Tafuta

2024.01.16 Kardinali Sergio Sebastiani ameaga dunia tarehe 16 Januari 2024 akiwa na umri wa miaka 92. 2024.01.16 Kardinali Sergio Sebastiani ameaga dunia tarehe 16 Januari 2024 akiwa na umri wa miaka 92. 

Papa ametuma salamu za rambi rambi kufuatia na kifo cha Kardinali Sergio Sebastiani

Kardinali Sergio amefariki tarehe 16 Januari,Roma akiwa na miaka 92.Alichaguliwa kuwa Kardinali na Mtakatifu Yohane Paulo II,Februari 2001.Alishika nyadhifa:Rais wa Sekretarieti ya Uchumi kwa zaidi ya miaka 10.Balozi:Amerika Kusini,Ufaransa,Madagasar,Mauritius na Uturuki.Katibu mkuu wa Kamati ya Jubilei ya 2000.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko Jumanne tarehe 16 Januari 2024 ametuma salamu za rambi baada ya kupata taarifa za kifo  cha Kardinali Sergio Sebastiani na ambaye ameugua kwa muda mrefu. Salamu zake zimetumwa kwa kaka yake Luciano Sebastiani ambapo Baba Mtakatifu katika telegramu hiyo, “anaelezea salamu zake za rambi rambi kwake na familia yake, ikiwa ni pamoja na Jimbo Kuu la Fermo ambapo alikuwa ni Padre mwenye bidii.”  “Katika nuru ya imani, Papa - anamshukuru Mungu kwa ushuhuda wa marehemu huyo Kardinali ambaye alitumia maisha yake kwa ukarimu katika huduma ya Injili pamoja na watangulizi wake wengi ambao walimkabihdi majukumu muhimu, hadi nafasi ya kuwa Rais wa Sekretarieti ya uchumi Vatican.”

Kardinali Sergio Sebastiani ameaga dunia akiwa na miaka 92
Kardinali Sergio Sebastiani ameaga dunia akiwa na miaka 92

Baba Mtakatifu aidha anamkumbuka marehemu “kama Katibu mkuu wa Kamati  kuu ya Jubilei ya mwaka 2000 aliyojikita nayo hasa katika maandalizi kwa nyayo za Mtakatifu Yohane Paulo II kwenye barua yake ya kitume ya Tertio Millennio Adveniente (iliyokuwa na lengo la maandalizi ya Jubilei ya mwaka 2000.) Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu Francisko “anainua sala zake kwa ajili ya roho ya mtumishi mwema na anayekesha ili kwa kusindikizwa na Bikira Maria, apokelewe katika karamu ya milele mbinguni” na amefanya hivyo kwa “kutuma baraka yake kwake yeye, watawa ambao walimsindikiza kwa upendo huku wakimhudumia na wale wote ambao wanashirikiuchungu wa kuondoka kwake.”

Mazishi Jumatano 17 Januari 2024 saa 8.30 alasiri katika Kanisa kuu la Mtakatifu Pietro

Mazishi ya Kardinali Sergio Sebastiani yataadhimishwa Jumatano, tarehe 17 Januari 2024, saa 8:30 mchana, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, kwa kuongozwa na Kardinali Giovanni Battista Re, Dekano wa Baraza la Makardinali kwa ushirikishi Makadinali waliopo Roma, maaskofu wakuu na maaskofu, mapadre na waamini. Na mwishoni mwa Maadhimisho hayo ya Ekaristi, Baba Mtakatifu Francisko ataongoza maombi ya mwisho na kumpa burihani marehemu. Kufuatia na kifo cha Kardinali Sergio Sebastiani (11.04.31, Italia). Baraza la Makardinali limeundwa sasa na Makardinali 239 miongoni mwao 132 wakupiga kura na 107 siyo wa kupiga kura.

Mtumishi wa Mungu Kardinali Sergio Sebastiani apekelewe mbinguni kwa amani
Mtumishi wa Mungu Kardinali Sergio Sebastiani apekelewe mbinguni kwa amani

Kardinali Sergio Sebastiani alizaliwa tarehe 11 Aprile 1931 huko  Montemonaco, Fermo na baada ya majiundo yake ya jandokasisi, alipewa daraja la ukuhani mnamo tarehe 15 Julai  1956 na Askofu Mkuu Norberto Perini. Aliteuliwa kuwa Askofu mkuu tarehe 27 Septemba 1976 na Papa Paulo VI na kuweka wakfu wa kiaskofu mnamo tarehe 30 Oktoba 1976 na Kardinali Jean-Marie Villot. Aliundwa kuwa katika baraza la Makardinali mnamo tarehe 21 Februari 2001 na Papa Yohane Paulo II.

Majukumu  mengine ya utume wake

Kardinali  Sergio Sebastian aliyefariki akiwa na miaka 92 alishika nyadhifa mbali mbali za kanisa na hasa kwa uzoefu wake wa kidiplomasia kama Balozi wa Kitume huko Madagascar na Visiwa vya Mauritius (1976-1985), Balozi wa kitume Uturuki (1985-1994), Amerika Kusini, Ufaransa, Katibu Mkuu wa Halmashauri Kuu ya Jubilei ya Mwaka Mtakatifu 2000 (1994-1995),Katibu Mkuu wa Kamati ya Jubilei ya Mwaka Mtakatifu wa 2000 (1995-1997), Rais wa Peregrinatio ad Petri Sedem(1996-1997), Rais wa Sekretarieti ya Kiuchumi ya Vatican (1997-2008) na hatimaye baada ya kustaafu amekuwa Kadinali shemasi na kuhani wa Mtakatifu Eustachi kuanzia (2001- hadi 2024 mahali ambapo mauti yamemfikia.

Salamu za Papa za rambi rambi kufuatia na kifo cha Kardinali Sergio Sebastiani

Imesasishwa saa 11.23 jioni 17 Januari 2024

16 January 2024, 16:41