Papa atatoa zawadi ya Waridi la dhahabu katika siku kuu ya Bikira Mkingwa dhambi
Vatican News
Tendo la kuheshimu Picha ya Bikira Maria Mkingiwa wa dhambi ya Asili iliyopo katika Uwanja wa Hispania jijini Roma na ambayo Baba Mtakatifu Francisko atakwenda huko jioni ya tarehe 8 Desemba 2023, kama utamaduni wa kila Siku Kuu ya Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya Asili. Hiyo itakuwa inafuatiwa na sherehe ndogo nusu saa baada ya kutoka katika Basilika ya Bikira Maria Mkuu mahali ambapo Papa atafanya ziara katika Kikanisa hicho na kutoa heshima kwa kuweka Waridhi la Dhahabu katika Picha pendwa ya Salus Populi Romani.
Historia ya zawadi ya dhahabu ni ya zamani
Waridi la Dhahabu lina mzizi wa kale,kwa sababu liinaashiria baraka ya Papa na utamaduni wa zawadi hiyo ulianza zama za Kati. Katika historia ya karne nyingi Wardi la dhahabi lilitolewa katika nyumba za watawa, mahali patakatifu,wafalme na watu mashuhuri kwa kutambua kujitolea kwao kwa imani na manufaa ya wote. Kwa njia hiyo,katika maelezo ya barua kutoka katika Basilika ya Bikira Maria Mkuu tunasoma kwamba,“Pamoja na zawadi ya Waridi katika picha ya Salus,Papa Francisko anasisitiza umuhimu wa kiroho na maana kubwa ambayo picha hiyo inaashiria katika maisha ya Kanisa Katoliki na pia ikiwa ni madhabahu kongwe ya Bikira Maria Mama wa Mungu.”
Waridi la Dhahabu mnamo mwaka 1551 na 1613
Tendo la Papa la kutoa Waridi la dhahabu katika picha ya Salus, siyo tendo la kipekee la kwanza, kwa sababu la kwanza lilikuwa ni mnamo 1551 ambapo Papa Julius III, ambaye alikuwa na ibada ya kina kwa Picha hiyo ya Maria inayohifadhiwa katika Basilika ya Kipapa ya Bikira Maria Mkuu,ambapo katika Altare ya Pango la Kuzaliwa kwa Bwana alikuwa ameadhimisha Misa yake ya Kwanza. Na kunako mwaka 1613 Papa Paulo V alitoa Waridi la Dhahabu katika hafla ya kutafsiri Picha inayoheshimiwa katika Kikanisa kipya kilichokuwa kimejengwa hasa kwa ajili hiyo. Hata hivyo katika Basilika hiyo hapakuhifadhiwa mabaki ya Waridi zote mbili za dhahabu zilizotajwa hapo juu ambao zilitolewa na Mapapa wawili,na ambazo labda zilipotea wakati wa uvamizi wa Napoleon kwa Selikali ya Kipapa (rej.Mkataba wa Tolentino 1797). Ujumbe unaendelea kwamba,“Kwa hiyo, baada ya miaka 400, Papa amechagua kutoa ishara inayoonekana ya kujitolea kwake katika Picha inayoheshimiwa ili kuimarisha kifungo cha milenia kati ya Kanisa Katoliki na jiji la Roma.”
Baada ya kusikia habari za heshima hiyo, kamishna maalum wa Basilika ya Mtakatifu Maria Mkuu, Monsinyo Rolandas Makrickas, alionesha furaha yake na kusema kuwa:"Zawadi ya Waridi la Dhahabu ni ishara ya kihistoria inayoonesha wazi uhusiano wa dhati wa Papa Francisko na Mama wa Mungu ambaye mahali patakatifu hapa anaheshimiwa kwa jina la Salus Populi Romani,yaani Afya ya Watu wa Roma. Na Watu wa Mungu wataweza kuimarishwa zaidi katika mafungamano yao ya kiroho na ibada kwa Bikira Maria. na hivyo Salus tunaomba zawadi ya amani kwa ulimwengu mzima.” Alihitimisha.