2023.12.07 Papa amekutana na wajumbe wa Harakati ya Wafocolari. 2023.12.07 Papa amekutana na wajumbe wa Harakati ya Wafocolari.  (Vatican Media)

Papa kwa Wafocolari:ukomavu wa kikanisa,uaminifu wa karama na kujitolea kwa amani

Na siku zote napenda kukumbuka kwamba ninyi mko karibu sana na siri ya Mungu,kwa siri nne za Mungu.Yaani mambo manne ambayo hayazekani kuyaelewa:hatujui ni mashirika ngapi ya watawa;Wajesuiti wanavyofikiri;Wasalesiansi wana pesa kiasi gani;na Wafocolari wanacheka nini! Ni Ucheshi wa Papa alioutoa kwa Harakati ya Wafocolari mjini Vatican,Desemba 7 wakisheherekea miaka 80 ya kuanzishwa Harakati hiyo.

Na Angella Rwezaula - Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Harakati ya Wafocolari mjini Vatican, Ahamisi tarehe 7 Desemba 2023 katika fursa ya Miaka 80 tangu kuanzishwa kwake. Katika hotuba yake, Baba Mtakatifu amesema ni tukio linalokwenda sambamba na siku ya Mtumishi wa Mungu Chiara Lubich alipoama kujiweka wakfu moja kwa moja kwa Bwana. “Kutokana na msukumo alioupokea katika mazingira ya kawaida kabisa ya maisha - alipokuwa anakwenda kufanya manunuzi kwa ajili ya familia yake, kitendo kikubwa cha mchango kwa Mungu kiliibuka, kama itikio la mwito wake ambao alihisi kuwa mtamu na wenye nguvu moyoni mwake. Ilikuwa mnamo tarehe 7 Desemba 1943, huko Trento, katikati ya vita; moja kwa moja katika mkesha wa Shereza za Bikira maria Mkingiwa dhambi ya Asili, "ndiyo" ya Maria ikawa "ndiyo" ya Chiara, ikizalisha wimbi la hali ya kiroho ambalo lilienea ulimwenguni kote, kumwambia kila mtu kwamba ni vizuri kuishi Injili kwa neno moja rahisi: Umoja.

Papa amekutana na wajumbe wa Harakati ya Wafocolari
Papa amekutana na wajumbe wa Harakati ya Wafocolari

Baba Mtakatifu amekazia kusema kuwa “katika miaka hii themanini, imesikia ujumbe huo katikati ya vijana katika jumuiya, familia, na watu waliowekwa wakfu, mapadre, na maaskofu, na hata katika mazingira mengine ya kijamii, kutoka ulimwengu wa shule hadi wa uchumi, wa sanaa hadi utamaduni wa mawasiliano na vyombo vya habari, na kwa namna ya pekee katika mazingira ya kiekumene na mazungumzo ya kidini. “Kwa hiyo mmekuwa chombo hai cha kazi kubwa, mipango na zaidi ya yote "kuzaliwa upya", uongofu, miito, maisha yaliyotolewa kwa Kristo na kwa ndugu zetu. Leo tunataka kumshukuru Mungu kwa haya yote.” Mnamo Februari 2021 kwa kuzungumza katika Mkutano wao Mkuu, Baba Mtakatifu alisisitiza tabia tatu muhimu kwa ajili ya safari yao yaani kuishi kwa umaninifu unaoendeleza karama, kuchagua vipindi vya mgogoro kama fursa ya ukomavu, na kujimwilisha kwa makini na ukweli wa kiroho (Hotuba 6 Februari 2021). Katika hili Papa amependa kuwakumbusha tena kwa ili wahisi na kuyahasisha katika misimamo mitatu: “ukomavu wa kikanisa, uaminifu kwa karama na kujitolea kwa amani.”

Wajumbe wa Wafocolari
Wajumbe wa Wafocolari


Kuhusiana na ya kwanza, Papa amewaalika wafanye kazi pamoja kwa sababu daima waweze kutimiza ndoto ya Kanisa la kisinodi kamili na kimisionari, kuanzia na jumuiya zao kwa kusaidia kufanya mtindo mmoja wa ushirikishwaji na uwajibikaji hata kwa ngazi ya serikali. Katika muktadha wa pili kuhusu uaminifu kwa karama, amewakumbusha baadhi ya maneno ya mwanzishili wao kuwa: “Waachie Injili tu kwa wale wanaowafuata. Ikiwa mtafanya hivi ubora ya umoja utabaki [...]. Kilichosalia na kitabaki daima ni Injili, ambayo haisumbuki na uchakavu wa wakati"(C. LUBICH, in La Parola di Dio, Roma 2011, 112-113).“Panda umoja kwa kupeleka Injili, bila kupoteza kamwe kazi ya umwilisho ambayo Mungu anaendelea kuitekeleza ndani yetu na kandokando yetu kwa njia ya Roho wake, ili Yesu awe habari njema kwa kila mtu, pasipo mtu yeyote kutengwa, na " ili kila mtu awe kitu kimoja tu(Yh 17,21).

Wajumbe wa Harakari ya Wafocolari
Wajumbe wa Harakari ya Wafocolari


Na tatu kuhusu jitihada ya amani. Baba Mtakatifu amesema: “Baada ya milenia mbili ya Ukristo, kwa hakika, hamu ya umoja inaendelea kuchukua, hatua katika sehemu nyingi za dunia, namna ya kilio cha kuhuzunisha ambacho kinadai jibu. Chiara aliisikia wakati wa mkasa wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia, akaamua kujitolea maisha yake yote ili “agano la Yesu” litimie. Leo, hii kwa bahati mbaya, dunia bado imesambaratishwa na migogoro mingi na inaendelea kuhitaji mafundi wa udugu na amani kati ya watu na mataifa. Hata hivyo Baba Mtakatifu amependa kuwachekesha kwamba: “Na siku zote ninapenda kukumbuka kwamba ninyi mko karibu sana na siri ya Mungu, kwa siri nne za Mungu.Yaani mambo manne ambayo hayazekani kuyaelewa:hatujui ni mashirika ngapi ya watawa;Wajesuiti wanavyofikiri;Wasalesiansi wana pesa kiasi gani; na Wafocolari wanacheka nini...!”

Wajumbe wa Harakati ya Wafocolari na Papa
Wajumbe wa Harakati ya Wafocolari na Papa

Kabla ya kuhitimisha, Baba Mtakatifu aidha amependa “kutoa mwaliko wa mwisho kwao, unaofaa katika wakati huu wa Majilio: ule wa kukesha. Hatari ya ulimwengu wa kiroho daima hujificha.” Kwa hivyo ni muhimu kwamba wao pia wajue jinsi ya kuguswa na uamuzi, mshikamano na uhalisia. Tukumbuke kwamba kutopatana kati ya kile tunachosema sisi na kile tulicho kweli ni kupinga ushahidi mbaya zaidi tunaweza kutoa kwa wengine. Baba Mtakatifu amehitimisha kwa kusema kuwa “kama alivyowakumbusha kuwa wao ni “Kazi ya Maria ni Yeye ambaye aliwasindikiza katika miaka hii 80 na wanajua vizuri kuwa hataacha kamwe kufanya hivyo. Kwa hiyo Bikira maria wa Nazareti awe kisima cha faraja na nguvu, kwa sababu wanaweza kuwa mitume wa umoja katika huduma ya kanisa na Ubinadamu. Amewashukuru kwa kile ambacho wanafanya. Amomba wanedelee na imani katika safari yao. Na kuwabariki.

Hotuba ya Papa kwa Harakati ya Wafocolari

 

07 December 2023, 14:05