2024.01.15 Papa na Uwakilishi Studium Biblicum Franciscanum 2024.01.15 Papa na Uwakilishi Studium Biblicum Franciscanum  (Vatican Media)

Papa akutana na wajumbe wa Chuo cha kifransiskani:Endeleza ushuhuda ulipoanzia ukristo

Jumatatu tarehe 15 Januari 2024 Papa Francisko alikutana na wajumbe wa Studium Biblicum Franciscanum iliyoanzishwa Yerusalemu miaka 100 iliyopita ambapo amezindua wito mpya wa amani katika maeneo matakatifu na ametualika kusali bila kuchoka.Endelezeni ushuhuda wenu ulipoanzia Ukristo.

Na Angella Rwezaula, Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu tarehe 15 Januari 2024 amekutana na Viongozi wa kitaaluma na wanafunzi, kutoka katika Chuo cha Mafunzo kifransiskani cha kibiblia (Studium Biblicum Franciscanum) kilichozaliwa huko Yerusalemu miaka 100 iliyopita. Katika salamu zake Baba Mtakatifu amewakaribisha na kumsalimia Patriaki, wa Yeruslemu, Kardinali Pierbattisita Pizzaballa.  Papa amesema kwamba wao wako Roma ambako mtume Petro aliwasili karibu miaka elfu mbili iliyopita, kuanzia, mwanzoni mwa kumfuata Yesu, kutoka katika nyumba ile ya Kapernaumu, kwenye Ziwa Tiberia, ambaye juu yake tunaweza kwenda na kusali shukrani kwa kazi ya subira ya maprofesa na wanaakiolojia wa Studium Biblicum Franciscanum. Papa aliongeza kusema: kwa “Sasa huwezi kwenda kwa urahisi kwa sababu eneo la vita linazuia.”

Papa alikutana na wajumbe wa Studium Biblicum Franciscanum
Papa alikutana na wajumbe wa Studium Biblicum Franciscanum

Chuo cha kifansiskani cha Mafunzo ya kibiblia (Studium Biblicum Franciscanum) kilizinduliwa huko Yerusalemu, kwenye Madhabahu ya Kupigwa mijeredi mnamo, tarehe 7 Januari 1924, na miaka michache baadaye kiliunganishwa na Chuo cha Mtakatifu Antonio cha  Roma, ambacho  sasa  ni Chuo Kikuu cha Kipapa cha Antonianum.  Baba Mtakatifu Francisko ameongeza kusema:"Ninachukua fursa hii kusema kwamba kuna vyuo vikuu vingi vya kikanisa Roma. Ni lazima mfikie makubaliano na kuunda aina fulani ya umoja: umoja katika mipango ya masomo... Mkubaliane na kuwa na mazungumzo." Kwa hiyo akiendelea alisema: Tangu wakati huo, historia yake daima imekuwa ikihusishwa na uwepo wa Ndugu Wadogo katika Nchi Takatifu. Leo, hii miaka mia moja baadaye, ningependa kukumbusha baadhi ya mantiki fulani.

Kwanza kabisa, ukweli kwamba Studium, pamoja na Maktaba na Makumbusho yake, imetoa na inaendelea kutoa msukumo wa uvumbuzi muhimu wa kiakiolojia katika maeneo mbalimbali, kufanya uvumbuzi wa thamani, hadi kufikia kupata, mnamo mwaka wa 2001, utambuzi wa (Facultas Scientiarum Biblicarum et Archaeologiae), yaani Kitivo cha Kisayansi cha kibiblia na Kiakiolojia. Hivi ndivyo upekee wao wa kuchanganya masomo ya Maandiko Matakatifu na kukaa kwao katika Mahali Patakatifu na utafiti wa kiakiolojia ulivyobainishwa; na hii imewaruhusu kupanua na kuimarisha kwa kiasi kikubwa programu na mbinu. Kwao upendo kwa maandiko ya Biblia umesimikwa katika wosia uleule wa Mtakatifu Francis, ambaye aliandika: “Watawa wale  ambao hawataki kufuata roho ya Maandiko ya kimungu wanauawa na barua, lakini badala yake wanataka kujua maneno tu  na kuwaeleza wengine.

