Papa 2023:Safari,mageuzi na miito ya amani bila kuchoka

Mwaka wa kina na mgumu unakaribia kumalizika kwa Papa,aliyeadhimisha miaka 10 ya upapa mwezi Machi.Ziara 5 za kitume:Congo DRC na Sudan Kusini,Hungaria,Lisbon,Mongolia na Marseille.Kulazwa hospitalini na upasuaji,Gemelli.Mamia ya mikutano,marekebisho ya Katiba ya Vatican na hati nyingine nyingi.Kikao cha 1 cha Sinodi Oktoba na miito mingi kwa Ukraine na Nchi Takatifu.

Na Salvatore Cernuzio  - Vatican.

2023 ulikuwa ni mwaka wa kushehereka miaka kumi  ya  kuchaguliwa kuwa Papa  katika kiti cha Mtume Petro. Ni mwaka wa ziara zilizohairishwa na kisha kurejeshwa kama vile (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Sudan Kusini) lakini pia ya zile zilizofutwa kama vile ya (Dubai kwa ajili ya Cop28); Ni mwaka wa matatizo ya kiafya kati ya kulazwa hospitalini, upasuaji wa laparotomi na bronchitis ya kuambukiza ya papo hapo. Mwaka wa vita, nchini  Ukraine :iliyoteswa” au ile  ya nchi iliyozuka na shambulio la kigaidi la Hamas na majibu ya Waisraeli huko Gaza, ambayo yalishuhudia kuongezeka kwa miito na juhudi za kidiplomasia. Mwaka wa hatua ya kwanza ya Sinodi ya kisinodi  iliyokuwa na washiriki zaidi ya 400 kutoka kila kona ya dunia na ya Uchaguzi wa  makadinali 21 wapya wenye asili tofauti za kijiografia. Mwaka, pia ulikuwa wa wa ‘majaribio: mchakato usioingiliwa wa mageuzi (moja juu ya yote, “Katiba" mpya ya Mji wa  Vatican); michakato ya fursa za kichungaji, kama vile hati ya Fiducia Supplicans juu ya baraka kwa watu wa jinsia moja na "wasiokuwa wa kawaida" ambayo imeibua hisia kali tofauti; kesi za kimahakama, hasa zile zinazojulikana kama "Palace of London" yaani ya Jimba la London. Kwa kifupi, mwaka  2023 umekuwa mwaka mkali na mgumu ambao unakaribia mwisho kwa Papa Francisko, ambaye alisherehekea siku yake ya kuzaliwa ya miaka 87 mnamo tarehe 17  Desemba iliyopita.

Kifo cha Benedikto XVI

Mwaka ambao uliahidi kuwa na changamoto tangu mwanzo kuanzia na kifo cha Papa Mstaafu Benedikto XVI akiwa na umri wa miaka 95 mnamo tarehe  31 Desemba 2022. Jorge Mario Bergoglio, baada ya kuutahadharisha ulimwengu kuhusu hali ya afya ya Joseph Ratzinger na kuweza kumuaga katika Monasteri ya Mater Ecclesiae, aliadhimisha misa ya mazishi ya mtangulizi wake katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mnamo  tarehe 5 Januari. Ilikuwa ni maadhimisho ya utulivu mbele ya waamini wapatao elfu 50 waliomuaga Baba Mtakatifu wa Bavaria, ambaye kisha alizikwa kwenye Groto za Vatican.

PAPA AKIAGA MTANGULIZI WAKE
PAPA AKIAGA MTANGULIZI WAKE

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Sudan Kusini

Ikiwa maombolezo yalikuwa mwanzoni mwa Januari 2023, furaha iliashiria mwisho wa mwezi kwa ziara ya  Papa barani Afrika ambaye alitimiza "ahadi yake" ya kutembelea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Sudan Kusini. Safari hiyo ilipangwa kufanyika mnamo  Julai 2022 lakini kwa sababu ya matatizo ya goti yalikuwa yamemzuia Papa kusafiri katika nchi hizo mbili. Hakuna mtu kati ya Wacongo na Wasudan Kusini aliyewahi kusema juu ya kughairiwa bali tu kuahirisha: Kuanzia Januari 31 hadi Februari 5, Papa Francisko alikwenda Kinshasa na kisha Juba, akikutana na maelfu ya watu ambao walipongeza miito  yake dhidi ya ufisadi na malengo ya uporaji ("(«Giù le mani dall’Africa»,ondoeni mikono yenu Afrika “ ni moja ya maneno muhimu yaliyosikia) na dhidi ya vita ambavyo vimesababisha vifo, majeruhi na watu waliokimbia makazi yao. Mkutano na waathirika wa ubakaji na mateso huko Kiwu Kaskazini katika Jimbo la Kinshasa (l’incontro con le vittime di stupri e torture nel nord Kiwu) ulikuwa wa kugusa moyo, kama ( la preghiera ecumenica a Juba)vile sala ya kiekumene huko Juba iliyoshirikishwa paoja na Mkuu  wa Kianglikana Justin Welby na msimamizi wa Mkutano Mkuu wa Kanisa la Scotland, Ian Greenshields.

