2023.11.18 Papa amekutana na washiriki wa Mkutano ulioandaliwa na CEI juu ya Ulinzi wa Watoto na watu waathirika wa nyanyaso. 2023.11.18 Papa amekutana na washiriki wa Mkutano ulioandaliwa na CEI juu ya Ulinzi wa Watoto na watu waathirika wa nyanyaso.  (Vatican Media)

Papa Francisko:Nyanyaso ni majeraha ambayo lazima yatibiwe

Papa amekutana na washiriki wa Mkutano ulioandaliwa na Baraza la Maaskofu Italia juu ya ulinzi wa watoto na watu walio katika mazingira magumu na kupokea matokeo ya uchunguzi wa shughuli za Huduma na Vituo vya Usikilizaji vya majimbo.Katika hotuba yake amesisitizia mafunzo na usikivu ambao uunda utamaduni wa kuzuia.

Na Angella Rwezaula, Vatican
Jumamosi tarehe 18 Novemba 2023, Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Washiriki wa Mkutano wa Kwanza ulioandaliwa na Baraza la Maaskofu Italia juu ya Ulinzi wa Watoto na Watu waathirika nchini Italia. Akianza hotuba yake,ametoa salamu zake kwa Kardinali Matteo Zuppi, Rais wa Baraza la Maaskofu Italia na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Bologna na pia washiriki wote. Papa amesema Mkutano huo unawakilisha kujitolea kwa Kanisa nchini Italia katika kukuza utamaduni wa ulinzi kwa watoto wadogo na walio hatarini zaidi. Na wamekutana naye wakiwa wanahitimisha mkurano huo wa kwanza kitaifa katika siku ambayo  kwa mwaka wa tatu,  mfululizo jumuiya zote za kikanisa nchini Italia zinahusika katika sala, katika ombi la msamaha na katika kuongeza ufahamu kuhusu ukweli huu wa uchungu. Hili ni muhimu kuhusika kwa watu wote wa Mungu. Na pia amewapongeza kwa sababu waliitikia mwaliko  wake upesi na ripoti kwenye mtandao wa eneo lako. 

Baba Mtakatifu Francisko amesisisitiza kuwa katika tukio hilo wamechagua kauli mbiu ya Uzuri Uliojeruhiwa. “Nitaponya jeraha lako na kukuponya majeraha yako”(Yer 30:17). Katika utumishi wao, waongozwe na hakika hii iliyotangazwa na nabii Yeremia: Bwana yuko tayari kuponya kila jeraha, hata lililo ndani kabisa. Ili hili litokee, hata hivyo, uongofu wetu na utambuzi wa mapungufu yetu ni muhimu. Hatuwezi kuacha katika hatua yetu ya kuwalinda watoto na walio hatarini na, wakati huo huo, kupambana na aina yoyote ya unyanyasaji, iwe ya kingono, ya mamlaka au ya dhamiri. Kuhusiana na hilo Papa amependekeza vitenzi vitatu ambavyo vinaweza kutoka  katika mwongozo wa kila mpango: Kulinda, Kusikiliza na Kutunza. Awali ya yote, kulinda: kushiriki kikamilifu katika maumivu ya watu waliojeruhiwa na kuhakikisha kwamba jumuiya nzima inawajibika kwa ulinzi wa watoto wadogo na wale walio katika mazingira magumu zaidi. Jumuiya nzima ya Kikristo, katika utajiri wa vipengele na ujuzi wake, lazima ihusishwe, kwa sababu hatua ya ulinzi ni sehemu muhimu ya utume wa Kanisa katika kujenga Ufalme wa Mungu. Kulinda kunamaanisha kuelekeza moyo wa mtu, kutazama na kufanya kazi kwa usahihi kwa upendeleo wa wadogo na wasio na kinga. Ni njia inayohitaji kufanywa upya ndani na kwa jamii, katika haki na ukweli.

