Jeshi la Israeli lilishambulia  Parokia ya Familia Takatifu huko Gaza. Jeshi la Israeli lilishambulia Parokia ya Familia Takatifu huko Gaza.  (ANSA)

Papa:“Raia wasio na silaha waliuawa huko Gaza,ni vita,ni ugaidi"

Baba Mtakatififu ametoa taarifa juu ya kilichotokea huko Gaza kwamba:"Ilitokea hata ndani ya Parokia ya Familia Takatifu,ambapo hakuna magaidi,lakini ni familia,watoto, wagonjwa na walemavu,watawa.Mama na binti yake waliuawa."

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko wakati wa salamu zake mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana, Dominika 17 Desemba 2023 amerejea kuombea amani katika Nchi Takatifu, hasa baada ya kupigwa risasi na jeshi la Israel nje ya Parokia ya Familia Takatifu katika Mji wa Gaza, unoteswa na kutamka majina ya wahanga walioshutikizwa katika  shambulio hilo baya lililotokea amesema “hakuna magaidi, lakini  ni familia, watoto, wagonjwa na walemavu, watawa. Mama na binti yake waliuawa.”

Baba Mtakatifu Francisko kwa hiyo amesema: “Na tusiwasahau kaka na dada zetu wanaoteseka kwa vita, huko Ukraine, Palestina na Israel na maeneo mengine yenye migogoro. Kukaribia kwa siku kuu ya Noeli kuimarishe dhamira ya kufungua njia za amani.” kwa kuongezea Papa amesema:  “Ninaendelea kupokea habari nzito na zenye uchungu kutoka Gaza. Raia wasio na ulinzi  wanakabiliwa na milipuko ya mabomu na risasi. Na hii ilifanyika hata ndani ya eneo la Parokia ya Familia Takatifu, ambapo hakuna magaidi, japokuwa ni familia, watoto, wagonjwa na walemavu,na watawa.”


Baba Mtakatifu ameongeza kusema: “Bi Nahida Khalil Anton, Mama na binti yake, Samar Kamal Anton, waliuawa na watu wengine kujeruhiwa na wapiga risasi, wakati wakienda kuoga bafuni. Nyumba ya Masista wa Mama Teresa iliharibika na jenereta lao lilipigwa. Mwingine anasema: “Ni ugaidi, ni vita.” Ndiyo, ni vita, ni ugaidi. Hii ndiyo sababu Maandiko yanasema kwamba: “Mungu anakomesha vita... avunja pinde na kuvunja mikuki” (Zab 46:9). Tuombe amani  kwa Bwana.”

17 December 2023, 16:31