Meya wa Roma,Mkuu wa Mkoa wa Lazio na ujumbe wao wakiwa na Papa
Vatican News
Kama ilivyo desturi ya kila mwanzoni wa mwaka mpya, wa kutakiana heri,Baba Mtakatifu Francisko aliwapokea Meya wa Roma, Bwana Roberto Gualtieri, na Mkuu wa Mkoa wa Lazio, Bwana Francesco Rocca, katika mkutano uliofanyika tarehe 4 Januari 2024, katika Jumba la Kitume mjini Vatican. Mikutano hiyo ilifanyika tofauti, mwishoni mwa asubuhi hiyo iliyokuwa imejaa vikao ving vya Papa Francisko.
Gualtieri: mkutano wa kutia moyo sana
Katika akaunti yake ya Facebook, Bwana Gualtieri alielezea juu mkutano huo na Papa Francisko kama mkutano wenye msukumo wa kina: “Ilikuwa jambo la kufurahisha kumwonesha maendeleo ya kazi ya mipango mingi ambayo tumeweka kwa ajili ya Jubilei, kwa kukaribisha na kutunza watu walio dhaifu”, aliandika Meya wa Mji wa Roma
“Ninamshukuru Baba Mtakatifu kwa mafundisho yake, kwa kujitolea kwake bila kuchoka kwa walio hatarini zaidi na kwa maneno yake ya ukarimu ya kuunga mkono na kutia moyo.” Bwana Gualtieri tena kupitia jukwaa la kijamii: "Roma inampenda Askofu wake, ambaye anawakilisha vyema wito wake wa mshikamano, udugu na amani.”