Papa na walinzi wa Watoto
Papa na walinzi wa Watoto

Wale wanaolinda, wale wanaoilinda mioyo yao, wanajua kwamba "hakuna ukimya au uficho unaoweza kukubaliwa juu ya suala la unyanyasaji" - hili si jambo la kujadiliwa -; na pia anajua kwamba ni muhimu "kufuatilia uthibitisho wa ukweli na uimarishaji upya wa haki ndani ya jumuiya ya kikanisa, hata katika kesi zile ambazo tabia fulani hazizingatiwi uhalifu na sheria za serikali, lakini zinachukuliwa kuwa uhalifu kwa kisheria”(taz. CEI-CISM, Miongozo ya ulinzi wa watoto na watu walio katika mazingira magumu). Kulinda pia kunamaanisha kuzuia matukio ya madhara, na hii inawezekana tu kupitia shughuli za mafunzo ya mara kwa mara, yenye lengo la kueneza unyeti na makini kwa ulinzi wa tete zaidi. "Na hii pia ni muhimu nje ya ulimwengu wetu wa kikanisa.  Baba Mtakatifu amesema wafikirie  kwamba, kulingana na takwimu za kimataifa, kati ya asilimia 42 na 46 ya unyanyasaji hutokea katika familia au katika ujirani. Kuyamaza, kila kitu kimefunikwa: wajomba, babu, kaka, kila kitu. Baadaye ni katika ulimwengu wa michezo, kisha shuleni, na kadhalika.

Kipengele cha pili ni kusikiliza. Baba Mtakatifu amejikita kueleza kuwa ili kuilinda, unahitaji kujua jinsi ya kusikiliza, kuweka kando kila aina ya kimbelembele na maslahi binafsi. Kusikiliza ni mwendo wa moyo na pia ni chaguo la msingi kwa kuwaweka wale ambao wameteseka au wanaoteseka na wale ambao ni dhaifu na walio hatarini katikati mwa matendo yetu yote. Hebu tumfikirie Yesu anayewakaribisha watoto na “watoto” wote (rej. Mt 19:14). Kuwasikiliza waathiriwa ni hatua muhimu ya kukuza utamaduni wa kuzuia, unaoonekana katika mafunzo ya jamii nzima, katika utekelezaji wa taratibu na utendaji mzuri, kwa uangalifu na uwazi wa hatua zinazojenga na kuhuisha uaminifu. Kusikiliza tu machungu ya watu waliopatwa na uhalifu huu mbaya hufungua mshikamano na kutusukuma kufanya kila linalowezekana ili unyanyasaji huo haurudiwi tena. Hii ndiyo njia ya pekee ya kushiriki kwa kweli kile kilichotokea katika maisha ya mwathirika, ili kuhisi changamoto kwa upyaji wa kibinafsi na wa jumuiya. Tumeitwa kwa mwitikio wa kimaadili, kukuza na kutoa ushuhuda wa ukaribu kwa wale ambao wameumizwa na unyanyasaji. Kujua jinsi ya kusikiliza ni kutunza waathiriwa. "Kutengeneza vitambaa vya historia vilivyochanika ni tendo la ukombozi, ni tendo la Mtumishi aliyeteseka, ambaye hakuepuka maumivu, lakini alichukua kila hatia juu yake mwenyewe (rej. Is 53:1-14). Hii ndiyo njia ya fidia na ukombozi: njia ya msalaba wa Kristo."

