Papa:Matokeo ya haki za binadamu bado hayajaonekana vya kutosha
Na Angella Rwezaula, - Vatican
Dominika tarehe 10 Desemba 2023, Baba Mtakatifu Francisko, mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana, akiwageukia waamini na mahujaji walifika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, katika Dominika ya II ya Majilio, amesema kuwa Miaka 75 iliyopita, tarehe 10 Desemba 1948, Azimio la Kimataifa la Haki za Kibinadamu lilitiwa saini. Ni kama barabara kuu, ambayo hatua nyingi zimepigwa, lakini nyingi bado hazipo, na kwa bahati mbaya wakati mwingine tunarudi nyuma. Ahadi ya haki za binadamu haijakamilika! Katika suala hili, mimi niko karibu na wale wote ambao, bila matangazo, katika maisha halisi ya kila siku, wanapambana na kulipa gharama kibinafsi kutetea haki za wale ambao hawahesabiwi.”
Kuachiliwa wafungwa wa Kiarmenia na Kiazabajani
Baba Mtakatifu akiendelea ameelezea kufurahi kwa sababu ya “kuachiliwa kwa idadi kubwa ya wafungwa wa Kiarmenia na Kiazabajani.” Ni mategemeo yake kwa matumaini makubwa kuwa ishara hii chanya ya uhusiano kati ya Armenia na Azerbaijan, itaendelea kwa ajili ya amani ya Caucasus ya Kusini, na amevihimiza vyama na viongozi wao kuhitimisha Mkataba wa Amani haraka iwezekanavyo.”
Mkutano wa Cop28
Baba Mtakatifu akikumbusha tukio la Kimataifa la Tabianchi linaloendelea huko Dubai ameleza kuwa “litakamilika baada ya siku chache. Ninawaomba muombe kwamba , matokeo mazuri yapatikane kwa ajili ya utunzaji wa nyumba yetu ya pamoja na ulinzi wa idadi ya watu.”
Tuombee Ukraine iliyoteswa, Palestina, Israel
Papa amesisitiza kuwa:“Na tunaendelea kuwaombea watu wanaoteseka kutokana na vita. Tunaelekea Noeli: Je tutaweza, kwa msaada wa Mungu, kuchukua hatua madhubuti kuelekea amani? Si rahisi, tunajua. Migogoro fulani ina mizizi ya kihistoria. Lakini pia tunao ushuhuda wa wanaume na wanawake ambao walifanya kazi kwa hekima na subira kwa ajili ya kuishi pamoja kwa amani.” Kwa kuata mfano wao! Kila juhudi zifanywe ili kushughulikia na kuondoa sababu za migogoro. Na wakati huo huo - tukizungumzia haki za binadamu - raia, hospitali, maeneo ya ibada lazima yalindwe, mateka lazima waachiliwe na kuhakikishiwa misaada ya kibinadamu. Tusisahau Ukraine iliyoteswa, Palestina, Israel.”
Moto Tivoli
Papa Francisko akiendelea amesema kuwa: “Pia ninawahakikishia maombi yangu kwa waathiriwa wa moto uliotokea siku mbili zilizopita katika hospitali ya Tivoli.” Amewsalilia wote kwa upendo, Warumi na mahujaji kutoka Italia na sehemu nyingine za dunia, hasa waamini wa Matakatifu Nicola Manfredi, maskauti watu wazima wa Scafati na vikundi vya vijana kutoka Nevoli, Gerenzano na Rovigo.” Kwa kuhitimisha amewatakia Dominika Njema, tafadhali wasisahu kusali kwa ajili yake, amewatakia mlo mwema na kwaheri ya kuonana.