Papa:Tukutane na Yesu kwa kila kaka na dada anayehitaji
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Katika Dominika ya kwanza ya Majilio tarehe 3 Desemba 2023, Baba Francisko aliongoza Sala ya Malaika wa Bwana kutokea katika Nyumba ya Mtakatifu Marta mjini Vatican, huku akimwachia Monsinyo Paolo Braida wa Sekretarieti ya Vatican usomaji wa tafakari ya Injili ya siku. Katika Tafakari hiyo Papa anabainisha kuwa: “Leo katika Dominika ya kwanza ya majilio kwa kifupi Injili ambayo Liturujia inapendekeza kutoka (Mk 13, 33-37), Yesu anatuelekeza ushauri mara tatu rahisi na wa moja kwa moja wa kesheni(rej. Mk. 13,33.35.37). Kwa hivyo mada ni kukesha. Je, tunapaswa kuielewaje? Wakati mwingine tunafikiria fadhila hii kama mtazamo unaochochewa na woga wa adhabu inayokaribia, kana kwamba ni kimondo kinakaribia kuanguka kutoka angani na kinatishia kutulemea ikiwa hatutakiepuka kwa wakati. Lakini hii hakika si maana ya kukesha kwa Kikristo!”
Yesu anaonesha kwa msemo, akizungumzia juu ya Bwana atakayerudi na watumishi wake wanaomsubiri(Mk 13,34). Mtumishi katika Biblia ni mtu wa imani wa bwana, ambaye mara nyingi kuna uhusiano wa kushirikiana na wa upendo. Tufikiria kwa mfano ambao mtumishi wa Mungu ulifafanuliwa na Musa (Nm 12,7) na hata Maria anajisemea mwenyewe kuwa, "Tazama, mimi Mjakazi wa Bwana" (Lk 1,38). Kwa hiyo kukesha kwa watumishi siyo kwa hofu, lakini kwa shauku, katika kusubiri ili kwenda kukutana na Bwana wao anayekuja. Katika tafakari hiyo Baba Mtakatifu anabainisha aidha kuwa watumishi hao “Wako tayari kwa kurudi kwakebwana kwa sababu wanampenda, kwa sababu wanapanga kumruhusu apate kuingia katika nyumba ya kukaribisha na safi akifika: wanafurahi kumuona tena, hadi kufikia wamngojea kurudi kwake kama sherehe ya familia kubwa ambayo wao ni sehemu yao. Ni subira yenye nguvu ya upendo ambao tunataka hata sisi kujiandaa kumpokea Yesu. Ni katika Noeli ambayo itaadhimishwa baada ya majuma machache, mwishoni mwa kipindi cha nyakati wakati atakuja kwa utukufu, kila siku wakati Yeye anataka kukutana nasi katika Ekaristi, katika Neno lake, katika kaka na katika dada hasa wale wenye uhitaji zaidi.”
Baba Mtakatifu vile vile katika tafakari hii amebainisha, kwamba, kwa namna ya pekee katika majuma haya, tuache tujiandae kwa uangalifu katika nyumba ya moyo, ili iwe nadhifu na ya ukaribishaji wa wageni. Na kiukweli, kuwa kidete kunamaanisha kuweka moyo wako tayari. Ni mtazamo wa mlinzi, ambaye usiku hajiruhusu kujaribiwa na uchovu, halali, bali anabaki macho akingojea mwanga unaokuja. Bwana ndiye nuru yetu na ni jambo zuri kuutayarisha moyo wa kumkaribisha kwa sala na kumkaribisha kwa upendo, ambayo ni matayarisho mawili ambayo, kwa mfano, yanamfanya ahisi furaha. Katika pendekezo hilo, wanasimulia kuwa Mtakatifu Martino wa Tour, mwanaume wa sala baada ya kukata na kumpatia nusu ya joho lake maskini aliota ndoto ya Yesu akiwa amevaa sehemu hiyo ya joho lake alilokuwa ametoa zawadi. Na tazama ndiyo ratiba nzuri kwa ajili ya Majilio. Kukutana na Yesu anayekuja katika kila kaka na dada ambaye anahitaji sisi na kushirikiana nao kile ambacho tuweza kama vile kusikiliza, kutoa muda na msaada wa dhati.
Kwa kuhitimisha, Baba Mtakatifu amebainisha kwamba ni vema leo hii tujiulize jinsi gani ya kuandaa moyo wa kukaribisha kwa ajili ya Bwana. Tunaweza kufanya hivyo kwa kukaribia Msamaha wake, Neno lake, Meza yake, huku tukitafuta nafasi ya maombi, kwa kumkaribisha kwa wale wanaohitaji. Tutaweze kuwa na subira bila kulalamika mara kwa mara, huku tukikesha mioyo yetu, yaani, kumtamani, kuwa kidete na tayari, kwa subira ya kukutana Naye. Bikira Maria, mwanamke wa subira, atusaidie kumpokea Mwanae anayekuja.” Inahitimisha Tafakari ya Baba Mtakatifu iliyosomwa na Monsinyo Paolo Braida.