Hungaria

Ahadi iliyotekelezwa pia ilikuwa ni ziara ya mwisho wa Aprili hadi Hungaria, ambayo ilimwona Papa akitembelea Hungaria kwa ajili ya kuhitimisha Kongamano la Ekaristi la kimataifa mnamo Septemba 2021, kabla ya kuendelea nchini Slovakia. Papa Francisko alitumia siku tatu katika nchi ya Hungaria (28-30 Aprili), pia alikutana na wakimbizi kadhaa wa Kiukreni. Na kwa kuangalia kwa usahihi Ukraine "iliyoteswa",(da Budapest ha posto la comunità internazionale davanti a un quesito:kutoka Budapest aliuliza  jumuiya ya kimataifa swali: "Juhudi za ubunifu za amani ziko wapi?"

PAPA HUNGARIA
PAPA HUNGARIA

WYD huko Lisbon

Amani kama lengo la vizazi vijavyo ilikuwa moja ya mada kuu ya ziara  ya Papa huko Lisbon nchini Ureno kwa Siku ya 37 ya Vijana Ulimwenguni kuanzia tarehe 2-6 Agosti, ambao pia alikwenda katika Madhabahu ya Mama wa Fatima. Wavulana na wasichana milioni moja na nusu walifika katika mji mkuu wa Ureno kwa ajili ya hafla kubwa ya ulimwengu, ambayo itarudiwa mnamo 2027 huko Seoul (Korea Kusini). Kimbunga cha mikutano ya hadhara na ya faragha kwa Papa ambaye, katika ufunguzi wa  siku ya Vijana (WYD,) ( in apertura della Gmg, ha pronunciato una delle frasi più rappresentative del pontificato) alitamka mojawapo ya vifungu vya uwakilishi vya upapa kuwa: "Kanisani kuna nafasi kwa kila mtu ... Kila mtu, kila mtu, kila mtu"

Mongolia

Ulikuwa haujapita hata mwezi mmoja baada ya Lisbon, Papa  Francisko alikwenda Mongolia, nchi ya bara la Asia iliyo katikati ya Urussi na China, nchi ya Genghis Khan na "nyumba" ya jumuiya ndogo ya Kikatoliki, iliyozaliwa upya kati ya vifusi vya ukomunisti, yenye karibu watu 1700 waliobatizwa. Kundi "ndogo" kiasi kwamba yote yanatosha katika picha moja: ile iliyopigwa mbele ya Kanisa Kuu la Watakatifu Petro na Paulo, mwishoni mwa moja ya mikutano mbalimbali iliyoakisi safari, ambayo pia haikusahaulika na ishara ya Papa huko. mwisho mwa Misa huko Ulaanbaatar, kwa  kupeana mikono na askofu mstaafu na Askofu katika Jimbo la Hong Kong  huku akituma salamu kwa "watu mashuhuri wa China".

PAPA MONGOLIA
PAPA MONGOLIA

Marseille na safari ambayo haikufanyika ya Dubai

Muda wa kutosha tu wa kupona kutokana na shida za Mongolia ambaco  mnamo Septemba 22 Papa Francisko alipanda ndege nyingine kufika Marseille na kushiriki katika ‘Rencontres Méditerranéennes; yaani Mikutano ya Mediterranea, tukio ambalo lilihusu  mada ya uhamiaji. Mbele ya mamlaka za kiraia na za kikanisa za nchi zinazoiangalia Mediterania, Papa Bergoglio alitoa hotuba ndefu na ya kina ambapo aliomba masuluhisho madhubuti ya kuzuia "Mare Nostrum"- yaani -‘bahari yetu’ kuwa "Mare Mortuum"- ‘bahari ya kifo’. Maneno mazito, kama yale ambayo Papa alipaswa kuwa nayo na alitaka kutamka katika muktadha mwingine huko(Dubai) kuhusu suala lingine la mada(shida ya tabianchi)wakati wa COP28. Safari ya ndege ilikuwa tayari, mpango ukakamilika na pia ulijumuisha mfululizo wa mikutano ya faragha na wakuu wa nchi na serikali. Ugonjwa wa pumu ulimlazimisha Papa Francisko kughairi safari hiyo, kwa kusikiliza pendekezo la madaktari.

