Tafuta

2023.12.09 Papa alikutana na Wawakilishii wa Zawadi kwa ajili ya Pango na Mti wa Siku Kuu ya Kuzaliwa kwa Bwana katika Uwanja wa Mtakatifu Petro. 2023.12.09 Papa alikutana na Wawakilishii wa Zawadi kwa ajili ya Pango na Mti wa Siku Kuu ya Kuzaliwa kwa Bwana katika Uwanja wa Mtakatifu Petro.   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa:mbele ya Pango la Kuzaliwa na himizo la kufikiri janga la Nchi Takatifu

Papa alikutana mjini Vatican na wajumbe kutoka maeneo ya asili ya mti wa Noeli na Pango la kuzaliwa kwa Bwana ambapo mwaka huu ni ukumbusho utengenezaji wa Pango la kwanza lilioundwa miaka 800 iliyopita na Mtakatifu Francis:"Kutoka Uwanja wa Mtakatifu Petro tufikirie Greccio,ambayo pia iturudishe Bethlehemu”

Na Angella Rwezaula - Vatican.

Uwakilishi wa Matengenezo ya Pango la Kuzaliwa kwa Yesu lililoundwa katika eneo la Rieti kwa mara ya kwanza. Mti uliochaguliwa kutengeneza mapambo ya  Noeli ni kutoka katika Bonde la Mairahuko jimbo la Cuneo nchini Italia. Hayo ndiyo yaliyo katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, ambapo Wawakilishi wa matengenezo hayo walikutana na Baba Mtakatifu Francisko, Jumamosi tarehe 10 Desemba 2023. Kwa mara ya kwanza, Pango la kwanza lilitengenezwa katika Bonde la Rieti Mkoa wa Lazio, mnamo 1223 na Mtakatifu Francis wa Assisi. Papa Francisko katika hotuba yake alisema, jinsi ambavyo Mtakatifu huyo alikumbuka safari aliyoifanya hadi Nchi Takatifu na kwamba ilikuwa bado hai na pango la Greccio lilimkumbusha mandhari ya Bethlehemu. Kwa hiyo, “ aliomba kuwakilisha mandhari ya Noeli katika kijiji hicho kidogo kwa sababu ndugu wengi walikuja kutoka sehemu mbalimbali na wanaume na wanawake pia walifika kutoka katika nyumba za mashambani katika eneo hilo, na kujenga mandhari illiyo hai ya kuzaliwa.

Papa wakati wa otuba kwa wawakilishi wa Mapambo ya Noeli katika Mji wa Vatican
Papa wakati wa otuba kwa wawakilishi wa Mapambo ya Noeli katika Mji wa Vatican

Na katika muktadha huo ndili  ilizaliwa mapokeo ya tukio la kuzaliwa kama tunavyoweza kuelewa Papa alisisitza. Mwaka huu 2023, kwa hiyo “ kutoka Uwanja wa Mtakatifu Petro, tufikirie Greccio, ambayo kwa hiyo inatuelekeza huko Bethlehemu. Na tunapomtafakari Yesu, Mungu alimuumba mwanadamu, mdogo, maskini, asiye na ulinzi, kwamba hatuwezi kuacha kufikiria janga ambayo wakazi wa Nchi Takatifu wanapitia, ili kuwaonesha hawa kaka na dada zetu, hasa kwa watoto na wazazi wao ukaribu wetu na msaada wetu wa kiroho. Hawa ndio wanaolipa gharama halisi ya vita.”

Ukimya na maombi

Papa alisisitiza kwamba “mbele ya kila tukio la kuzaliwa kwa Kristo, hata zile zilizotengenezwa nyumbani kwetu, tunakumbuka kile kilichotokea Bethlehemu zaidi ya miaka elfu mbili iliyopita.”  Na hii “inapaswa kuamsha ndani yetu hamu ya ukimya na sala, katika maisha yetu ya kila siku ambayo mara nyingi huwa na shughuli nyingi. Kunyamaza, kuweza kusikiliza kile ambacho Yesu atuambia kutoka katika pango hilo na umoja wa holi. Sala, ili kuonesha mshangao wenye shukrani, huruma, labda machozi ambayo tukio la Kuzaliwa kwa Yesu hutuamsha ndani yetu. Na katika haya yote Maria ndiye kielelezo chetu: hasemi chochote, lakini anatafakari na kuabudu.”

Mti huo unatukumbusha umuhimu wa kutunza mazingira

Katika Uwanja wa Mtakatifu Petro  karibu na eneo la Pango la kuzaliwa kwa Yesu, kuna mti wenye urefu wa mita 28.Vifaa vya mapambo vimetolewa na Caritas. Ni utajiri mzima katika tambarare, wa kulinda wale kukua katika milima ya juu. Hili pia ni chaguo linalotufanya tutafakari, tukionesha umuhimu wa kutunza nyumba yetu ya pamoja: Ni ishara ndogo ambayo ni muhimu katika uongofu wa kiikolojia, ishara za heshima na shukrani kwa zawadi za Mungu. Mkutano wa Papa Francisko na wajumbe hao ulitangulia tukio lililokuwa likisubiriwa kwa hamu kubwa lililopangwa kufanyika jioni. Yaani Uzinduzi wa kiutamaduni wa eneo la Kuzaliwa kwa Yesu na kuwasha mti wa Noeli katika Uwanja wa Mtakatifu Petro kufanyika saa kumi na moja jioni. Sherehe hizo zitaongozwa na Kadinali Fernando Vérgez Alzaga, rais tawala wa Mji wa Vatican.

Hotuba ya Papa kwa Watengenezaji Pango na Mti wa Noeli

 

09 December 2023, 15:03