Papa kwa wafanyakazi wa Vatican:Mungu anajificha katika udogo wa Mtoto anayezaliwa
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Hata mwaka huu, Noeli inatufanya tukutane kwa ajili ya kubadilishana matashi mema. Asante kwa kufika kwenu, hata na familia zenu. Ndivyo Baba Mtakatifu ameanza kuwakaribisha, wafanyakazi wa Vatican wote wakiwa na familia zao ndugu na marafiki, katika ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican, Alhamisi tarehe 21 Desemba 2023. Baba Mtakatifu katika hotuba hiyo amesema kwa kutafakari pamoja Fumbo la Kuzaliwa kwa Yesu ni vizuri kuweza kuona mtindo wa Mungu ambaye sio mkubwa au wa kelele, lakini kinyume chake ni mtindo wa kujificha, na kwa udogo. Ni maneno muhimu ya kujificha na udogo. Haya yanatuonesha sehemu ya unyenyekevu wa Mungu ambao hauji kwetu ili kutuvuta katika ukuu wake, au kwa kupendekeza kwa sifa, lakini kwa kuwepo kwa namna ya kawaida zaidi iwezekanavyo, na kujifanya mmoja wetu.
Kujificha na udogo. Mungu anajificha katika udogo wa Mtoto anayezaliwa, katika wenzi wawili wa ndoa, Maria na Yosefu, ambao hawapo chini ya mataa, katika umaskini wa hori la wanyama, kwa sababu hapakuwapo na nafasi kwao katika nyumba za wageni. Hizi ndizo ishara za Mwana wa Mungu ambaye baadaye atajiwakilisha ulimwenguni kama mbegu ndogo inayokufa ikiwa imefichika kwenye udongo ili kuzaa matunda. Yeye ni Mungu wa watoto wadogo, Mungu wa mwisho na pamoja Naye, sote tunajifunza njia ya kufuata ili kuingia katika Ufalme wa Mungu. Yeye ni Mungu wa wadogo na walio wa mwisho na kwa Yeye sisi sote tunajifunza njia ya kufuata kuingia katika Ufalme wa Mungu: si kwa udini unaoneshwa na wa kijujuu, lakini kugeuka kuwa wadogo kama watoto. Baba Mtakatifu Francisko aidha amewaeleza jinsi ambavyo wao wanaojua vema maneno hayo mawili. Kazi yao mjini Vatican inajikita zaidi katika kificho cha kila siku, mara nyingi kwa kupeleka mbele mambo ambayo wanaweza kufikiria hayana maana na kiunyume chake yanachangia kutoa huduma kwa Kanisa na kwa Jamii.
Baba Mtakatifu amewashukuru kwa hili. Na kuwatakia kwamba wanaweza kuendelea na kazi zao kwa roho ya shukrani, kwa utulivu na unyenyekevu na kutoka hapo katika uhusiano na wafanyakazi wenzao, kike na kiume wanatoa ushuhuda wa kikristo. “Hata hapa, au tuseme, kwanza kabisa hapa, kuna hitaji la kweli? Tazameni uficho na udogo wa Yesu pangoni; Tazameni unyenyekevu wa pango la kuzaliwa mlilofanya nyumbani; na muwe na uhakika kwamba wema, hata wakati umefichwa na hauonekani, hukua bila kufanya kelele yoyote. Ni vizuri, hukua bila kupiga kelele yoyote, huzidisha bila kutarajia na kueneza harufu ya furaha. Wasisahau hili: “uzuri unaokua bila kufanya kelele yoyote na hutoa amani hiyo furaha hiyo ya moyo ambayo ni nzuri sana.
Baba Mtakatifu amependa kuwatakia heri ya mtindo huo wa uficho na udogo-kwa familia zao na watoto wao. Leo hii tunaishi katika wakati ambao wakati mwingine kuonekana kumekuwa wasiwasi wa kuonekana, kila mtu anajaribu kujionesha. "Ni wakati wa "make-up": kila mtu hujipodoa, sio tu usoni, lakini hujipodoa kwenye nafsi zao na hii ni mbaya, na wanajaribu kujiweka kwenye maonesho. Kuonekana”, hasa kupitia ile inayoitwa mitandao ya kijamii. Ni sawa na kutaka glasi za vioo vya thamani bila kuwa na wasiwasi kuhusu ikiwa divai ni nzuri.” Divai nzuri hunyweka kwenye glasi ya kawaida. Lakini katika kuonekana kwa familia na barakoa hazihesabiki bali katika familia kila kitu kinajulikana au kwa hali yoyote hudumu muda mfupi; cha muhimu ni kwamba divai nzuri ya upendo, huruma na kuhurumiana haikosekani. Na hii ndiyo mtindo wa Mungu wa "ukaribu, huruma na upole." Na tunajua vizuri kuwa upendo haupigi kelele. Tunauishi katika uficho na udogo wa ishara za kila siku, kwa umakini ambao tunajua jinsi ya kubadilishana.
Papa amependa kwa hiyo kuwatakia matashi mema ya kuwa makini, katika nyumba zao na katika familia zao, ya kuwa na mambo madogo madogo ya kila siku, ishara ndogo za shukrani na umainifu wa kutunzana. “Kwa kutazama pango, tunaweza kufikiri umakini na huruma ya Maria na Yosefu kwa kwa mtoto ambaye amezaliwa. Papa amesisitiza kuwa ndiyo matashi na mtindo huo anaowatakia wote. Kwa kuhitimisha, amewaatakia Noeli takatifu njema. Ni matashi mema ambayo anayapanua hata kwa watoto wao na vijana, kwa familia zao, wazee ambao wanaishi nao, hasa wagonjwa wapendwa. Tufungue mioyo kwa furaha: Bwana anakuja katikati yetu. Heri na Noeli nyote. Na tafahadhali msali kwa ajili yangu.”