PAPA MARSILIA
PAPA MARSILIA

Matatizo ya kiafya

Mnamo 2023, Papa Francisko alilazwa hospitalini mara mbili katika hospitali ya  Gemelli Roma  ambapo kwa mara ya kwanza mnamo Machi kwa ajili ya  ugonjwa wa  kupumia unaoambukiza ambao ulihitaji usimamizi wa tiba ya antibiotic; mara ya  pili kati ya Mei na Juni kwa ajili ya upasuaji wa laparotomia na ukuta wa tumbo kwa kutumia bandia. Ukaaji wa kwanza wa hospitali ulidumu kwa muda mfupi; wa pili ulichukua kama siku kumi. Alipoachiliwa tarehe 16 Juni, Papa alirejea katika shughuli kamili mara moja. Jibu la “Niko hai” lilikuwa kwa mtu yeyote aliyeuliza kuhusu hali yake ya afya. "Haipo kwenye ajenda" badala yake kwa wale waliohofia uwezekano wa kujiuzulu upapa kutokana na udhaifu wa chombo hicho. Jaribio lingine kwa Papa lilikuwa ugonjwa wa kupumua mkali uliompatia shida mwishono mwa mwezi  Novemba na ambao ulimlazimu kufuta ahadi za umma na za kibinafsi. Kama ilivyokuwa nyakati za UVIKO, Papa alithibitisha wakati wa sala ya Malaika Bwana akia katika Nyumba ya Mtakatifu  Marta, lakini kwa mara ya kwanza kwa msaada wa monsinyo kutokana na ugumu wa kusoma. Vivyo hivyo kwa katekesi ambapo hata hivyo Papa, ijapokuwa kwa sauti ndogo, alitaka kuwa yeye mwenyewe asome maombi ya mwisho kwa ajili ya amani.

PAPA HOSPITALINI GEMELLI
PAPA HOSPITALINI GEMELLI

Maumivu ya vita na utume wa Kardinali Zuppi

Vita, vita vyote, kuanzia na vile vya Ukraine na kuishia na vile vilivyolipuka katika Nchi Takatifu, vimekuwa msalaba wa mwaka huu wa 2023. Mwaka ambao pia utakumbukwa kwa ajili ya utume wa Kardinali Matteo Zuppi, rais wa  Baraza la Maaskofu Italia (CEI), kuwa mjumbe wa Papa kwa ajili ya "kupunguza mvutano" huko Ukraine. Ziara hizo zimegawanywa katika hatua nne (Kyiv, kuanziaa 5-6 Juni; Moscow, 28-29 Juni; Washington, 17-19 Julai; Beijing, Septemba 13-15), ujumbe huo ulimwona Kardinali Zuppi katika mazungumzo na mamlaka ya kisiasa na kikanisa ya nchi hizo nne, hasa kuhusu suala la watoto wa Kiukraine kupelekwa Urussi kwa nguvu. Suala pekee ambalo Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky mwenyewe aliomba msaada kutoka Vatican, alipopokelewa mnamo Mei 13 kwa dakika 40 mjini Vatican  kwa mara ya kwanza tangu mwanzo wa vita baada ya mazungumzo kadhaa ya simu (ya mwisho mnamo Desemba 28) .

KARDINALI MATTEO ZUPPI RAIS WA CEI
KARDINALI MATTEO ZUPPI RAIS WA CEI

Kwa upande wa Kiukraine, uwepo wa Papa pia ulihuishwa na kutumwa kwa dawa, chakula na misaada na kwa safari nyingi za Kardinali mlozi Konrad Krajewski, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Upane aliyekwenda kwenye maeneo yaliyokumbwa na vita. Kardinali Krajewski pia alikuwa mwakilishi wa Papa katika Yerusalemu wakati wa sikukuu hizi za Noeli 2023, aliyetumwa kupeleka ukaribu wa Askofu wa Roma kwa Wakristo wa Bethlehemu na, kwa mbali, kwa wakazi waliouawa wa Gaza.

