2023.12.31 Baada ya misia ya kumbukizi ya kifo cha Papa Bebedikto XVI Askofu Mkuu  Georg Gänswein aliyeadhimisha misa amebariki kaburi lake 2023.12.31 Baada ya misia ya kumbukizi ya kifo cha Papa Bebedikto XVI Askofu Mkuu Georg Gänswein aliyeadhimisha misa amebariki kaburi lake  (Vatican Media)

Mwaka mmoja uliopita kifo cha Papa Benedikto XVI

Tarehe 31 Desemba 2023,saa 2.00 katika Kanisa kuu la Mtakatifu Petro,iliadhimishwa Misa Takatifu ya kumbukumbu ya mwaka wa I wa kifo cha Papa Benedikto XVI kilichotokea tarehe 31 Desemba 2022 iliyoongozwa na Askofu Mkuu Georg Gänswein.Na Kufuatia tafakari kuhusu miaka ya mwisho ya maisha ya Papa Benedikto XVI na urithi wake.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Papa Benedikto XVI, alikuwa Papa wa 265, aliyefariki dunia mnamo tarehe 31 Desemba 2022. Kwa kufanya kumkumbuka, Ibada ya Misa Takatifu imeadhimishwa asubuhi saa 2.00 kamili tarehe 31 Desemba 2023 katika Kanisa kuu la Mtakatifu Petro, kwenye Madhabahu ya Kiti kitakativu. Aliyeiongoza alikuwa Askofu Mkuu  Georg Gänswein, katibu wa Joseph Ratzinger tangu 2003 hadi siku za mwisho za maisha yake, ambaye kisha alizungumza katika mkutano kwenye majengo ya Campo Santo Teutonico kutoa tafakari juu ya urithi wa Papa Mstaafu. Wakati wa mahubiri hayo, Askofu Mkuu Gänswein alimfafanua Papa Benedikto wa kumi na sita kuwa "mfano mwangavu", akionesha shukrani kwa Mungu "kwa ajili ya zawadi ya maisha yake, utajiri wa mafundisho yake, kina cha taalimungu yake ya mfanyakazi huyo rahisi na mnyenyekevu katika shamba la mizabibu ya Bwana. Askofu Mkuu Ganswein alisema: “Noeli, siku bora zaidi ya mwaka!” Haya ndiyo aliyoyasema Benedikto wa kumi na sita, akiwa amejawa na mshangao, mwaka mmoja uliopita, katika Noeli yake ya mwisho hapa duniani, iliyoadhimishwa kwa roho ya imani kuu, furaha ya ndani na sala ya kujiamini.

Leo hii, Sikukuu ya Familia Takatifu, aliongeza Askofu Mkuu Ganswien "inaadhimisha kumbukumbu ya mwaka wa kwanza wa kurejea kwake katika nyumba ya Baba, ambapo - tunapotarajia na kusali - anaweza kutafakari fumbo kuu la Noeli milele. Mwangwi wa Noeli unapanuka katika liturujia ya Oktava nzima, wakati wa furaha na nuru. Katika hali hii maalum ningependa kutafakari, kuanzia baadhi ya maneno ya Benedikto XVI, jinsi ambavyo sala ni sehemu ya maisha ya Familia Takatifu: mwelekeo ambao ulibainisha sana maisha ya kila siku ya marehemu Papa na unaweza kutusaidia kuelewa fumbo hilo la  Kanisa kwamba ni familia kuu ya Mungu.” Askofu Mkuu Georg Gänswein akiendelea alisema “Hebu tuanze kutoka katika Injili ya Sikukuu hii, ambayo inatuambia kipindi cha uwasilishaji wa Yesu hekaluni. Mwinjili Luka anasimulia kwamba Maria na Yosefu, “siku za utakaso wao zilipotimia, sawasawa na sheria ya Musa, walimchukua mtoto Yerusalemu ili kumtoa kwa Bwana” (Lk 2,22). Sawa na kila familia ya Kiyahudi inayotii sheria, wazazi wa Yesu walikwenda hekaluni ili kuwaweka wakfu wazaliwa wao wa kwanza kwa Mungu na kutoa dsadka. Wakaondoka kuelekea Yerusalemu pamoja na Yesu, ambaye alikuwa na  umri wa siku arobaini tu, ili kumpeleka kwa Bwana. Katika hija hii ya imani na uwasilishaji wa Yesu hekaluni Benedikto wa kumi na sita aliona onesho la sala yao kwa Bwana, ambayo tayari waliiona na kutafakari kwa mtoto wao Yesu.”

