Tukio la Alhamisi 21 Desemba 2023 huko Prague la ufyatuaji risasi katikati ya Uwanja wa Jan Palach katika Kitivo cha Sanaa cha Chuo Kikuu cha Charles. Tukio la Alhamisi 21 Desemba 2023 huko Prague la ufyatuaji risasi katikati ya Uwanja wa Jan Palach katika Kitivo cha Sanaa cha Chuo Kikuu cha Charles.   (ANSA)

Papa atoa salamu za rambi rambi huko Prague

Akiwakabidhi marehemu kwa huruma ya upendo ya Mwenyezi Mungu,Baba Mtakatifu snaomba nguvu na faraja ya kimungu juu ya familia na marafiki wanaoomboleza, na analihakikishia taifa maombi yake katika wakati huu mgumu.Ndiyo ujumbe wa Baba Mtakatifu uliotiwa saini na Kardinali Parolin,Katibu wa Vatican kufuatia na risasi katika Chuo Kikuu cha Charles huko Prague.

Vatican News

Akiwa amehuzunishwa sana na taarifa ya kupoteza maisha na majeraha yaliyosababishwa na kupigwa risasi katika Chuo Kikuu cha Charles huko Prague, Baba Mtakatifu anaelezea ukaribu wake wa kiroho kwa wale wote walioathiriwa na janga hili. Akiwakabidhi marehemu kwa huruma ya upendo ya Mwenyezi Mungu, Baba Mtakatifu unaomba nguvu na faraja ya kimungu juu ya familia na marafiki wanaoomboleza na analihakikishia taifa maombi yake katika wakati huu mgumu. Ndiyo ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko uliotiwa saini na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican kuhusu mkasa uliotokea Alhamisi 21 Desemba 2023 huko Prague wa ufyatuaji risasi katikati ya Uwanja wa Jan Palach katika Kitivo cha Sanaa cha Chuo Kikuu cha Charles huko Prague Juamhuri ya Czech.

Masikitiko ya Askofu Mkuu wa Prague kwa niaba ya Baraza la Maaskofu wa CZECH

Na katika tamko la Askofu Mkuu Jan Graubner, wa Prague rais wa Baraza la Maaskofu wa Czech,  kuhusiana na tukio anabainisha kuwa kuwa: “Ni kwa huzuni kubwa nilipopata habari za kupigwa risasi katika Kitivo cha Sanaa cha Chuo Kikuu cha Charles huko Prague, ambapo watu 14 walipoteza maisha na wengine wengi walijeruhiwa. Ninatoa rambirambi zangu za dhati na masikitiko makubwa kwa familia za wahanga wote ambao sasa wako katika majonzi na ninawahakikishia ukaribu wetu. Ninawaombea marehemu familia zao, wapendwa wao na marafiki zao na kwa ajili ya uponyaji wa majeruhi wote. Ninamwomba Mungu alete faraja kwa kila mtu katika kipindi hiki cha kabla ya Noeli na awasaidie kushinda maumivu na maombolezo. Mapadre wa Jimbo kuu la Prague wanapatikana ili kutoa msaada wa kiroho na ushauri kwa wote.”

Rambi rambi kutoka kwa Rais wa Italia

Na kwa upande wa ujumbe kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Italia,Bwana Sergio Mattarella: “Italia nzima ilijifunza kwa masikitiko makubwa habari za ufyatuaji risasi ambao ulishtua Chuo Kikuu cha Prague na kusababisha waathirika kadhaa na majeruhi kadhaa. Katika tukio hili la huzuni ninapenda kuwatumia maneno ya rambirambi za dhati za Jamhuri ya Italia na yangu mwenyewe. Tuko karibu na hisia za mshikamano wa pamoja kwa machungu ya familia zilizoshtushwa na kitendo cha ukatili huo na tunawatakia majeruhi ahueni ya haraka na timilifu.”

22 December 2023, 16:03