Papa na wafranciskani
Papa na wafranciskani

Na wamehuishwa wale na roho ya Maandiko matakatifu ambao hawahusishi kila sayansi wanayoijua na kutamani kuijua kwa utu wao wa kimwili, bali wanairudisha kwa neno na mfano kwa Bwana aliye juu sana (Mawaidha, VII: FF 156).  Kwa Francis, ujuzi wa Neno la Mungu, na pia kujifunza kwake, si masuala ya elimu rahisi, bali uzoefu wa asili ya hekima, ambayo lengo lao la imani ni kuwasaidia watu kuishi Injili vizuri zaidi na kuwafanya kuwa wema.  Mwanafunzi mwaminifu wa Mtakatifu wa Assisi alielewa hili vyema: Mtakatifu Bonaventure wa Bagnoregio, ambaye wanajitayarisha kuadhimisha ukumbusho wake wa miaka 750 ya kifo chake. Katika Dibaji maarufu ya Breviloquium alisema, sambamba na mapokeo ya Wafransiskani, kwamba ili kukaribisha zawadi ya Neno la Mungu ni lazima “kumkaribia kwa imani rahisi Baba wa nuru na kusali kwa moyo wa unyenyekevu, kwa sababu Yeye, kwa Mwana na katika Roho Mtakatifu, atujalie utambuzi wa kweli wa Yesu Kristo na, pamoja na utambuzi pia upendo.”

Katika tukio la kuadhimisha miaka mia moja, Baba Mtakatifu Francisko amewasihi wasipoteze mtazamo wa aina hiyo kwa Maandiko. Uchunguzi wa kina na wa kisayansi wa vyanzo vya Biblia, ulioboreshwa na mbinu za kisasa zaidi na taaluma zinazohusiana, unaweza kwao daima kuunganishwa na maisha ya watu watakatifu wa Mungu na kulenga huduma yao ya kichungaji, kwa amani na kwa manufaa ya karama yao maalum katika Kanisa. “Kujifunza, kutafakari, kutafakari juu ya Biblia na maandiko ya Biblia, yote ndani ya moyo wa Kanisa, ambalo ni watu watakatifu, waaminifu wa Mungu wanaosonga mbele. Nje ya mwili wa Kanisa mafunzo haya hayana maana. Kilicho na thamani ni moyo wa Kanisa, wa Mama Mtakatifu wa Kanisa.” Papa alisisitiza. Baba Mtakatifu aidha aliwambia kuwa, katika wakati huu, ambao Bwana anatuomba tusikilize na kulijua Neno lake vyema zaidi, ili kulifanya lisikike ulimwenguni kwa njia inayozidi kueleweka, kazi yao ya busara na ya shauku ni ya thamani zaidi kuliko hapo awali.

Kardinali Pizzaballa akimsalimia Papa
Kardinali Pizzaballa akimsalimia Papa

 

Baba Mtakatifu amewahimiza, kwa hivyo, waendelea kuitekeleza na kuihitimu katika utafiti, ufundishaji na shughuli za kiakiolojia. Hali ya sasa ya Nchi Takatifu na watu wanaokaa ndani yake inatuhusisha na kututia uchungu. Ni mbaya sana kutoka kwa kila mtazamo. “Ni mbaya sana. Nilimsikiliza Padre Faltas, mambo aliyonijulisha; na kila siku ninawasiliana na parokia ya Gaza, ambapo wanateseka sana kutokana na hali hii. Hii ni mifano miwili tu, lakini hii yote ni kubwa zaidi. Hali ni mbaya sana.” Tunapaswa kuomba na kutenda bila kuchoka ili janga hili likome. Na hili liwe kichocheo zaidi cha ninyi kuzama ndani zaidi sababu na ubora wa uwepo wenu katika sehemu hizo za mateso, ya uwepo wenu huko, katika mauaji ya watu hao, ambayo imani yetu imekita mizizi huko.” Papa Francisko ameongeza kusema “Nini cha kusema kwa Wafransiskani? Asante kwa uwepo wenu katika Nchi Takatifu, asante! Na msonge mbele kwa ujasiri. Asante kwa kila kitu mnachofanya! Ninawabariki kutoka ndani ya moyo wangu. Na ninapendekeza kwamba msisahau kuniombea. Asante.” Papa Francisko amehitimisha.

Papa na wajumbe wa Studiium Biblicum Franciscanum
15 January 2024, 17:09