Papa:Turudi katika jangwa na tukae kimya kwa ajili ye Neno

Jangwa na sauti ni maneno mawili yaliyoongoza tafakari ya Papa katika Dominika ya Pili ya Majilio tarehe 10 Desemba 2023,akiwageukia waamini na mahujaji waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican.“Ikiwa hatujuhi kunyamaza ni viguu kuwa na jambo zuri la kusema.Ukimya wa kina zaidi ni neno lenye nguvu.”

Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko, akiwa katika dirisha la Nyumba ya kitume mjini Vatican kwa kuwageukia waamini na mahujaji waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, Mjini Vatican, Dominika tarehe 10 Desemba 2023, kabla ya Sala ya Malaika wa Bwana, ameanza kusema kuwa: Katika Dominika ya Pili ya Majilio, Injili inaelezea kwetu Yohane Mbatizaji, mtangulizi wa Yesu (rej. Mk 1,1-8) na anamfafanua kama “sauti iliayo jangwani(Mk 1,3). Jangwa ni mhali patupu,mahahali ambapo hakuna makutano, na sauti, kuwa katikati kwa ajili ya kuzungumza utafikiri ni picha mbili zinazopingana, lakini kwa upande wa Yohane Mbatizaji zinaunganika. Baba Baba Mtakatifu ameendelea kwana na Jangwa. Yohane anahubiria pale karibu na mto. Yohane alikuwa karibu na mahali ambapo watu wake, kwa karne nyingi kabla, walikuwa wameingia katika Nchi ya Ahadi (Gs 3,1-17). Kwa kufanya hivyo ilikuwa ni kama kusema kuwa: ili kuweza kusikiliza Mungu tunapaswa kurudi katika mahali ambapo kwa miaka 40, Yeye alisindikiza, alilinda na kuelimisha watu wake katika jangwa. Eneo hili ni mahali pa ukimya na kuwa na mambo muhimu tu, mahali ambapo huwezi kuruhusu kuwa na mambo yasiyo na maana, lakini inahitaji kujikita kwa undani kwa kile ambacho ni muhimu ili kuweza kuishi.

Sala ya malaika wa bwana 10 Desemba 2023
Sala ya malaika wa bwana 10 Desemba 2023

Papap Francisko amekazia kusema kuwa suala hili ni mwito wa leo hii, ili kuweza kuendelea katika safari ya maisha ni lazima kujivua yale yaliyo ya ziada, kwa sababu kuishi vizuri haina maana ya kujaza mambo yasiyo na maana, badala yake ni kuondoa yale ya ziada, ili kuchimba kwa kina ndani yake, ili kupokea kile ambacho ni muhimu mbele ya Mungu. Ni kwa kupitia ukimya na sala tu, tunatengeneza nafasi ya Yesu ambaye ni Neno la Baba, na tutajua namna ya kujikomboa dhidi ya uchafuzi wa maneno yasiyofaa na masengenyo. Ukimya na utulivu, katika maneno, katika matumizi kwenye mambo, katika vyombo vya habari na mitandao ya kjamii, sio tu kujinyima au fadhila, lakini ni mambo muhimu ya maisha ya Kikristo.

Angelus ya Papa 10 Desemba 2023
Angelus ya Papa 10 Desemba 2023

Baba Mtakatifu Francisko katika picha ya pili amelezea Sauti. Hiyo ni chombo ambacho tunaonesha kile ambacho tunafikiria na tunabeba ndani ya mioyo yetu. Tunaendelea kwa hiyo kwamba ukimya umefungamana sana kwa sababu unaelezea kile ambacho kimekomaa ndani, kutokana na kusikiliza kile ambacho Roho anapendekeza. Ikiwa hatujuhi kunyamaza, ni viguu kuwa na jambo zuri la kusema, wakati huo huo ukimya wa makini zaidi, ni neno lenye nguvu. Sauti yake inahusishwa na ukweli wa uzoefu wake na uwazi wa moyo wake. Baba Mtakatifu Francisko amesisitiza kuwa tunaweza kujiuliza kwamba: Je Kimya ina nafasi gani katika siku zangu? Ni ukimya mtupu, labda wa kukandamizi au ni nafasi ya kusikiliza, ya sala na mahali pa kulinda moyo? Je Maisha yangu ni ya kiasi au yamejaa mambo ya kupita kiasi? Hata kama kuna maana ya kwenda kinyume na dunia, Papa ameongeza kusema kuwa: “tuthamanishe ukimya wa kiasi na kusikiliza.” Papa amehitimisha akisema kwamba: “Bikira Maria, wa ukimya, atusaidie kupenda jangwa, ili kugeuka kuwa sauti aminifu ambayo inatangaza Mwanae ajayekuja.”

Tafakari ya Papa Domini ya II ya Majilio

 

10 December 2023, 15:44