Papa:Wakatoliki wahamasike kwa uwazi na azma katika nyanja ya kijamii
Vatican News
Muktadha wa wasiwasi wa ukosefu wa utulivu wa kimataifa unaonesha haja ya uwiano wa kijamii, udugu na upatanisho kati ya makundi na jumuiya. Hayo ndiyo tunayosoma katika ujumbe kutoka kwa Baba Mtakatifu Francisko, uliotiwa saini na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican uliotumwa kwa washiriki wa mkutano wa Juma za Kijamii Ufaransa, unaoendelea mjini Lyon hadi tafungamani, kulingana na mafundisho ya Papa Francis, ambayo wakati huo huo yanashughulikia migogoro ya kijamii na kimazingira na yanatuhimiza kutotenganisha kile ambacho kina uhusiano wa karibu, ujumbe huo unasomeka.
Kulinda kazi ya uumbaji ni kazi ya kila mtu
Katika ujumbe huo unanukuu vifungu kutoka katika Waraka wa Laudate Deum, ambapo Papa anakumbusha kwamba "kujitolea kwa kibinafsi kwa ulinzi wa uumbaji" peke yake hakutoshi "kushughulikia mgogoro wa hali ya tabianchi tunayokabiliana nayo sasa." Kinachohitajika ni mchakato mpya ambao siasa pia inahusika, pamoja na watendaji mbalimbali wa kijamii na vyombo vya kati. Kwa hiyo mwaliko unaotoka katika Waraka wa Kitume wa Fratelli tutti "kujenga jamii iliyohuishwa na hisia za urafiki na udugu unakuwa pendekezo thabiti la kuchunguza aina mpya za ushirikiano."
Wakatoliki wanapaswa kuhamasishwa katika nyanja ya kijamii
Uwepo wa Papa katika Mkutano wa COP28 huko Dubai ni ushuhuda, kama tunavyosoma zaidi, "wa ahadi yake ambayo inawahimiza Wakatoliki wote kuhamasisha kwa uwazi na uamuzi katika nyanja ya kijamii". Ni imani inayowafunga “wanafunzi wa Bwana kwa undani zaidi kwenye hatima ya wanadamu, ya viumbe vyote hai na ya nyumba yetu ya pamoja”. Shauku kwa wale waliohudhuria mkutano huo ni kwamba mtazamo wao "usaidie Kanisa la Ufaransa katika utume wake", na kwamba tumaini lao linaweza kuwa kubwa kama "upya wa Bwana Yesu" ambao "unang'aa hasa kati ya maskini, walio mbali sana, kutoka katika mantiki ya nguvu, ambapo Ufalme wa Mungu tayari unabadilisha mawazo na mioyo na kuandaa maisha yetu ya baadaye".