Papa amepokea Hati na barua za utambulisho kwa Mabalozi kutoka nchi 6 wasiyo wakazi
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Alhamisi tarehe 7 Desemba 2023, Baba Mtakatifu Francisko amekutana na kupokea Hati na barua za Utambulisho kutoka kwa Mabalozi wapya wasio wakazi wanaowakilisha Nchi zao katika Jiji la Vatican. Hawa ni mabalozi kutoka Kuwait, New Zeland, Malawi, Guinea, Sweden na Chad. Katika hotuba yake Papa amefutahi kuwakaribisha kwa uwasilishaji wa Barua zinazowaidhinisha kama Mabalozi maalum Wasio Wakazi na Wawakilishi wa taifa lao katika mji wa vatican. Papa amewaomba wawafikishie Wakuu wao wa Nchi hisia zake za heshima, wakati huo huo hakiwakikishia kuwakumbuka katika sala kwa ajili yao na kwa ajili ya wananchi wao. Wanaanza utume wao katika wakati wa taabu hasa, unaooneshwa na kuongezeka kwa mizozo ya kivita, katika kile ambacho: “nimekiita kwa muda mrefu vita vya tatu vya ulimwengu vivilivyomegeka vipande vipande. Kwa kuzingatia wigo wa kimataifa wa migogoro inayoendelea, jumuiya ya kimataifa inajikuta ikilazimika kukabiliana na, kupitia zana za amani za diplomasia, changamoto ya kutafuta suluhisho la jumla la dhuluma kubwa zinazoisababisha mara nyingi.”
Katika Waraka wa kitume wa hivi karibuni wa Laudate Deum, Papa Francisko amebainisha kwamba alisema: “ili kukabiliana na changamoto hii kuna haja ya dharura ya urekebishaji upya wa diplomasia ya pande nyingi, ili kutoa majibu thabiti kwa matatizo yanayojitokeza na kubuni mifumo ya kimataifa yenye uwezo wa kushughulikia mazingira, afya, utamaduni na matukio ya kijamii yanayoendelea hivi sasa (rej. nambari 37-43).” Kazi nzuri na yenye subira ya kidiplomasia ambayo wanajitolea sio tu kutafuta kuzuia na kutatua mizozo, lakini pia kujumuisha kuishi kwa amani na maendeleo ya watu, kukuza heshima ya utu wa mwanadamu, kutetea haki zisizoweza kutengwa za kila mwanaume, wanawake na watoto na kukuza mifano ya maendeleo fungamani ya kiuchumi na kibinadamu.
Katika suala hili, Baba Mtakatifu anakazia kuwa Vatican inaelezea wasiwasi wake hasa kwa mustakabali wa nyumba yetu ya pamoja, hasa kwa athari ambazo mabadiliko ya tabianchi na uharibifu wa mazingira asilia unaweza kuwa nayo kwa wanafamilia walio hatarini zaidi. Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP28, ambao kwa sasa unafanyika Dubai na ambapo Papa amethibitisha alivyopenda kuwepo, unaweza kuwa hatua ya kihistoria katika kujibu kwa hekima na kuona mbele vitisho hivi vya wazi na vya sasa kwa manufaa ya wote kwa wote kama alivyosema katika Hotuba ya Mkutano, wenye kauli : “wakati ni wa dharura. [...] mustakabali wa kila mtu unategemea sasa tunayochagua.” “Tunaomba kwamba viongozi wa mataifa waungane katika kuchukua hatua madhubuti ambazo zitaturuhusu kukabidhi kwa vizazi vijavyo ulimwengu unaofanana zaidi na bustani yenye rutuba ambayo Muumba amekabidhi kwa utunzi na usimamizi wetu.”
Baba Mtakatifu amewambia mabalozi hao kuwa uwepo na utendaji wa Vatican ndani ya jumuiya ya kimataifa unasukumwa na hamu ya kukuza udugu wa kibinadamu na amani ambayo, kama vile Nabii Isaya anatangaza, ni "tunda la haki" (taz. Isa 32:17). Papa amesema wao wanapofanya utume wao, anawatakia heri, zikiambatana na maombi, kwa juhudi zao katika huduma hii bora, na anawahakikishia uwepo wa mara kwa mara wa ofisi za Curia ili kuwasaidia katika utimilifu wa kazi yao, na majukumu. Mungu awabariki sana wao, familia yao, washirika wao na wananchi wao.
Kuhusiana na Mabalozi hao:
Balozi wa Jamhuri ya Chad: Bwana Ahmad Makaila alizaliwa tarehe 14 Oktoba 1971, ameoa na ana watoto wawili. Hadi uteuzi wake alikuwa Balozi wa Ufaransa tangu tarehe 31 Januari 2023.
Balozi wa Jamhuri ya Sweden: Bwana Per Holmstrong, alizaliwa tarehe 11 Februari 1961 huko Stocolm, Baba wa Familia na watoto wawili. Hadi uteuzi huo alikuwa ni kaimu Mkurugenzi na Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano na Maendeleo ya Kimataifa MAE tangu (2018 – 2023).
Balozi wa Jamhuri ya Kuwait: Bwana Yagoub Yousef E.Kh,Alsanad, alizaliwa tarehe 27 Desemba 1969, ni baba wa familia na watoto wanne. Hadi uteuzi huo alikuwa ni Balozi nchini Uswiss tangu 2022 na Hata katika Ufalme wa Liechtenstein (tangu Oktoba 2023)
Balozi wa Jamhuri ya Guinea: Bwana Aliou Barry alizaliwa tarehe 10 Mei 1977 huko Tougué (Guinea). Baba wa Familia na watoto wawili. Hadi uteuzi huo alikuwa ni Balozi wa Gunea nchi Ujerumani tangu 16 Mei 2023.
Balozi wa Jamhuri ya New Zealand: Tara Deborah Morton. Alizaliwa tarehe 29 Juni 1980. Hadi uteuzi huo aliliwa Balozi wa New Zeland nchini Hispania kiwakilisha pia Andorra, Malta na Marocco (tangu Januari 2023)
Balozi wa jamhuri ya Malawi: Bwana Joseph John Mpinganjira. Alizaliwa tarehe 8 1964. Ni baba wa Familia na mtoto mmoja. Hadi uteuzi huo alikuwa ni Balozi wa Malawi nchini Ujerumanitangu 2021.