Papa atuma ujumbe kwa Kanisa la Siro-Malabar:kinzani hazitoki kwa Roho Mtakatifu

Papa alituma ujumbe wa video kwa Kanisa kuu la Ernakulam-Angamaly,nchini India,mbele ya wale wanaokataa maadhimisho ya Liturujia kulingana na mtindo ulioamuliwa na Sinodi ya Syro-Malabar na kusababisha migawanyiko na vurugu.Katika ujumbe alisisitiza kwamba nyuma ya migawanyiko hiyo kuna sababu ambazo hazina uhusiano wowote na adhimisho la Ekaristi wala Liturujia.Ni sababu za kidunia.

Salvatore Cernuzio na Angella Rwezaula-  Vatican.

Kukomesha mapigano, upinzani na hata vurugu, ambazo hazijakosekana kwa zaidi ya tukio moja, kuepuka kugeuka kuwa dhehebu linaloibuka na sio kulazimisha kusababisha vikwazo. Ndiyo mawazo ya ujumbe madhubuti wa Baba Mtakatifu kwa njia ya video kwa Kanisa Kuu la Ernakulam-Angamaly, ambapo wengi wao wanakataa mfumo wa kiliturujia ulioanzishwa na Sinodi ya Syro-Malabar. Baba Mtakatifu Francisko aliingilia kati mgawanyiko  hiyo inayopatikana ndani ya Kanisa hilo lenye ibada ya Mashariki. Kanisa kubwa na kongwe nchini India, ambalo ni chanzo cha furaha na fahari kwa Kanisa la Ulimwengu, limesambaratishwa ndani na mzozo unaoonekana kulenga mwelekeo wa kuadhimishwa kwa Misa na mapadre,yaani,iwe ni kuelekezwa kwa jumuiya au altareni. Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake  anafafanua kuwa sababu za kweli katika kinzani hiyo ni zingine. Papa anasema kuwa: “Ninajua kuna sababu za upinzani ambazo hazihusiani na adhimisho la Ekaristi wala Liturujia. Ni sababu za kidunia. Hazitoki kwa Roho Mtakatifu. Kama hazitoki kwa Roho Mtakatifu, zinatoka kwingine.”

Ombi la Baba Mtakatifu  la dhati kwa wale wanaoasi maamuzi ya Sinodi aliwaeleza kuwa: “Tafadhali msiendelee kuumiza mwili wa Kristo! Msijitenge naye tena! Na ikiwa wamewadhulumu basi wasameheni kwa ukarimu.” Majadiliano yamekuwa yakiendelea kwa miongo kadhaa katika Kanisa hilo la kale la Mashariki ambalo ni  la pili kwa ukubwa kuungana Roma baada ya lile la Kiukraine- tangu wakati huo, kwa maendeleo ya Kilatini, liturujia ilikaribia zaidi ya Magharibi na ibada ya asili ya Kisiria ya Mashariki (inayotazama altare) imebadilishwa kwa sehemu na mtindo unaotazama Jumuiya. Mnamo 1934 Papa Pio XI alikuwa ameomba kukaribiana na ibada ya zamani, iliyoachwa kwa karne nyingi; katika miaka ya 1980, maandishi mapya ya Matakatifu ya Qurbana, Misa ya ibada ya Syro-Malabar, yalichapishwa. Na tangu wakati huo matatizo yamanza kutokea.

Sinodi ya Kanisa Kuu la Maaskofu wa Syro-Malabar, iliyoadhimishwa mnamo mwaka 2021, ilitafuta suluhisho la maelewano ambapo sehemu ya kwanza ya ibada hiyo, yaani, Liturujia ya Neno, na sehemu ya mwisho inaadhimishwa na kuhani akiwatazama watu, wakati sehemu kuu ya ibada, ya Liturujia ya Ekaristi, inaadhimishwa na Padre anayetazama Mashariki, akitazama altare. Uamuzi wa Sinodi uliidhinishwa na Vatican  lakini haukukubaliwa na kila mtu. Mnamo tarehe 28 Novemba 2021, tarehe iliyochaguliwa kwa ajili ya utekelezaji wa Maandishi Matakatifu ya Qurbana, makanisa 34 yaliamua kutekeleza uamuzi wa sinodi, wakati katika Kanisa kuu la Ernakulam-Angamaly, mapadre wengi na waamini waliendelea kujithibitisha Liturujia yao maalum  na mshereheshaji kila wakati wakikabiliana na waamini  tofauti na wengine wa Kanisa la Syro-Malabar.

