Tafuta

Hospitali ya Kipapa ya Bambino Gesu ilikuwa tayari kumpokea mtoto  wa ugonjwa nadra Indi Gregory kutoka Uingereza. Hospitali ya Kipapa ya Bambino Gesu ilikuwa tayari kumpokea mtoto wa ugonjwa nadra Indi Gregory kutoka Uingereza.  (Vatican Media)

Papa Francisko anawaombea Indi Gregory na wazazi wake

Mawazo pa Papa amegeuki mtoto wa Kiingereza anayeugua ugonjwa wa nadra wa mitochondrial na ambaye atatengwa na msaada wa maisha unaomuweka hai,baada ya majaji wa kiingereza kukataa kumhamisha kuja Italia licha ya ukweli kwamba Hospitali ya Bambino Gesù ilikuwa imejitolea kumkaribisha.

Vatican news

Baba Mtakatifu Francisko anaungana  na familia ya mtoto Indi Gregory, ya baba na mama yake  na anawaombea na kwa ajili yake na kuelekeza mawazo yake kwa watoto wote ambao katika saa hizi hizi duniani kote wanaishi kwa uchungu au kuhatarisha maisha yao kwa sababu ya ugonjwa na vita. Hivi ndivyo Msemaji wa Vyombo vya Habari, Vatican Dk.  Matteo Bruni, alivyoripoti. Indi Gregory ni mtoto wa kike  wa miezi minane wa Kiingereza anayesumbuliwa na aina ya ugonjwa nadra wa (mitochondrial) unaozingatiwa na madaktari kuwa hauwezi kuponywa, na ambaye hivi karibuni Mahakama Kuu ya London nchini Uingereza imekataa uwezekano wa uhamisho kuja Italia, baada ya kupata uraia,  ili kuweza kupata matibabu, hasa katika Hospitali ya Watoto ya Bambino Gesù ambayo ni Hospitali ya Kipapa  iliyopatikana, kufuatia matakwa yaliyotolewa na wazazi wa mtoto huyo.

Baada ya majaji wa Kiingereza kukataa kukubali rufaa iliyowasilishwa na mama na babake, mtoto huyo mdogo atanyimwa usaidizi wa maisha unaomuweka kuwa hai katika Kituo cha Matibabu cha Malkia huko Nottingham na kuhamishiwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi.

Maombi ya Papa Francisko

Baba Mtakatifu amekuwa akiingilia kati mara kadhaa huko nyuma katika visa kama hivyo. Mnamo tarehe 15 Aprili 2018, katika Sala ya Malkia wa Mbingu, aliwakabidhi Vincent Lambert na Alfie Evans mdogo kwa sala za kila mtu na watu wengine wanaoishi "katika hali ya ugonjwa mbaya, wakisaidiwa kimatibabu kwa mahitaji ya msingi. Hizi ni hali dhaifu - alisema - chungu sana na ngumu. Tunaomba kwamba kila mgonjwa daima aheshimiwe kwa utu wake na kutunzwa kwa njia inayolingana na hali yake, kwa mchango wa pamoja wa wanafamilia, madaktari na wahudumu wengine wa afya, kwa heshima kubwa kwa maisha."

"Ningependa kurudia na kuthibitisha kwa nguvu - Papa alisema tena mwishoni mwa katekesi yake  tarehe 18 Aprili 2018,  kwamba Bwana pekee wa maisha, tangu mwanzo hadi mwisho wa asili, ni Mungu! Na jukumu letu, ni kufanya kila kitu kulinda maisha. Hebu tufikirie kwa ukimya na kuomba ili maisha ya watu wote na hasa ya ndugu zetu hawa wawili yaheshimiwe."

Mnamo mwaka wa 2017, Papa Francisko alifuatilia akisema "kwa upendo na hisia ya Historia ya Charlie Gard" huku  akielezea "ukaribu wake na wazazi wake", kama ilivyokuwa imeripitiwa na  Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican kwamba,  Papa anawaombea, akitumaini kwamba hamu yao ya kukumsindikiza na kumtunza mtoto wao mpaka mwisho. Naye Askofu Mkuu Vincenzo Paglia, rais wa Chuo cha Kipapa cha Maisha, akirejea  suala hilo la Charlie Gard, alikuwa amesema: "Mungu hakati mipira yoyote".

Mawazo ya Papa kwa Kesi ya Indi Gregory Mtoto wa Ugonjwa nadra
11 November 2023, 14:12