Askofu Mkuu Ganswein ameadhimisha misa kwa ajili ya kumbu kumbu ya kifo cha Papa Mstaafu
Askofu Mkuu Ganswein ameadhimisha misa kwa ajili ya kumbu kumbu ya kifo cha Papa Mstaafu

“Katika Katekesi nzuri, aliendelea kueleza Katibu wa papa mstaafu, kuwa  iliyofanyika tarehe 28 Desemba 2011, Benedikto wa kumi na sita alielezea mtazamo wa tafakari wa Maria kwa maneno haya: “Mtazamo wa moyo wake tayari umeelekezwa kwake wakati wa Tangazo, anapopata mimba yake kupitia kazi ya Roho Mtakatifu; katika miezi ifuatayo alihisi uwepo wake hatua kwa hatua, mpaka siku ya kuzaliwa, wakati macho yake yaliweza kutazama kwa huruma ya mama kwenye uso wa mwanawe, anapomvika nguo za kitoto na kumweka horini.” Kwa njia hiyo “kumbukumbu za Yesu, zikiwa zimekazwa katika akili na moyo wake, zilitia alama kila wakati wa kuwapo kwa Maria. Aliishi na mtazamo wake kwa Kristo na kuthamini kila neno lake. Mtakatifu Luka anasema: “Kwa upande wake [Maria] aliyaweka hayo yote, akiyatafakari moyoni mwake”(Lk 2, 19), na hivyo alieleza mtazamo wa Maria mbele ya fumbo la Umwilisho, mtazamo ambao utaendelea katika kipindi chote cha Ukristo kuwepo: kulinda mambo kwa kuyatafakari moyoni.” Kwa njia hiyo Askofu kuu alibainisha kuwa “mwinjili anatujulisha moyo wa tafakari wa Mama wa Mungu, “mfano wa kila mwamini anayehifadhi na kulinganisha maneno na matendo ya Yesu, ulinganisho ambao daima ni maendeleo katika kumjua Yesu”; kuingia katika urafiki na Yeye, ambayo inakuwa, kwa kusema, ‘kuambukiza’. Kuishi katika ushirika wa kina na Yesu, kama Maria, ili kuambukiza mioyo ya kaka na dada: huu ni mwelekeo wa kimsingi wa Kanisa la kuvutia na la kimisionari.”

Misa kwa ajili ya kumbukizi ya Papa Mstaafu
Misa kwa ajili ya kumbukizi ya Papa Mstaafu

Askofu Mkuu Guanswein aidha alifafanua juu ya Papa mstaafu kwamba: “Katika miaka ya baada ya kujiuzulu kutoka kwa huduma ya Mtakatifu petro,  Benedikto XVI alijitolea zaidi ya yote kwa mwelekeo huu wa maisha ya imani. Tunakumbuka maneno yake yaliyotamkwa wakati wa sala ya Malaika wa Bwana ya tarehe 24 Februari 2013: “Bwana ananiita 'kupanda mlima', kujitolea zaidi kwa maombi na kutafakari. Lakini hii haimaanishi kuliacha Kanisa, badala yake, ikiwa Mungu ataniomba hivi ni kwa usahihi ili niendelee kulitumikia kwa kujitolea na upendo uleule ambao nimejaribu kufanya hivyo nao hadi sasa.” Sala ya Papa Benedikto wa kumi na sita, hasa katika miaka ya mwisho wa maisha yake, ilitofautishwa na kuongezeka kwa nguvu na mambo ya ndani. Hili pia lilijitokeza katika mtazamo wake na uso wake: alizidi kuwa tafakari ya Bwana mmoja ambaye, kwa nguvu za Roho Mtakatifu, aliendelea kuliongoza Kanisa lake. Katika Katekesi iliyotajwa, Papa Benedikto alieleza kwamba mtu wa kwanza kupata nguvu ya kuambukiza ya sala ya Maria alikuwa Mtakatifu Yosefu: “Upendo wake wa unyenyekevu na wa dhati kwa mchumba wake na uamuzi wa kuunganisha maisha yake na ya Maria ulimvutia na kumtambulisha pia ambaye tayari alikuwa 'mtu mwenye haki' (Mt 1:19), ndani ya urafiki wa pekee na Mungu... Injili, kama tujuavyo, haijahifadhi neno lolote la Yosefu: yake ni kimya, lakini mwaminifu, uwepo wa kudumu, na wa bidii.”