Kinzani hizo zimefikia sauti za hasira kiasi kwamba Askofu Mkuu Cyril Vasil', aliyetumwa na Baba Mtakatifu  Francisko mnamo mwezi  Agosti uliopita  ili kusuluhisha hali ya Kanisa kuu,  kwa kuhakikisha utekelezaji wa mageuzi ya kiliturujia yaliyoidhinishwa na Sinodi, aliteseka juu ya vitendo vya uchokozi  kama vile kurusha mayai na vitu vingine. Katika hali hii yote ngumu, kwa hivyo, neno la Papa Francisko sasa linafika kwa njia ambayo yeye mwenyewe anatambua kuwa isiyo ya kawaida, ujumbe kwa video, lakini lengo ni kwamba hakuna mtu mwenye shaka zaidi juu ya nini anawaza Papa.” Tayari katika siku za nyuma, kwa hakika, Baba Mtakatifu alikuwa amelihutubia Kanisa hilo la kale la Kihindi kwa njia ya barua mbili: moja mnamo Julai 2021 iliyoandikwa kwa Maaskofu, mapadre, watawa kike na kiume na walei, ambao  Papa Fransisko aliwahimiza “kutembea pamoja na watu wa Mungu kwa sababu umoja unashinda migogoro yoyote; na barua nyingine  ilikuwa ni mnamo Aprili 2022 iliyotumwa kwa Kanisa kuu la Ernakulam-Angamaly ambapo alitoa mwaliko wa kuzingatia maamuzi ya Sinodi ya Kanisa la Syro-Malabar juu ya Mtindo wa kuadhimisha  liturujia uliotolewa na katika  Qurbana.

Barua hizo zinaonekana kuwa hazikuwa na matokeo yaliyotakiwa, kama  vile Papa mwenyewe alivyobainisha kuwa: “Tayari niliawaandikia mara kadhaa huko nyuma, lakini nunajua kuwa sio kila mtu amesoma barua zangu,” alisema kwenye video ambapo, pamoja na mambo mengine, aliongeza kusema inatutaka tutii maamuzi ya Sinodi, na tusiwafuate wale - wakiwemo mapadre - wanaosukuma upinzani na kwa hiyo kutoa sadaka ili kuhifadhi ushirika, ambao  bila huko hakuna Kanisa  na kuna hatari ya kugeuka kuwa aina ya “dhehebu linaloibuka.” Tafadhali kuwa makini! Uwe mwangalifu, shetani asije akakushawishi ukageuka kuwa dhehebu. Wewe ni Kanisa, usiwe dhehebu. Usilazimishe mamlaka ya kikanisa yenye uwezo kutambua kwamba umeacha Kanisa, kwa sababu haushiriki tena na wachungaji wako na pamoja na Mrithi wa Mtume Petro, aliyeitwa kuwathibitisha ndugu wote katika imani na kuwahifadhi. katika umoja wa Kanisa. Kwa maumivu makubwa, basi, vikwazo husika vitapaswa kuchukuliwa. Sitaki kuja kwa hilo.

Baba Mtakatifu baadaye alisisitiza juu ya uamuzi wa Sinodi ambayo, “baada ya kazi ndefu na ya kuchosha, ilipata makubaliano juu ya njia ya kuadhimisha Qurbana Takatifu. Hisani na upendo kwa ushirika vilisukuma washiriki wake kuchukua hatua hii, hata kama baadhi yao hawaoni aina hii ya sherehe kuwa bora. “Ninajua kwamba kwa miaka mingi baadhi, ambao wanapaswa kuwa mifano na walimu wa kweli wa ushirika, hasa mapadre, wamekuwa wakiwasukuma kutotii na kupinga maamuzi ya Sinodi. Ndugu msiwafuate!” Papa alikumbuka kwa uchungu kwamba vurugu zilitokea hasa ​​dhidi ya wale wanaotaka kubaki katika ushirika na kusherehekea kama Sinodi ilivyoanzishwa.”

Kwa hiyo, Baba Mtakatifu aliwaeleza moja kwa moja watu waamini wa Mungu, wakleri, wanaume na wanawake watawa na zaidi ya yote “waamini walei wapendwa” ambao anasema, wana imani kubwa kwa Bwana na kulipenda Kanisa. Katika jina la Bwana, kwa manufaa ya kiroho ya Kanisa lenu, la Kanisa letu, ninakuomba mponye mpasuko huu. Ni Kanisa lenu, ni Kanisa letu. Mrejesha ushirika, mbaki katika Kanisa Katoliki!” Askofu wa Roma amewaomba mapadre wasijitenge na njia ya Kanisa lao, bali watembee pamoja na maaskofu wao: “Mkubalianeni kutekeleza yale ambayo Sinodi yenu imeanzisha... Je! Kanisa limezuiwa na mipango mingi haiwezi tena kutenda mema katika huduma ya watu watakatifu wa Mungu, katika huduma ya utakaso wa watu wa Mungu?”.

Katika kuelekea kwenye Maandalizi ya Noeli Papa Francisko anatumaini kwamba jimbo kuu litakubali kwa unyenyekevu na uaminifu kupatana na Kanisa lingine, kwa kuheshimu dalili zote za Sinodi. Dalili iko wazi: “Kwa hivyo, kwa Noeli  ijayo, katika Jimbo Kuu Ernakulam-Angamaly kama katika Kanisa zima la Syro-Malabar, Qurbana inapaswa kuadhimishwa kwa ushirika, kwa kufuata mtindo wa Sinodi". Papa pia alisema, “itakuwa Noeli kwa watu wao wote, kwa kila mtu.” Kwa hiyo pendekezo la mwisho, likimnukuu Mtakatifu Paulo katika Waraka wa kwanza kwa Wakorintho: “Ekaristi na iwe kielelezo cha umoja wenu. Msiuvunje Mwili wa Kristo ambao ni Kanisa, ili msile na kunywa hukumu yenu.”

11 December 2023, 12:17