KARDINALI KRAJEWSKI HUKO NAZARETH
KARDINALI KRAJEWSKI HUKO NAZARETH

Miito  kwa Israeli na Palestina

“Mlipuko wa mzozo katika Mashariki ya Kati, kufuatia shambulio la kikatili la magaidi wa Hamas dhidi ya Israeli  mnamo tarehe 7 Oktoba, umetulazimisha kufikiria upya mbinu mpya za kuingilia kati kwa suluhisho la amani”. Kwa upande wake, Papa tangu wakati wa kwanza alisisitiza ni nini hasa zingekuwa njia za kuondokana na  kimbunga cha vurugu: kuachiliwa kwa mateka wa Israel na kusitishwa kwa mapigano mara moja. Papa Francisko mwenyewe, baada ya kupigiwa simu na  Rais Biden, Abbas na Erdogan, alikutana mnamo Novemba 22 na familia za mateka na pia jamaa za watu wanaougua athari za milipuko ya mabomu katika Ukanda huo ambapo waathrika hadi sasa ni zaidi ya elfu 20. Ishara hiyo, pamoja na baadhi ya maneno ya Papa juu ya ukweli kwamba kinachotokea sasa katika Ardhi Takatifu ni "ugaidi", yameibua ukosoaji na mabishano hasa kutoka kwa wawakilishi wa ulimwengu wa Kiyahudi. Kama ilivyo kwa Urussi na Ukraine, Papa Francisko anashikilia kanuni hiyo ya "usawa" ambayo imekuwa "mtindo" wa diplomasia ya Vatican, kama Kardinali Parolin alivyosema hivi karibuni, ambapo Diplomasia haiangukii katika makundi ya kisiasa bali katika utume wa msingi wa Mrithi wa Petro: wa kukaa karibu na wale wanaoteseka, na bila ubaguzi.

PAPA ALIKUTANA NA FAMILIA ZA PALESTINA
PAPA ALIKUTANA NA FAMILIA ZA PALESTINA

Sinodi ya Kisinodi

Vita katika eneo la Mashariki ya Kati vilianza wakati il Sinodo sulla Sinodalità,Sinodi ya Sinodi ikiadhimishwa mjini Vatican mwezi mzima wa Oktoba, kilele cha safari ya miaka mitatu ilianza "kutoka chini", na majimbo ya mabara matano, na kikao cha kwanza cha ratiba ambayo Papa Francisko anataka kuendelea mwaka 2024 . Sinodi  iliyotanguliwa na uchapishaji wa ( risposte del Papa ai Dubia )majibu ya Papa kwa Dubia ya Makardinali watano juu ya masuala ya mafundisho - ilifunguliwa tarehe 4 Oktoba na kushuhudia ushiriki wa Makardinali 464, Maaskofu, wanaume na wanawake watawa, wamisionari, wanaume na wanawake walei. Wakipangwa kwenye meza za duara, mababa na mama wa sinodi walitoa mawazo na vidokezo vya kuitikia maombi na matakwa ya Makanisa yote ulimwenguni kuhusu mada kama vile wajibu wa walei na wanawake, huduma ya maaskofu, ukuhani, utume wa kidijitali, uekumene, unyanyasaji.  Kila kitu kilikuja pamoja katika ripoti ya mwisho iliyopigiwa kura na kuchapishwa tarehe 28 Oktoba.

PAPA WAKATI WA SINODI
PAPA WAKATI WA SINODI

Laudate Deum na hati zingine

Katika mwaka unaojulikana na makadinali wapya na uteuzi mpya katika Curia Romana, kwa upyashaji wa C9 yaani makardinali washauri wa Papa, kwa kuinua au kugawanya nafasi, nyaraka kadhaa zinapaswa pia kuoneshwa. Kwanza kabisa, Waraka wa kitume l’esortazione apostolica Laudate Deum, Laudate Deum, ambao ni mwendelezo wa Laudato si' ambao Papa kwa mara nyingine tena aliinua kilio dhidi ya mgogoro wa nyumba ya yetu ya Pamoja  (4 Oktoba); Baadaye Waraka wa kitume C'est la confiance (l’esortazione apostolica C’est la confiance) kwa ajili ya kumbukumbu ya miaka 150 ya kuzaliwa kwa Mtakatifu Teresina  wa Mtoto Yesu (lettera apostolica Sublimitas et miseria hominis )(15 Oktoba); hatimaye barua ya kitume Sublimitas et miseria hominis iliyotolewa kwa kazi ya mwanafalsafa na mtaalimungu Blaise Pascal, katika karne ya nne ya kuzaliwa kwake (19 Juni).  Nyaraka zingine kadhaa zilizochapishwa mnamo 2023 zimefunga hatua muhimu za mchakato wa mageuzi ulioanza tangu mwanzo wa upapa. Miongoni mwa haya, Sheria ya Msingi iliyotolewa tarehe 13 Mei inasimama wazi, (la Legge fondamentale emanata il 13 maggio)ambayo Papa aliifanyia marekebisho ya "Katiba" ya mji wa Vatican, kuchukua nafasi ya ile ya mwaka 2000, ili kutekeleza ahadi za kimataifa zilizofanywa na Kiti Kitakatifu. Tarehe 6 Januari, Papa alichapisha katiba ya kitume Katika Ushirika wa Kinanisa( costituzione apostolica In Ecclesiarum Communione) ili kupanga upya Vikariati ya Roma. Hii ilifuatiwa, katika kipindi cha mwaka, na amri, maandishi  na  (Motu propri,) barua binafsi, ikiwa ni pamoja na marekebisho ya sheria ya jinai na mfumo wa mahakama wa Vatican (12 Aprili).