Washiriki wa Mkutano wa Ulinzi wa Watoto na watu waathirika
Washiriki wa Mkutano wa Ulinzi wa Watoto na watu waathirika

Ni kwa kufuata tu njia ya kujali na kusikiliza inawezekana kuponya. Katika wakati huu, utamaduni wa uharibifu umeenea, kinyume na Injili inavyosema; jamii zetu lazima ziwe kichocheo cha afya kwa jamii, katika uwezo wao wa kuchukua makosa ya zamani na kufungua njia mpya. "Tiba" ya majeraha pia ni kazi ya haki. Hasa kwa sababu hii ni muhimu kuwashtaki wale wanaofanya uhalifu huo, hata zaidi ikiwa katika mazingira ya kikanisa. Na wao wenyewe wana wajibu wa kimaadili wa uongofu wa kina wa kibinafsi, ambao unaongoza kwenye utambuzi wa uongofu  wao wenyewe wa kitaaluma, kwa kuanza tena maisha ya kiroho na kwa ombi la unyenyekevu la msamaha kutoka kwa waathirika kwa matendo yao. Kwa hiyo natoa shukrani zangu kwa hali halisi mnayowakilisha, huduma za ulinzi wa watoto na vituo vya kusikiliza, zilizoenea kote nchini kama sehemu za kugeukia ili kupata sikio la kusikiliza. Endelea kufanya kila juhudi. "Na pia chunga jambo baya sana linalotokea, ambalo ni filamu za picha mbaya  ambazo watoto hutumia. Hii hutokea, kwa hakika, inaweza kufikiwa na mtu yeyote anayelipa, kwenye simu yake ya mkononi. Filamu hizi zinatengenezwa wapi? Nani anawajibika? Katika nchi gani? Tafadhali, fanyieni kazi  kwa sababu hili ni pambano ambalo tunapaswa kupambana kwa sababu jambo baya zaidi ni kuenea katika simu za mikononi."

Papa na Kardinali Zuppi Rais wa CEI
Papa na Kardinali Zuppi Rais wa CEI

Papa Francisko amewatia moyo waendelee kufanya kila juhudi ili wale wote ambao wamejeruhiwa na janga la unyanyasaji wajisikie huru kurejea kwenye Vituo vya Kusikiliza kwa kujiamini, wakipata ukaribisho huo na usaidizi unaoweza kutuliza majeraha yao na kufanya upya imani iliyosalitiwa. Kujali kunamaanisha kushiriki shauku na ujuzi wa kikanisa na kujitolea kutoa mafunzo kwa wachungaji wengi iwezekanavyo. Kwa njia hii, mabadiliko ya kweli ya kiutamaduni yanakuzwa ambayo yanawaweka walio wadogo na walio hatarini zaidi katikati katika Kanisa na katika jamii. Kitendo chak hiki cha kikanisa kinaweza kuhimiza umakini zaidi katika jamii yote ya Italia juu ya tauni hii ambayo kwa bahati mbaya inahusisha wengi sana, watoto na watu wazima. Katika mkutadha wa Matokeo ya uchunguzi wa shughuli za Huduma na Vituo waliyomkabidhi siku hiyo, Papa amesema yanaakisi mambo mazuri sana wanayojua kufanya katika eneo hilo na kuwafanya wawe karibu na wale ambao wamejeruhiwa na majeraha.

Baba Mtakatifu amewapongeza kwa kuwa amesema wanachofanya ni cha thamani kwa waathiriwa na kwa jumuiya nzima ya kikanisa. Ushahidi wa kujitolea mara kwa mara na wa pamoja unajitokeza kutoka katika kurasa hizo. Hii ndiyo njia ya kuunda uaminifu, uaminifu unaoongoza kwenye upyaji wa kweli. Hatimaye Papa amependa kuwashukuru kwa msaada wanaoutoa kwa Mabaraza mengine ya Maaskofu; pamoja na kuunga mkono mipango ya Tume ya Kipapa ya Ulinzi wa Watoto Wadogo kuelekea nchi hizo, hasa nchi zinazoendelea, ambazo zina rasilimali adimu kwa ajili ya kuzuia na kutekeleza sera za ulinzi. Ameomba waendelee mbele, na yeye yupo pamoja nao katika kazi yao na kuwabariki kutoka ndani ya moyo wake. Anawaombea kwa sababu kazi yao si rahisi, na wao tafadhai wasisahau kumuombea kwa sababu kazi yake amethibitisha pia kuwa si rahisi.

18 November 2023, 12:19