Papa:Kanisa linajifunza kushukuru na kutumaini kutoka kwa Bikira Maria

Kiukweli shukrani za kidunia na tumaini la kidunia ni za kijujuu,zinakosa jambo muhimu la uhusiano na Mungu pamoja na ndugu.Shukrani,matumaini na maandalizi ya 2025 ni maneno yaliyosikika katika Tafakari ya Masifu ya Jioni ya Siku Kuu ya Bikira Maria Mama wa Mungu katika kuhitimisha mwaka 2023 na kuingia mwaka mpya 2024.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika mahubiri ya Baba Mtakatifu Francisko Francisko wakati wa Masifu ya Kwanza ya Siku Kuu ya Bikira Maria Mama wa Mungu na kusali Sala ta Te deum yaani ya Kushukuru Mungu kwa kufunga mwaka yaliyofanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, jioni tarehe 31 Desemba 2023, kwa kuudhuriwa na waamini 6,500 kulingana na taarifa iliyotolewa,  Baba Mtakatifu amesisitiza  kuonja mwelekeo wa shukrani na matumaini: si katika mtazamo wa kidunia, lakini katika ule muhimu wa uhusiano na Mungu na ndugu. Kwa kutazama Jubilei ijayo ya 2025, anatumai kuwa Roma itakuwa ishara ya matumaini kwa wale wanaoishi huko na kwa wale wanaoitembelea. Baba Mtakatifu akianza mahubri yake amesema “Imani inaturuhusu kuishi muda huu kwa namna tofauti kulingana na mantiki za kidunia. Imani katika Yesu Kristo, Mungu aliyefanyika Mwili, kwa kuzaliwa na Bikira Maria anatoa namna mpya ya kuhisi wakati na maisha. Ninaweza kuyafupisha kwa maneno mawili: shukrani na matumaini.”

Papa Francisko katika Te  Deum 31 Desemba 2023
Papa Francisko katika Te Deum 31 Desemba 2023

Baba Mtakatifu amesema mmoja anaweza kujiuliza: lakini si kile ambacho wanafanya wote jioni ya mwisho wa mwaka? Wote wanashukuru, wote wanatumaini, waamini au wasio amini.”Labda inawezekana kuwa hivyo au labda ndivyo hivyo! Lakini kiukweli, shukran za kidunia, tumaini la kidunia ni za kiju juu, zinakosa jambo muhimu ambalo ni lile la uhusiano na aliye juu na kwa wengine, na Mungu pamoja na ndugu. Wamegandamizwa na ubinafsi, juu ya maslahi yao, na hivyo hawana pumzi, hawawezi kwenda zaidi ya kuridhika na matumaini. Badala yake, katika Liturujia hii, ambayo inahitimishwa na wimbo mkuu wa Te Deum laudamus, unaweza kupumua hali tofauti kabisa: ile ya sifa, ya mshangao, ile ya shukrani. Na hii haifanyiki kwa sababu ya ukuu wa Basilika, sio kwa sababu ya taa na nyimbo - vitu hivi ni matokeo -, lakini kwa sababu ya Fumbo ambalo antifoni ya zaburi ya kwanza ilionesha hivi: "Mabadilishano ya ajabu! Muumba alichukua nafsi na mwili, alizaliwa na bikira; […] anatupatia  umungu wake.” Ubadilishanaji huu wa ajabu.”

Masifu ya Jioni na Te Deum
Masifu ya Jioni na Te Deum

Baba Mtakatifu akiendelea amsema “Liturujia inatuwezesha kuingia katika hisia za Kanisa; na Kanisa, kwa kusema, linajifunza kutoka kwa Mama Bikira. Hebu tufikirie jinsi shukrani inavyopaswa kuwa katika moyo wa Maria alipomtazama Yesu aliyezaliwa karibuni. Ni uzoefu ambao mama pekee anaweza kuwa nao, na bado ndani yake, katika Mama wa Mungu, ana kina cha pekee, kisichoweza kulinganishwa. Maria anajua, peke yake pamoja na Yosefu, mahali ambapo Mtoto huyo anatoka. Hata hivyo yuko pale, anapumua, analia, anahitaji kula, kufunikwa, na kutunzwa. Fumbo linatoa nafasi kwa shukrani, ambayo inajitokeza katika kutafakari kwa zawadi, kwa bure, huku kukiwa na wasiwasi wa kuwa na kuonekana. Kanisa linajifunza kutoa shukrani kutoka kwa Mama Bikira. Na pia lijifunze matumaini. Mtu anaweza kufikiri kwamba Mungu alimchagua Maria wa Nazareti, kwa sababu aliona tumaini lake mwenyewe likiakisiwa moyoni mwake. Kile ambacho  alikuwa Yeye mwenyewe amemwingiza ndani yake kwa Roho wake. Maria daima amejawa na upendo, amejaa neema, na kwa sababu hiyo pia amejazwa na uaminifu na matumaini.

