku ya Maskini duniani.

Baba Mtakatifu amesema kuwa, Leo tunaadhimisha Siku ya VII ya Maskini Duniani, ambayo mwaka huu inaongozwa na kaulimbiu, "Usiwaondolee macho maskini" (Tb, 4,7). Ninawashukuru wale wote wa majimbo na Parokia ambao wamehimiza mipango ya mshikamano na watu na familia zinazojitahidi kusonga mbele. Na siku hii pia tunawakumbuka wahanga wote wa barabara: tuwaombee, kwa ajili ya familia zao na tujitoe katika kuzuia ajali. Baba Mtakatifu amependa kutaja Siku ya Uvuvi Duniani, ambayo itaadhimisha  tarehe 21 Novemba 2023. Amewasalimu wote kwa upendo, mahujaji kutoka Italia na sehemu nyingine za ulimwengu.

Papa hakusahau kuwaombea watu wa Ukraine
Papa hakusahau kuwaombea watu wa Ukraine

Amewasalimu waamini wa Madrid, Ibiza na Warsaw, na washiriki wa Baraza la Umoja wa Walimu Wakatoliki Ulimwenguni. Amewasalimu vikundi kutoka Aprilia, Mtakatifu Ferdinando di Puglia na Mtakatifu Antimo; Chama cha FIDAS cha Orta Nova, na washiriki katika "Siku za Kushiriki" za Harakari ya  Kitume ya Vipofu. Salamu maalum kwa jumuiya ya Ecuador ya Roma, ambayo inaadhimisha siku kuu ya Bikira wa Quinche. Na salamu kwa watoto wa Mama wa Moyo Safi. Kwa kuhitimisha amewatakia Dominika Njema na tafadhali wasisahau kumuombea. Amewatakia mlo na mchama mwema.

Papa baada ya sala ametoa wito,Myanmar,Israel,Palestina na Ukraine
19 November 2023, 13:33