Kwa hiyo, Yosefu pia ni kielelezo kwa wazazi na sisi sote: “alimfundisha Yesu sala, pamoja na Maria. Yeye, hasa, atakuwa alimsindikiza kwenye sinagogi, katika ibada za Jumamosi, pamoja na Yerusalemu, kwa ajili ya sikukuu kuu za watu wa Israel. Yoseph, kulingana na mapokeo ya Kiyahudi, atakuwa ameongoza sala ya nyumbani katika maisha ya kila siku na kwenye hafla kuu za kidini. Kwa hivyo, katika siku za maisha ya kila siku huko Nazareti, kati ya nyumba ya kawaida na karakana ya Yosefu  Yesu alijifunza kubadilisha maombi na kazi, na pia kumpatia Mungu jitihada za kupata mkate unaohitajika kwa ajili ya familia. Askofu Mkuu  Guanswein alisisitiza kuwa Familia Takatifu ni picha ya kila familia, inayoitwa kuunda Kanisa la nyumbani, ambalo, karibu na uwepo wa Yesu, uhusiano wa kimwana na Mungu Baba unaonekana, ambao pia hubadilisha mahusiano ya kibinadamu kati ya watu. Benedikto wa kumi na sita hakubeba  jina la Yosefu tu bali pia alijaribu kumwiga Mlinzi wake, zaidi ya yote kwa upendo wake mkubwa kwa Yesu na Maria na kwa uaminifu wake kwa maisha ya kila siku yaliyoangaziwa na sala na kazi." 

Katibu wa  Papa mstaafu alisistza kwamba "Moyo wa kila siku kwake ulikuwa ni Ekaristi, chemchemi ya mwanga, nguvu na faraja. Pia alikuza kwa uaminifu liturujia ya masifu  na rozari, sala ambazo zilikuwa katika siku muundo wake. Uhusiano wa karibu sana na Bwana uliakisiwa katika mahusiano na watu waliomzunguka; mahusiano ambayo yalitofautishwa na ukarimu mkubwa, unyenyekevu na usahili, na pia katika kazi yake ya kithaalimungu na kichungaji, iliyoelekezwa daima kuelekea ukuu wa Mungu na ujenzi wa Kanisa. Turudi kwa mara nyingine tena kwa Familia Takatifu, ambamo ndani yake tunaweza kustaajabia fumbo la Kanisa linaloanza, fumbo la ushirika na Bwana na kati yetu. Benedikto wa kumi na sita asema hivi: “’Yale tuliyoyaona na kuyasikia, tunawahubiri ninyi pia, ili nanyi pia muwe na ushirika nasi’ ( 1 Yoe 1:2 ). Kwa hivyo, ushirika huu wa pande mbili na Mungu na kila mmoja hauwezi kutenganishwa. Pale ambapo ushirika na Mungu unaharibiwa..., mzizi na chanzo cha ushirika kati yetu pia huharibiwa. Na ambapo ushirika kati yetu haupatikani, ushirika na Mungu wa Utatu pia si hai na ni kweli."

Papa Benedikto wa kumi na sita Askofu Mkuu Guanswein aliendeleakusema:“Katika Ekaristi Yesu hutulisha, anatuunganisha pamoja naye, pamoja na Baba, na Roho Mtakatifu na sisi kwa sisi, na mtandao huu wa umoja unaokumbatia ulimwengu ni hakikisho la ulimwengu ujao katika wakati wetu.” Katika Ekaristi Bwana anaendelea kulijenga Kanisa, akituvuta kwake na kutuunganisha sisi kwa sisi ili kuunda familia yake kuu. Ushirika huu katika familia ya Kanisa, Baba Mtakatifu Benedikto anaendelea kusema, “Hakika ni habari njema, dawa tuliyopewa na Bwana dhidi ya upweke unaotishia kila mtu leo, zawadi ya thamani inayotufanya tujisikie kukaribishwa na kupendwa katika Mungu, ni nuru inayofanya Kanisa ling'ae kama ishara iliyoinuliwa kati ya watu. Kwa hivyo Kanisa linajidhihirisha, licha ya udhaifu wote wa kibinadamu ambao no sura zake za kihistoria, uumbaji wa ajabu wa upendo, uliofanywa ili kumfanya Kristo kuwa karibu na kila mwanamume na kila mwanamke ambaye kweli anataka kukutana naye, hadi mwisho wa nyakati. Na katika Kanisa Bwana daima hukaa pamoja nasi.” Katibu wa Papa Mstaafu kwa njia hiyo alisema, “katika Ekaristi fumbo la Noeli linabaki kuwepo, katika Ekaristi Kanisa linajengwa kuwa familia ya Mungu, katika Ekaristi tunaunganishwa na waamini wote, wakiwemo watakatifu na wapendwa wetu. Katika Ekaristi pia tunabaki kuungana na Benedikto wa kumi na sita, tukimshukuru Maalimungu  yake na kielelezo angavu cha huyu “mtenda kazi rahisi na mnyenyekevu katika shamba la mizabibu la Bwana”. Amina” Alihitimisha.

