Simu kati ya Papa na rais mteule Milei wa Argentina
Mazungumzo yao yamethibitishwa na Msemaji wa Vyombo vya habari Vatican,Dk.Bruni.Milei alichaguliwa kuiongoza nchi hiyo ya Amerika Kusini Dominika iliyopita tarehe 19 Novemba 2023 kwa asilimia 56 ya kura zote.
Vatican News
Papa Francisko amekuwa na mazungumzo ya simu tarehe 21 Novemba 2023 na Javier Milei, Rais mteule wa Argentina. Habari hiyo, ambayo tayari iliienezwa na magazeti ya Argentina, ilithibitishwa na Msemaji mkuu wa Ofisi ya Vyombo vya Habari ya Vatican, Dk. Matteo Bruni.
Milei, kiongozi wa muungano wa "La libertad advancing", alichaguliwa Dominika tarehe 19 Novemba 2023 katika usukani wa nchi hiyo ya Amerika Kusini kwa zaidi ya 56% ya kura dhidi ya mgombea anayeendelea na Waziri wa Uchumi, Sergio Massa.
22 November 2023, 10:02