Baba Mtakatifu Francisko, Jumatano tarehe 29 Novemba 2023 amekutana na kuzungumza na wachezaji wa Timu ya Celtic “Celtic Footbal Club” Baba Mtakatifu Francisko, Jumatano tarehe 29 Novemba 2023 amekutana na kuzungumza na wachezaji wa Timu ya Celtic “Celtic Footbal Club” 

Ujasiri, Sadaka na Udumifu Ni Mambo Msingi katika Michezo

Baba Mtakatifu Francisko, Jumatano tarehe 29 Novemba 2023 amekutana na kuzungumza na wachezaji wa Timu ya Celtic “Celtic Footbal Club” ambayo siku ya Jumanne tarehe 28 Novemba 2023 “imechapana na Timu ya S.S. Lazio ya Roma ambayo imeibuka kidedea kwa kuwacharaza Celtic magoli mawili kwa nunge.” Celtic Fooball Club ilianzishwa kunako mwaka 1887 Jijini Glasgow ili kupambana na umaskini miongoni mwa wananchi; huu ni urithi mkubwa kwa timu hii.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko anasema, michezo ni mahali pa kuwakutanisha watu katika medani mbalimbali za maisha ili kufikia lengo linalotarajiwa. Michezo ni kiungo maalum cha majiundo na tunu msingi za maisha ya kiutu na kijamii. Hapa ni mahali pa kukuza na kudumisha: ukarimu, unyenyekevu, sadaka, udumifu na furaha kwa kuhakikisha kwamba, kila mtu anajitahidi kuchangia kadiri ya uwezo na karama zake, kielelezo makini cha ujenzi wa umoja na mshikamano wa udugu wa kibinadamu unaobomolea mbali kuta za tabia ya ubinafsi, uchoyo na ubaguzi na kuwakirimia watu wa Mungu ile furaha ya moyoni! Michezo katika mtazamo wa Kikristo ni njia ya utume na mchakato wa utakatifu wa maisha.

Timu ya Celtic ilianzishwa kunako mwaka 1887 ili kupambana na umaskini
Timu ya Celtic ilianzishwa kunako mwaka 1887 ili kupambana na umaskini

Mama Kanisa katika maisha na utume wake, ni Sakramenti ya wokovu; ni mtangazaji wa Habari Njema na shuhuda wa Kristo Yesu aliyeteswa, akafa na kufufuka kwa wafu. Michezo katika nafasi mbalimbali ni jukwaa la kutangaza na kumshuhudia Kristo kwa walimwengu. Ni wakati wa kuwashirikisha wengine, ile furaha ya Injili inayobubujika kutoka kwa Kristo Yesu na Kanisa lake. Michezo ni wakati muafaka wa kuonja: uzuri na utakatifu wa kazi ya uumbaji kwa kukutana na watu walioumbwa kwa sura na mfano wa Mungu. Wanamichezo wa kweli ni wajumbe na mashuhuda wa Kristo Mfufuka wanapokuwa uwanjani. Wanamichezo wanaweza kuwa ni watakatifu, kwani daima wanaitwa na kuhamasishwa kuendeleza mchakato wa maboresho ya maisha yao kila kukicha! Ujasiri, Sadaka na Udumifu ni mambo msingi katika michezo.

Ujasiri, Sadaka na Udumifu ni mambo msingi katika michezo
Ujasiri, Sadaka na Udumifu ni mambo msingi katika michezo

Ni katika muktadha wa umuhimu wa michezo, Baba Mtakatifu Francisko, Jumatano tarehe 29 Novemba 2023 amekutana na kuzungumza na wachezaji wa Timu ya Celtic: “Celtic Footbal Club” ambayo siku ya Jumanne tarehe 28 Novemba 2023 “imechapana na Timu ya S.S. Lazio ya Roma ambayo imeibuka kidedea kwa kuwacharaza Celtic magoli mawili kwa nunge.” Itakumbukwa kwamba, “Celtic Footbal Club” ilianzishwa kunako mwaka 1887 huko Glasgow ili kupambana na baa la umaskini miongoni mwa wananchi wa Jiji la Glasgow, leo hii kuna hatari ya kugeuza soka kuwa chanzo cha mapato na faida kubwa. Lakini ikumbukwe kwamba, michezo ni mahali pa kukuza na kudumisha fadhila za ujasiri, ustahimilivu, ukarimu, utu na heshima kwa watu wengine walioumbwa kwa sura na mfano wa Mungu. Wachezaji wa Timu ya Celtic wanapaswa kutambua urithi unaothaminiwa na Timu yao, dhamana na majukumu mazito wanayojitwika mebegani mwao na kwamba, wanapaswa kuonesha uadilifu, ubora wa soka pamoja na fadhila mbalimbali, changamoto na mwaliko wa kuwa ni vyombo na mashuhuda wa michezo.

Timu ya Celtic
29 November 2023, 14:57