WARAKA WA LAUDATE DEUM WA PAPA FRANCISKO
WARAKA WA LAUDATE DEUM WA PAPA FRANCISKO

Waamini wanaomba

Kuhusu hati, zile zilizotolewa na Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa, ambalo kwa sasa linaongozwa na Kadinali Victor Manuel Fernández  wa Argentina, kati ya Novemba na Desemba katika kujibu maswali kutoka kwa maaskofu au makadinali. Kuna mada mbalimbali: (la possibilità per le persone transessuali di ricevere il Battesimo,)uwezekano wa watu wa jinsia moja kupokea Ubatizo, pamoja na watoto wa wapenzi wa jinsia moja hata kama walizaliwa kutoka katika tumbo la kukodisha;(divieto): marufuku kwa Wakatoliki kujiunga na Freemason; utunzaji wa majivu ya marehemu nyumbani; kuhimiza akina mama wasio na waume ili kupata Sakramenti. Hati nyingine, iliyochapishwa tarehe 18 Desemba, ni Fiducia Supplicans ambayo, iliyoidhinishwa na Papa, ambayo ilifungua uwezekano wa kuwabariki watu "wasio wa kawaida" wa jinsia moja,  lakini  iwe nje ya ibada yoyote au  isiyoiga mtindo wa  harusi. Hati hiyo ingawa ilikubaliwa katika majimbo kadhaa( reazioni contrarie),imezua athari mbaya kwa baadhi ya maaskofu na waamini wengi.

KARDINA VOCTOR EMANUEL FERNANDEZ
KARDINA VOCTOR EMANUEL FERNANDEZ

Michakato

Kwa mwaka 2023 basi itakumbukwa kwa kuwa mwaka ulioona hitimisho la mchakato mrefu na mngumu wa mahakama juu ya usimamizi wa fedha za Vatican, uliohitimishwa baada ya kusikilizwa kwa kesi 86 mnamo 16 Desemba na kifungo cha kwanza cha miaka 37 kwa washtakiwa tisa. Kesi ya madai ya mkaguzi mkuu wa zamani Libero Milone na kesi ya usimamizi wa fedha ya Kwaya ya Kikanisa cha Sistine ilianza kusikilizwa katika Mahakama ya Vatican mnamo Januari na Mei. Kuhusu kesi, tarehe 27 Oktoba Papa Francisko aliamua kuondoa sheria ya vikwazo ili kuruhusu kesi ya Mjesuit wa  wa zamani na msanii maarufu Marko Rupnik, mshitakiwa wa unyanyasaji wa kisaikolojia na kijinsia na baadhi ya watawa.

MAHAKIMU WA MAHAMA YA KIPAPA
MAHAKIMU WA MAHAMA YA KIPAPA

Kuhusu mwaka 2024, unaokuja Papa mwenyewe alifichua ahadi zake za baadaye katika baadhi ya mahojiano mengi yaliyotolewa mwaka huu. Papa Bergoglio amezungumza mara kadhaa kuhusu uwezekano wa safari ya kuelekea nchini kwao Argentina, kuanzia mwezi Novemba chini ya uongozi wa rais mpya Javier Milei. Alirudia pia katika mahojiano ya hivi karibuni  na Televisheni ya Mexico N+ ambapo alizungumza juu ya uwezekano wa safari za Ubelgiji na Polynesia. Hapo awali alitaja safari ya Kosovo. Huku akisubiri uthibitisho juu ya “harakati  la kimataifa”, mwakani Papa ataendelea kutembelea ndani ya Roma,na mikutano na mapadre katika parokia mbalimbali, akianzia na zile za pembezoni kama alivyokuwa amefanya katika miezi ya hivi karibuni ya  kwenda kanisani. Vitongoji vya Primavalle, Villa Green na Asilia. Pia kwa 2024, ziara ya Verona imepangwa tarehe 18 Mei na tunatazamia Jubilee ya 2025, ambayo maandalizi yanaendelea na mikutano miwili ya nchi mbili imefanyika kati ya Vatican  na Serikali ya Italia.

31 December 2023, 10:51