Tafuta

Maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 25 tangu kuanzishwa kwa Chama cha “Nolite Timere” yananogeshwa na kauli mbiu mbiu “Tunatoa matumaini ili kuanza upya” Maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 25 tangu kuanzishwa kwa Chama cha “Nolite Timere” yananogeshwa na kauli mbiu mbiu “Tunatoa matumaini ili kuanza upya”   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Mauaji ya Kimbari Nchini Rwanda 1994: Matumaini Kwa Yatima na Waathirika wa Mauaji ya Kimbari

Baba Mtakatifu Francisko amekazia umuhimu wa kumbukizi hii, ili kamwe watu wasiyasahau kamwe mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini Rwanda kunako mwaka 1994. Hiki ni kielelezo cha ushirikiano na mshikamano wa kidugu, kwani vita na biashara ya silaha ni mambo yanayowanyima watoto furaha ya maisha kwa kutoa huduma ya kiuchumi, kielelezo cha mshikamano na udugu wa kibinadamu unavuka mipaka ya umri, utaifa, utamaduni na hali ya mtu kijamii! Utu na Haki!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S., Vatican.

Chama cha “Nolite Timere” kilianzishwa kwa juhudi za Askofu mkuu Salvatore Pennacchio, aliyekuwa Balozi wa Vatican nchini Rwanda pamoja na Padre Tommaso Cuciniello kunako mwaka 1994, nchini Rwanda kwa ajili ya kuwasaidia watoto yatima waliokuwa wameathirika kutokana na mauaji ya kimbari nchini Rwanda. Huu pia ulikuwa ni mchango mkubwa uliotolewa na Mtakatifu Yohane Paulo II. Chama cha “Nolite Timere” kinaadhimisha kumbukizi ya Jubilei ya Miaka 25 ya uwepo na huduma kwa watoto yatima nchini Rwanda. Wajumbe wa Chama hiki, Jumamosi tarehe 27 Januari 2024 wamekutana na kuzungumza na Baba Mtakatifu Francisko mjini Vatican kwa kunogeshwa na kauli mbiu “Tunatoa matumaini ili kuanza upya.”

Jubilei ya Miaka 25 tangu kuanzishwa kwa Chama cha Nolite Timere
Jubilei ya Miaka 25 tangu kuanzishwa kwa Chama cha Nolite Timere

Baba Mtakatifu Francisko katika hotuba yake, amekazia umuhimu wa kumbukizi hii, ili kamwe watu wa Mungu wasiyasahau kamwe mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini Rwanda kunako mwaka 1994. Hiki ni kielelezo cha ushirikiano na mshikamano wa kidugu, kwani vita na biashara ya silaha ni mambo yanayowanyima watoto furaha ya maisha kwa kutoa huduma ya kiuchumi, kielelezo cha mshikamano na udugu wa kibinadamu unavuka mipaka ya umri, utaifa, utamaduni na hali ya mtu kijamii. Baba Mtakatifu Francisko anasema, mauaji ya kimbari yaliyotokea kunako mwaka 1994 nchini Rwanda, ni tukio ambalo linapaswa kukumbukwa na Jumuiya ya Kimataifa, ili kamwe, watu wasitumbukie tena huko.

Mshikamano wa udugu wa upendo na maskini
Mshikamano wa udugu wa upendo na maskini

Maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 25 tangu kuanzishwa kwa Chama cha “Nolite Timere” yananogeshwa na kauli mbiu mbiu “Tunatoa matumaini ili kuanza upya” kwa kuwapokea na kuwasaidia watoto yatima katika mpango maalum wa kuasili watoto. Itakumbukwa kwamba kuasili watoto ni mchakato wa kisheria ambao huhamisha uwajibikaji wa mzazi kutoka kwa wazazi wa kuzaliwa kwa mtoto kwenda kwa wazazi wao wa kuwalea. Huu ni mpango unaosaidia kuwapatia watoto yatima: fursa za masomo na malezi ya kiutu, kijamii na maisha ya kiroho. Baba Mtakatifu amewapongeza viongozi wa Kanisa na watawa wa Shirika la Masista wa Bizeramariya pamoja na mapadre wa Jimbo Katoliki la Kabgayi, nchini Rwanda. Huduma hii ni kielelezo cha mshikamano na ushirikiano wa dhati unaovunjilia mbali kuta za utengano, kwani huruma na upendo ni mambo yasiyokuwa na kizuizi na kwamba, ni kwa njia hii Chama hiki kimekuwa ni chemchemi ya upendo usiokuwa na mipaka na matumaini kwa leo na kesho iliyo bora zaidi. Vita pamoja na biashara ya silaha duniani inawaondolea watoto furaha ya kweli na kumbe, Chama cha “Nolite Timere” kinapenda kujikita katika kukuza na kudumisha mshikamano, urafiki wa kijamii, ushirika na mafungamano yanayodumu. Hiki ni kielelezo cha mshikamano na udugu wa kibinadamu unaovuka mipaka ya umri, utaifa, utamaduni na hali ya mtu kijamii.

Miaka 25 ya Chama Cha Nolite Timere
Miaka 25 ya Chama Cha Nolite Timere

Baba Mtakatifu Francisko anawaalika waamini na watu wote wenye mapenzi mema kuwaheshimu watu wa kujitolea wanaoendelea kusadaka: muda, vipaji, uzoefu na mang’amuzi mbalimbali kama sehemu ya mchakato wa ujenzi wa jamii inayosimikwa kwenye usawa. Watu wa kujitolea kwa njia ya huduma yao inayosimikwa katika mshikamano wa upendo wa kidugu kama sehemu ya mchakato wa ujenzi wa ulimwengu unaokita mizizi yake katika haki, amani, ustawi, maendeleo na mafao ya wengi ni muhimu sana katika ulimwengu mamboleo. Huu ni utajiri na amana kwa binadamu wote na chachu ya watu kutajirishana na kushirikishana muda, vipaji, uzoefu na mang’amuzi. Hii ni nguvu ya ujenzi wa jamii, kielelezo makini cha upendo na ukarimu. Baba Mtakatifu Francisko anawaalika waamini na watu wote wenye mapenzi mema kusali kwa ajili ya kuombea amani duniani kwani waathirika wakuu ni watoto, wanaoendelea kupoteza maisha, kudhalilishwa na kudhulumiwa haki, utu, na heshima yao. Kwa pamoja, Jumuiya ya Kimataifa inapaswa kukataa dhana ya vita!

Rwanda Mauaji ya Kimbari 1994

 

29 January 2024, 14:06