Baba Mtakatifu katika katekesi yake, Jumatano tarehe 24 Januari 2024 amejikita katika uchoyo kama mzizi wa dhambi. Uchoyo ni tamaa kubwa na ya ubinafsi kuhusu uchu wa mali, madaraka na chakula. Baba Mtakatifu katika katekesi yake, Jumatano tarehe 24 Januari 2024 amejikita katika uchoyo kama mzizi wa dhambi. Uchoyo ni tamaa kubwa na ya ubinafsi kuhusu uchu wa mali, madaraka na chakula.   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Katekesi Kuhusu Fadhila na Mizizi ya Dhambi: Uchoyo na Uchu wa Mali na Madaraka

Baba Mtakatifu Francisko katika katekesi yake, Jumatano tarehe 24 Januari 2024 amejikita katika uchoyo kama mzizi wa dhambi. Uchoyo ni tamaa kubwa na ya ubinafsi kuhusu uchu wa mali, madaraka na chakula. Na choyo na ubinafsi ni kati ya magonjwa yanayopekenyua kwa kiasi kikubwa: utu, heshima na haki msingi za binadamu. Uchoyo ni chanzo kikuu cha vita, migogoro na kinzani zinazotumia rasilimali kubwa kwa ajili ya masilahi ya watu wachache katika jamii.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S., Vatican.

Mababa wa Kanisa wanasema kwamba, fadhila ni tabia ya kawaida na imara ya kutenda mema. Yamruhusu mtu si kutenda mema tu bali kutoa kilicho chema kabisa cha nafsi yake. Mtu wa fadhila huelekea mema kwa hisi zake zote pamoja na nguvu za kiroho. Hutafuta mema na kuyachagua kwa matendo halisi. Kuna fadhila za kibinadamu ambayo ni hali thabiti, maelekeo imara, ukamilifu wa kawaida wa akili na utashi zinazotawala matendo ya binadamu, zinazoratibu harara na kuongoza mwenendo kufuata akili na imani. Zinawezesha raha, kujitawala na furaha katika kuishi maisha mema kimaadili. Fadhila adili hupatikana kwa juhudi za kibinadamu kuungana na upendo wa Mungu. Shabaha ya mtu mwenye fadhila ni kuwa kama Mungu. Kuna fadhila kuu ambazo hutenda kazi kama bawaba nazo ni: Busara, haki, nguvu, na kiasi. Rej. KKK. 1803-1803. Kuna fadhila tatu za Kimungu: imani, matumaini na mapendo. Ni katika muktadha huu, Baba Mtakatifu Francisko, Jumatano tarehe 27 Desemba 2023 ameanza mzunguko mpya wa Katekesi kuhusu fadhila na mizizi ya dhambi mambo msingi katika kuulinda moyo. Katika mzunguko huu wa Katekesi, Baba Mtakatifu amekwisha kuchambua kuhusu: Dhambi na vishawishi vya dhambi, ulafi pamoja na tamaa mbaya! Baba Mtakatifu katika katekesi yake, Jumatano tarehe 24 Januari 2024 amejikita katika uchoyo kama mzizi wa dhambi. Uchoyo ni tamaa kubwa na ya ubinafsi kuhusu uchu wa mali, madaraka na chakula. Na choyo na ubinafsi ni kati ya magonjwa yanayopekenyua kwa kiasi kikubwa: utu, heshima na haki msingi za binadamu. Uchoyo ni chanzo kikuu cha vita, migogoro na kinzani zinazotumia rasilimali kubwa kwa ajili ya masilahi ya watu wachache katika jamii.

Katekesi kuhusu fadhila na mizizi ya dhambi:uchoyo
Katekesi kuhusu fadhila na mizizi ya dhambi:uchoyo

Kuendelea na hatimaye, kushamiri kwa biashara ya silaha duniani ni matokeo ya uchoyo, ubinafsi, na uchu wa mali na madaraka. Uchu wa fedha, mali na madaraka unamfunga mtu kiasi cha kushindwa kuwa na ukarimu. Hii ni dhambi inayowapekenya watu wengi na inakita mizizi yake moyoni mwa mtu, uchu wa fedha unaweza kuwabwaga chini hata Wamonaki ambao kimsingi wameyafia mambo haya, lakini ikiwa kama waliridhika kuwa na wingi wa mali, kielelezo cha uchoyo na ubinafsi. Ili kuweza kuganga na hatimaye, kutibu ugonjwa huu ni vyema kukumbuka kwamba, baada ya kifo, mali zote za dunia zinabaki, mwanadamu kamwe hawezi kushuka na mali pamoja na utajiri wake kaburini na kwamba mwanadamu hapa duniani ni msafiri na wala hana makazi ya kudumu. Uchu wa fedha, mali na madaraka ni kielelezo cha woga dhidi ya fumbo la kifo. Umiliki wa mambo haya ni kama uhakika na usalama wa maisha. Baba Mtakatifu Francisko amewakumbusha waamini kuhusu mfano wa tajiri mpumbavu! “Kisha, nitajiambia, Ee nafsi yangu, una vitu vyema vingi ulivyojiwekea akiba kwa miaka mingi; pumzika basi, ule, unywe, ufurahi. Lakini Mungu akamwambia, “Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanataka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani? Ndivyo alivyo mtu ajiwekeaye nafsi yake akiba, asijitajirishe kwa Mungu.” Lk 12:19-21. Wezi tu ndio mara nyingi wanaweza kuwafundisha matajiri kujitajirisha kwa Mungu. Kristo Yesu aliwahubiria watu akiwataka kujiwekea hazina mbinguni: “Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba; bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi; kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako.” Mt 6:19-21.

Katekesi kuhusu fadhila na mizizi ya dhambi:uchoyo
Katekesi kuhusu fadhila na mizizi ya dhambi:uchoyo

Mababa wa Jangwani wanasema, wamonaki walikuwa na tabia ya kuwatafuta wezi na kuwapatia hata kile kidogo walichokuwa wamebakiza. Kwa bahati mbaya sana, matajiri wengi hawana uhuru tena wala muda wa kujipumzisha, daima wanakuwa ni watu wa hofu, kwa utajiri walioupata kwa jasho kubwa, unaweza kutoweka mara moja kama ndoto ya mchana. Kuwa na utajiri kwa wenyewe si dhambi bali huu ni wajibu unaopaswa kufanyiwa kazi. “Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.” 2Kor 8:9. Mali inaweza kuwa ni chanzo cha baraka, lakini kwa bahati mbaya kwa wengi imekuwa ni chanzo cha ukosefu wa furaha ya kweli. Kuna watu ni wachoyo hata kwa wagonjwa na jambo hili ni hatari sana kwa maisha anasema Baba Mtakatifu Francisko.

Mizizi ya Dhambi: Uchoyo
24 January 2024, 16:47