Askofu Mkuu Guanswein alibariki kaburi la Papa benedikto 16 baada ya misa
Askofu Mkuu Guanswein alibariki kaburi la Papa benedikto 16 baada ya misa

Ikumbukwe Papa Benedikito alikaa katika Kiti cha Kharifa wa Mtume Petro kuanzia tarehe 19 Aprili 2005 hadi 28 Februari 2013, na  alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 95, katika monasteri ya Mater Ecclesiae, mjini Vatican, ambako alichagua kuishi baada ya kujiuzulu utumishi wa askofu wa Roma mnamo tarehe 11 Februari 2013. Habari za kifo hicho, zilizotolewa na Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican asubuhi ya siku ya mwisho ya 2022, wakati Kanisa likijiandaa kuadhimisha Masifu ya kwanza ya maadhimisho ya Bikira Maria Mama wa Mungu, mara moja ilikwenda duniani kote na jumbe nyingi za rambirambi zilifika kutoka mabara matano, kuanzia Mabaraza ya Maaskofu, viongozi wa dini, wakuu wa nchi na serikali ambao walitaka kusisitiza sifa mbalimbali za "mfanyakazi mnyenyekevu katika shamba la mizabibu la Bwana". Alasiri, katika mahubiri yaliyotamkwa katika Kanisa Kuu la Vatican, wakati wa Te Deum, maneno ya Papa  Francisko  alisema kwa "Papa Mstaafu", mtu mtukufu na mkarimu. “Tunajisikia shukrani nyingi mioyoni mwetu – alisema kwa hisia-, shukrani kwa Mungu kwa kumtoa kwa Kanisa na kwa ulimwengu; shukrani kwake, kwa mema yote aliyofanya, na zaidi ya yote kwa ushuhuda wake wa imani na sala, hasa - aliongeza - katika miaka hii ya mwisho ya maisha ya kustaafu".

Mwaka mmoja wa kifo cha Papa Benedikto XVI 31.12.2022 -31.12.2024

Wasiwasi wa Francisko

Papa alikuwa wa kwanza kutoa heshima kwa mwili wa Benedikto XVI, muda mfupi baada ya kifo chake.  Papa Francisko mwenyewe siku chache mapema, mwishoni mwa Katekesi yake  tarehe 28 Desemba, alikuwa amewajulisha waamini hali ya kiafya ya mtangulizi wake. "Napenda kuwaomba nyote  kwa sala maalum kwa ajili ya Papa Mstaafu Benedict, ambaye kimya kimya analisaidia Kanisa", ili Bwana amfariji na kumuunga mkono "katika ushuhuda huu wa upendo kwa Kanisa, mpaka mwisho". Siku hiyo hiyo, Papa Ratzinger alipokea Upako wa Wagonjwa.

Kuaga mwisho

Baada ya taarifa za kifo chake, maelfu walitaka kumuaga Baba Mtakatifu Mstaafu, kwanza katika kanisa la Monasteri ya Mater Ecclesiae kwa ajili ya walio karibu naye, kisha kuanzia tarehe 2 hadi 4 Januari ibada hiyo ilihamia kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, ambalo aliona ziara ya waamini zaidi ya 200 elfu. Mazishi hayo yalifanyika tarehe 5  Januari 5, katika Uwanja wa Mtakatifu Pettp ambayo iliwaona  Takriban makadinali 130, maaskofu 400 na karibu mapadre 3,700 walioshirikiana na Papa Francis. Utangazaji wa mazishi hayo pia ulishuhudia uwepo wa waandishi wa habari 1,600 walioidhinishwa katika Ofisi ya habari ya Vaticanhuku watangazaji 200 wakiunganishwa. Mwili wa Papa Benedikito  XVI ulizikwa katika groto ca Vatican  mahali pale alipokuwa amezikwa  Mtakatifu Yohane Paulo II Na  baada ya kuhamishiwa kwenye Basilika juu  mnamo 2011 katika Kikanisha cha Mtakatifu Sebastian.

Kumbukizi ya kifo cha Papa Benedikto 16
31 December 2023, 16:08