Masifu ya jioni na  Te deum 31.12.2023
Masifu ya jioni na Te deum 31.12.2023

Aidha Papa alisisitza kua kuhusu hiyo ya Maria na Kanisa si matumaini, ni kitu kingine: ni imani katika Mungu mwaminifu kwa ahadi zake (taz. Luka 1:55); na imani hii inachukua namna ya matumaini katika mwelekeo wa wakati, tunaweza kusema "njiani". Mkristo, kama Maria, ni msafiri wa matumaini. Na hii itakuwa mada ya Jubilei ya 2025: "Mahujaji wa Matumaini". Baba Mtakatifu amesisitiza kuwa, tunaweza kujiuliza: Je, Roma inajiandaa kuwa “mji wa matumaini” katika Mwaka Mtakatifu? Sote tunajua kuwa shirika moja la maandalizi ya  Jubilei limekuwa likiendelea kwa muda. Lakini tunaelewa vizuri kwamba, kwa mtazamo tunaochukua hapa, sio hasa kuhusu hilo; bali ni ushuhuda wa jumuiya ya kikanisa na kiraia; ushuhuda ambao, zaidi ya katika matukio, unajumuisha mtindo wa maisha, katika ubora wa kimaadili na kiroho wa kuishi pamoja. Na kwa hivyo swali linaweza kutengenezwa hivi: je, tunafanya kazi, kila mmoja katika eneo letu, ili jiji hili liwe ishara ya tumaini kwa wale wanaoishi huko na kwa wale wanaotembelea? Mfano. Kuingia kwenye Uwanja wa Mtakatifu Petro na kuona kwamba, katika kukumbatia nguzo, watu wa kila taifa, kila utamaduni na dini wanatembea kwa uhuru na utulivu, ni mang’amuzi yanayotia matumaini; lakini ni muhimu kuthibitishwa na ukaribisho mzuri wakati wa ziara katika Basilika, na vile vile katika huduma za habari na maulizo.

Masifu ya jioni na Te Deum 31 .12.2023
Masifu ya jioni na Te Deum 31 .12.2023

Mfano mwingine:uzuri wa  kituo cha kihistoria cha Roma ni ya kudumu na ya ulimwengu wote; lakini watu wazee au watu wenye ulemavu wa magari lazima pia waweze kufurahia; na "uzuri mkubwa" lazima ufanane na mapambo rahisi na utendaji wa kawaida katika maeneo na hali ya maisha ya kawaida, katika maisha ya siku za juma. Kwa sababu jiji ambalo linaweza kuishi zaidi kwa raia wake pia linakaribishwa zaidi kwa kila mtu. Papa Francisko amesisisitza kuwa , safari ya hija, hasa ikiwa ya lazima, inahitaji maandalizi mazuri. Hii ndiyo sababu mwaka ujao, unaotangulia Jubilei, umejitolea kwa ajili ya maombi. Mwaka mzima wa maombi. Na ni mwalimu gani bora tungeweza kuwa naye kuliko Mama yetu Mtakatifu? Hebu tujiweke katika shule yake: tujifunze kutoka kwake kuishi kila siku, kila dakika, kila kazi yenye mtazamo wa ndani ilimgeukia Yesu.Furaha na huzuni, kuridhika na matatizo. Yote katika uwepo na kwa neema ya  Bwana Yesu. Wote kwa shukrani na matumaini.” Papa Francisko amehitimisha.

Tafakari ya Papa wakati wa masifu ya I na Tedeum tarehe 31 Desemba 2023
31 December 2023, 18:00