Papa:Baraka za samu ya Mtoto Yesu na kuombea watoto
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Mara baada ya Tafakari, sala ya Malaika wa Bwana, kwa waamini na mahujaji wengi sana katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, Baba Mtakatifu Francisko ameanza ameeleza juu ya kutangaza kwa Mwenyeheri Kardinali Eduardo Pironio, katika madhabahu ya Mama Yetu wa Luján, nchini Argentina. Mwenyeheri mpya amemfafanua kama: “mchungaji mnyenyekevu na mwenye bidii, shuhuda wa matumaini, mtetezi wa maskini. Alishirikiana na Mtakatifu Yohane Paulo II katika kuwahamaisha Walei na katika kuanza Maadhimisho ya Siku za Vijana Duniani. Na mfano wake utusaidie kuwa Kanisa linalotoka nje, ambalo linakuwa msindikizaji wa kusafiri kwa kila mtu, hasa wale walio dhaifu zaidi.” Baada ya kusema hayo, Baba Mtakatifu ameongeza kuomba wampigie makofi mwenyeheri mpya!
Baba Mtakatifu ametoa salamu kwa wote, kwa familia, vikundi vya parokia na vyama, vya kitume ambao wametoka Roma, Italia na sehemu nyingi za dunia. Hasa, amewasalimu mahujaji kutoka Marekani na Poland; waamini wa Mormanno, Acilia na Viterbo. Papa amesalimia watoto wapendwa na vijana kutoka katika vikundi mbali mbali na shule za Roma, ambao wameleta sanamu za Mtoto Yesu ili kubarikiwa. Amewabaki kwa kufanya ishara ya Msalaba. Na katika kubariki mtoto Yesu kwa kila mmoja aliyeleta, Papa amewaomba wasali mbele ya pamho kwa ajili aua watoto ambao watakuwa na Noeli ngumu, katika maeneo ya vita, katika kambi za wakimbizi, katika hali ya umaskini mkubwa. Asante kwa hilio na Noeli njema kwenu na familia zenu! Ameomba wapigiwe makofi watoto. Hatimaye amewatakia Dominika Njema na tafadhali wasisahau kusali kwa ajili yake. Amewatakia mlo mwema na kwaheri ya kuonana.